Chadema raha

Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,897
4,620
Kwa kweli mimi sio mwanasiasa lakini ni mwanajamii anaeshiriki moja kwa moja mafanikio ama maangamizi ya taifa.

Kama kutakuwa na shule bora, hospitali bora, nishati bora, maji safi nk ni unafuu wangu wa maisha yangu binafsi na kama ni kinyume chake ni msiba wangu binafsi kama ilivyo hivi sasa chini ya serikali ya sisiem.

Hivyo kwa jinsi nilivyowashuhudia Chadema jangwani leo hii nimejiridhia kuwa ukombozi wangu na watoto wangu upo mlangoni na hakuna mwenye ubavu wa kuuzuia tena.

Hivyo ninalotaka kusema ni hile NINA FURAHA SANA NIMETUMA MCHANGO WANGU CHADEMA KUPITIA MPANGO WA M-PESA WALIOZINDUA LEO. JIBU NILILOPATA NI HILI ''G93ZR300 IMETHIBITISHWA Tsh,..... IMETUMWA KWA CHADEMA KWENYE AKAUNTI NO, .... TAREHE 26/5/12 SAA 8:48PM''

Nimefurahi sana kuwa mmojawao wa wenye kuchangia ukombozi wa mlalahoi. Wewe je utataka kuwa mmoja wao?
.
 
Wakichangisha wananchi wanasema kwa niNi wanatumia kampuni ya vodacom,hawa magamba roho zinawauma sana.Nyerere alisema haya madini tuyaache hadi tutapokuwa na uwezo nayo, wakampuuza. Pia aliwaambia nimeangalia vyama vyote nimeona CHADEMA ndo chama makini. Pamoja tutashinda ile nyomi ya jangwani leo si mchezo, hakuna cha fujo wala vuguru mkutano umeisha safi na baraka ya mvua.
 
Weka hiyo account # hapa na wengine tuweze kuwakilisha michango yetu.
 
chadema rahaaa, utamuu. Yan ukiwa ndan ya chadema raha yake haielezeki.
 
Weka hiyo account # hapa na wengine tuweze kuwakilisha michango yetu.

Comrade fanya hivi usipate taabu *150*00# menu ya M PESA then ukiisha kuisoma menu kwenye kuweka namba utaweka 111333 namba ya siri ni namba yako ya simu ndio ivo tu
 
W. J. Malecela, uliniahidi utakuja jangwani Mkuu wangu. Vipi mbona hukutokea? Au Baba yako amekukataza? Kung'ang'ani itikali ya kisa ni ya Baba ni sehemu ya ujinga. FUNGUKA

TUMBIRI,
tumbiri@jamiiforums.com

Ule umati kweli unaweza kumwona mtu! we rafiki watania sana.Kova kaogopa kivuli chake hakuna cha fujo wala vibaka. Leo
CHADEMA SQUARE palikuwa na raha ajabu, ila Bananga naye yumo kama Sugu. Kweli Lema ana majembe Arusha.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu baada ya kuachana pale na msafara wa makao makuu, nkapata kampan kuna kikundi kilikuw kinapg mchakamchaka kwa nyimbo nzuri na bendera za kutosha 2kaliunga mpaka ubungo hapo da leo nalala nkiwa na aman tele
 
wataongea mengi sana hawana la kusema. yan mpaka REJAO NA RTTZ WALIKWENDA KWENYE MKUTANO, WALIONGEZA IDADI.
 
Wakuu baada ya kuachana pale na msafara wa makao makuu, nkapata kampan kuna kikundi kilikuw kinapg mchakamchaka kwa nyimbo nzuri na bendera za kutosha 2kaliunga mpaka ubungo hapo da leo nalala nkiwa na aman tele

.
Dar ni watu wanao ogopa mvua sala ila leo kwa raha ya chama chao Chadema kiliyowapa hawakujali kabisa kunyeshewa wakati wa matembezi yao kurudi makwao.
.
 
wataongea mengi sana hawana la kusema. yan mpaka REJAO NA RTTZ WALIKWENDA KWENYE MKUTANO, WALIONGEZA IDADI.

RITZ NA REJAO walitegemea pale pana porojo kumbe ndivyo sivyo na hisia zao, wakakuta kauli za maana na ufafanuzi bora mfano daktari kamili kasema chama kinapinga posho za kibaguzi( sitting allowance).Alisema walimu na watumishi wengine hawana standing allowance? Hapo unategemea watakuja na hoja gani? Inawabidi wakae kimya.
 
weka hiyo account # hapa na wengine tuweze kuwakilisha michango yetu.

*150*00# namba ya kampuni 111333 umemaliza kaka, fanya hivyo mara nyingi uwezavyo ili m4c iendelee hadi 2015
 
JINSI YA KUTUMA PESA KWA VODACOM M-PESA KUCHANGIA CHADEMA KWA M4C


*150*00# Ok!...........>pay bill............>enter business no(111333)............> enter reference no.( your mob.no.)............>Amount ...........>enter PIN......>enter 1. to comfirm.........>ok!
 
mimi binafsi sikwenda ila nikisoma nakuona watu walivyojitoa kwa moyo inafurahisha sana jamani ama kweli tunaweza kunufaika na rasilimali tulizokuwa nazo hapo baadae Mungu nibariki CHADEMA Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom