CHADEMA, nini sasa kwenda mbele?

CHADEMA, nini sasa kwenda mbele?

TOMNOTKAT

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2013
Posts
836
Reaction score
1,080
Mwamba ana mzigo mzito kipindi hiki. Anatakiwa afanye maamuzi magumu ambayo yatakuwa kufa au kupona kwa Chadema.

Wakubali, wakatae, huu uchaguzi umekwisha na hakuna vikwazo wala matamko ya wazungu yanayoweza kubadili matokeo. Na hakuna mzungu yeyote anayeweza kutuporomeshea mabomu kila Chadema au Lissu. Hatuna kitu muhimu chakutosha, kufanya wazungu wakianzishe. Na Chadema wakifanikiwa kuwekea serikali vikwazo, watakao umia zaidi ni wananchi ambao Chadema itarudi kuwaomba kura.

Ukweli ni kuwa Chadema ilituvutia wengi sana enzi zile za Mwembe Yanga, na ni ile Chadema ndo ilikuwa chagizo kutufikisha hapa tulipo. Kutuletea Magu.
Kwahiyo kwa wanaojinasibu na utendaji wa Magu (ambao kiukweli amejitahidi kutekeleza ilani yao iliyopita), wasisahau kuwa utedaji huo uliuchagizwa na Chadema ya Mwembe Yanga.

Nini sasa hatma ya hiki chama, kilichoikomboa Tanzania toka mikononi mwa wanaccm wachache?

Maamuzi ya Mbowe ya sasa, yatakuwa na umuhimu mkubwa sana kwa hatma ya Chadema kama chama cha siasa zenye ushawishi nchini.

Ushauri wangu:

1.) Aruhusu akina mama waende bungeni kupitia viti maalum ili sera zao zipate nafasi ya kusikika kwa hii miaka 5. Wakipotea kabisa hewani, itawabidi
2025 waanze kujinadi upya. Wachaguwe tu wanawake makini. Sio wakwenda kufanya fujo. Iwe kwamba, wakisimama kuongea, wasikilizaji tubaki tunaongelea hoja waliyoitoa na sio wao kama personality.
Isitoshe, Chadema inahitaji hiyo ruzuku ili iendelee kujiendesha. Haiwezi kutegemea misaada ya wazungu tu 100%. Isitoshe inasemekana wafadhili wenyewe
wameaminishwa na Lissu, pesa yao haiko salama ikipelekwa kwenye chama moja kwa moja, ni lazima ipitie kwake. Sasa uendeshaji wa chama kwa kusubiri allowance
toka Ubelgiji kwa TL, itakuwa shughuli, na Mwamba analijua hili.

2.) Uongozi mkuu wa Chadema ujiuzuru. Chadema inahitaji kuleta uongozi mpya, uliosoma ili ibadili aina ya siasa inazofanya. Na kutumia akina Boni kama
injini ya chama, haisaidii. Maana watakuwa wanaendelea kutumia nguvu na fujo badala ya akili.
Chadema inahitaji busara sana kwenye uongozi wake, na viongozi wanye nia nzuri na siasa za chama, sio manufaa yao binafsi.
Mwamba lazima awe na uhakika na madhumuni ya viongozi wanaomzunguka.(Ukiangalia movie ya Tundu Lissu kwenye huu uchaguzi, ni kana kwamba
Chadema ilikuwa inafanya kazi kutimiza malengo ya Lissu, na sio Lissu, kufanya kazi kutimiza malengo ya Chadema).

3.) Mbowe aendelee kumtilia shaka Zitto Zuberi Kabwe. Mbowe hajawahi kumuamini Zitto tangu amfukuze kwenye chama chake, na asitegemee kuwa Zitto yule amebadilika.

