CHADEMA njooni kijiji cha Old Shinyanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA njooni kijiji cha Old Shinyanga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by komredi ngosha, May 1, 2012.

 1. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  habari jf,
  nipo kijiji cha Old Shinyanga, kilichopo manispaa ya Shinyanga mjini kwa muda wa siku mbili sasa. Nimekuta uozo wa hali ya juu, ubadhirifu mkubwa wa mali za wananchi na kukosekana uongozi wenye tija.
  kijiji hiki kina mwenyekiti kutoka CCM, diwani wa CCM na mbunge wa CCM bwana Masele. Hapa ndio ngome ya CCM jimbo la Shinyanga mjini lakini watu wameanza kuchoshwa na chama chao kwa kua viongozi hao wamekua mapazia tu. Baadhi ya tuhuma wanazopewa ni kama ifuatavyo:
  1. Mwenyekiti wa kijiji hajawahi kufanya kikao kuwasomea wananchi ripoti ya mapato na matumizi kwa zaidi ya miaka miwili
  2. Mwenyekiti na Diwani wake wanatuhumiwa kula fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo
  3. Mwenyekiti, diwani na katibu mwenezi wa ccm wa tawi kijijini hapa wamepatikana na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya wizi, kwa kukubali kupewa rushwa na vikundi vya majambazi waweze kufanya uhalifu wao mpaka wananchi wameamua kuchukua hatua mkononi
  4. Ahadi hewa za mbunge masele

  kinachowaumiza wengi, chadema haijaamua kupiga kambi hapa hua inabip tu hata ofisi ya chama haipo. Chonde chonde makamanda wa chadema shinyanga mjini tuwasiliane watu wanahitaji ukombozi !
   
Loading...