Kwa maelezo uliyotoa hapa, najiuliza hasa umuhimu wa CHADEMA utakuwa upi kwetu sisi wananchi na hata kwa serikali? CHADEMA isiyoweza kushindana kwa lengo la kuibadili CCM madarakani haitakuwa na maana yoyote kwetu. Ni heri ing’atuke tu.
Halafu, umesifu harakati za Mwembe Yanga. Sijui kama umejiuliza kuwa lugha aliyotumia Dr. Slaa kumuelezea Kikwete na serikali yake wakati ule ingechukuliwaje ingekuwa katika utawala huu wa JPM? Elewa kuwa ile CHADEMA iliyokukosha wakati ule iliyokuwa na jeuri ya kuchapisha orodha ya mafisadi akiwemo Rais kama kiongozi wa mafisadi papa iliwezekana wakati ule. Leo hii Mchapishe JPM kivile halafu umtangaze pale Mwembe Yanga kama fisadi uone upepo utakavyokuvumia.
Uko sahihi kwa kiasi fulani kwamba CHADEMA “ile” ndiyo iliyochagiza ujio wa Magufuli CCM. Na Magufuli sio mjinga kuachia ile CHADEMA iendelee na mambo yake. Moto wake anaujua. Ile kushika hatamu tu, kapiga marufuku “siasa huria”, maandamano, Bunge live na kudhibiti media zote kutangaza habari za upinzani huku yeye akifanywa newsmaker mkuu. Kajaza polisi wa kufuatilia mazungumzo ya watu n.k.
Kwa kifupi ni kuwa Magufuli haitaki kabisa CHADEMA “iliyofanikisha” ujio wake madarakani. Kwake, “vyama rafiki” ni km UDP, TLP, UMD na NRA. Naona maelezo yako hapa yakizingatiwa na Mbowe kikamilifu, basi CHADEMA itatimiza sifa zote za kuwa “chama rafiki” kwa CCM.
Kwa vile tayari tuna vyama rafiki vya kutosha na Magufuli tayari yupo anatekeleza ajenda/ilani zote kama unavyodai na hatuna gerentii kwamba “vichaa” ndani ya CHADEMA watatulia, itakuwa vyema ukishauri CHADEMA kianze mchakato wa kujifuta (disband). Kimeshakamilisha umuhimu wake. Kama huo SIO mtizamo wako ni bora utuelimishe kama kuna kitu cha kipekee CHADEMA kinaweza kufanya tofauti na vyama vingine vilivyopo.