4.) Mwamba kama mtu mzima, akubali yaishe. Nilishawahi kushauri hili huko nyuma kabla ya uchaguzi. Ile kauli ya Mwamba ya 2016 kuwa Jiwe watamchinjia baharini, ilimkera
mlengwa na alishasema hivyo wazi. Alisema hawezi kukaa na mtu aliyesema wakamchinjie baharini.
Namsihi aombe kuonana na mkulu kwa njia yakusema wanataka maridhiano, aombe radhi kiutu uzima yaishe.
Sote tunamjua Mkulu alivyo kiburi. Mwenye akili timamu asitegemee mkulu ndo awaite kutafuta maridhiano nao. Wahenga wanasema, mkubwa hakosei. Sasa huyu tumtake, tusimtake
ndo mkuu kwa sasa. Chadema hawawezi shinda vita ya NANI ZAIDI?!!
Wakubali yaishe, ili waanze kukijenga chama chao upya.

5.) Chadema ichukuwe tahadhari na hawa washauri wao ambao ni wanaharakati na celebrities wa mitandaoni. Wajiulize nini malengo yao? Wengi wao, harakati zao za mitandaoni
ndo zinazowaweka mjini. Hata yule dada mwenye mdomo mchafu, matusi ndo yanayompa traffic, traffic ya clicks ndo inampa kula. Sio kwamba anafanya afanyavyo sababu ya
mapenzi yake kwa Chadema. Wengine chuki zao kwa CCM ni zakulazimisha ili waendelee kuwepo mjini.

Je, Chadema inataka kujihusisha na watu wa aina gani? Na mambo ya aina gani?

Kila lenye heri kwa Chama hiki Muhimu nchini ✌🏿✌🏿✌🏿✌🏿✌🏿✌🏿✌🏿✌🏿✌🏿✌🏿
 
Awamu ya Kikwete iliruhusu demokrasia ndio maana hadi wewe leo unayakumbuka ya Mwembe yanga!Slaa yule angekuwa ndio anafanya yale kwenye utawala huu basi angeshatangulizwa mbele za haki zamani sana!

Awamu hii sio kwamba hakuna ufisadi ila hakuna uwazi na wanaojaribu kuongea wanashughulikiwa ipasavyo!Hebu angalia manunuzi yanavyofanywa kinyemela na CAG amepigwa pini kukagua sehemu zenye miradi nyeti na manunuzi makubwa kama ATCL,kuna nini hapo?

Kama tutawekewa vikwazo basi na iwe hivyo wote tuumie pengine akili zitaturudi!
 
Tatizo mindset ya mbowe ni kupiga pesa Kwa kupitia chama , Yes ...he managed to make huge cash violently , but now the honeymoon is over , kukigeuza chama kuwa chama cha ukombozi ni ngumu inahtaj mass support with multiple fierce fighting, kibongo bongo ni ndoto za alinacha ....mwenye roho hyo ni Lisu tatizo people's are too innocent to couple the situation .....
 
Awamu ya Kikwete iliruhusu demokrasia ndio maana hadi wewe leo unayakumbuka ya Mwembe yanga!Slaa yule angekuwa ndio anafanya yale kwenye utawala huu basi angeshatangulizwa mbele za haki zamani sana!
Awamu hii sio kwamba hakuna ufisadi ila hakuna uwazi na wanaojaribu kuongea wanashughulikiwa ipasavyo!Hebu angalia manunuzi yanavyofanywa kinyemela na CAG amepigwa pini kukagua sehemu zenye miradi nyeti na manunuzi makubwa kama ATCL,kuna nini hapo?
Kama tutawekewa vikwazo basi na iwe hivyo wote tuumie pengine akili zitaturudi!
Vikwazo kamwe haviumizi wote na serikali hii haifanyi biashara sana na nchi za Magharibi za kuithiri ipasavyo kwa vikwazo. Angalia mwenendo wa Magu tangu 2015 kwa wamagharibi na mashariki. Vikwazo havita tatua chochote na Chadema haitanufaika navyo.

Pamoja na maumivu waliyonayo Chadema, ni muda wakutumia akili hata za kuazima na sio hasira kwenye kufanya maamuzi.
 
Basi na hivyo vikwazo vije tuone kama ni kweli hatutaathirika!Wakisema tu tujinunulie ARV wenyewe tutatafutana!Huyo China ambaye tunajidai naye yeye anachangia kiduchu sana kwenye bajeti yetu tegemezi

EU na US wakisema wakate mrija basi ujue bajeti itakuwa na hali ngumu kutekelezeka ukizingatia mikopo mikubwa mikubwa tuliyonayo ambayo kila mwaka tunatenga fungu kulipa!

Vikwazo vikifanya hali ya watu kuwa mbaya huenda serikali ikajirudi na kuacha demokrasia itamalaki!Na hapo ndipo upinzani utanufaika kwa haki kutendeka kwenye chaguzi na utekelezaji wa majukumu yao ya kisiasa!
 
Awamu ya Kikwete iliruhusu demokrasia ndio maana hadi wewe leo unayakumbuka ya Mwembe yanga!Slaa yule angekuwa ndio anafanya yale kwenye utawala huu basi angeshatangulizwa mbele za haki zamani sana!
Awamu hii sio kwamba hakuna ufisadi ila hakuna uwazi na wanaojaribu kuongea wanashughulikiwa ipasavyo!Hebu angalia manunuzi yanavyofanywa kinyemela na CAG amepigwa pini kukagua sehemu zenye miradi nyeti na manunuzi makubwa kama ATCL,kuna nini hapo?
Kama tutawekewa vikwazo basi na iwe hivyo wote tuumie pengine akili zitaturudi!

Slaa siyo shamba amesoma na kuelimika.
Tatizo ujinga na shule elimu zenu zinawafanya msiambilike.
Kufulieni mbali.
 
Tulishasema zamani baada ya kuona mwelekeo kuwa huyu bwana chama KITAMFIA mikononi, sasa ndo hivyo kama mlivyosikia chama kimeambulia kiti ki 1 tu. Sasa huko si kama ndo kufa kwenyewe....!
 
Hiyo ishu viti maalum kwenda bungeni mbona wanachama walishakataa chadema ikikubali kuingia kwenye mtego huo itakuja kuwa kama tlp
 
Mi-ccm inapougulia nyongo kwa ajili ya CDM kuliko CDM yenyewe ndipo penye maajabu ya firauni.

Mmeshaambiwa tochi batteries hazichangwi na magunzi mmeng'ang'ania viti maalum. Si mwende nyie?

Tulipo tunasubiri ya California na uraya uraya pale Dar na hasa kuwa Kawe ya Schwarzenegger
 
CCM hawaeleki walisena hawataki upinzani wakawatumia NEC polisi na TISs kuvuruga uchaguzi, alafu wameona wamefanya upuuzi wanarudi upya kuishauri chadema,

Magufuli ndo atuombe wananchi msamaha vinginevyo hakuna litakalofanikiwa awamu hii
 
Basi na hivyo vikwazo vije tuone kama ni kweli hatutaathirika!Wakisema tu tujinunulie ARV wenyewe tutatafutana!Huyo China ambaye tunajidai naye yeye anachangia kiduchu sana kwenye bajeti yetu tegemezi!EU na US wakisema wakate mrija basi ujue bajeti itakuwa na hali ngumu kutekelezeka ukizingatia mikopo mikubwa mikubwa tuliyonayo ambayo kila mwaka tunatenga fungu kulipa!
Vikwazo vikifanya hali ya watu kuwa mbaya huenda serikali ikajirudi na kuacha demokrasia itamalaki!Na hapo ndipo upinzani utanufaika kwa haki kutendeka kwenye chaguzi na utekelezaji wa majukumu yao ya kisiasa!
Soma kwanza uelewe mada ndipo ujibu. Acha kukurupuka
 
Slaa siyo shamba amesoma na kuelimika.
Tatizo ujinga na shule elimu zenu zinawafanya msiambilike.
Kufulieni mbali.
Tunasubiri utujengee shule, ulituahidi kabla hujaenda kuwa Yaya huko canada
 
Mbona mataga mnaumia Sana wakat haya mliyataka wenyewe??. Kaeni bungen wenyewe tuone mnapoipeleka nchi
 
Back
Top Bottom