Ndugu wana JF Great thinkers,
Natamani sana kuiona Tanzania ikipata ukombozi wa pili wa kiuchumi,Ni aibu kuwa na Tanzania maskini kiasi hiki pamoja na ukweli kuwa imejaliwa kuwa na raslimali lukuki ambazo kama tungezitumia vizuri tungekuwa tunaelea kwenye dunia nyingine kabisa kiuchumi. Lakini kwa miaka mingi ijayo kama hali ikiendelea hivi sioni mwanga wa kuiona Tanzania hiyo.
Nimekuwa nikifuatilia mambo ya kisiasa yanayoendelea huko nyumbani Tanzania na nimejiridhisha kuwa dhamira ya wanasiasa kutufikisha kwenye nchi ya maziwa na asali ni ndogo sana (upende usipende kunauhusiano mkubwa sana kati ya politiki na maendeleo ya nchi). Vyama vya siasa CCM,CDM,NCCR , CUF etc ukiviangalia kwa jicho la tatu havina mkakati wowote wa kututoa kwenye tope tulilonasa kidogo Chadema wameanza kuonyesha mwanga lakini nadhani wanabidi kujipanga zaidi na kufanyia kazi udhaifu wao mbalimbali ambao mara kadhaa umeahinishwa humu ndani. Lakini kwa sababu ya hasira kali ambayo watu wamekuwa nayo dhidi ya CCM yeyote anayetoa hoja ya kusahihisha mambo ndani ya CDM anaonekana mbaya sana na anatumika,mimi napenda kuwahakikishia sio kweli,tujifunze kuvumiliana na kusikilizana linapokuja suala la nchi, wengine tumeweka utaifa mbele siasa baadae sana.
CDM kama chama ambacho kimebeba matumaini ya wa Tanzania,inabidi mara kwa mara kijitathmini na kuweka mikakati au kueleza mikakati itakayotumia katika kutufikisha nchi ya asali,kwa mfano waTanzania tungependa kujua Chadema kitaendesha nchi kwa mfumo upi? Ujamaa?Ubepari?Free market socialism?.Tungependa kufahamu mkakati mlionao wa kuvuna madini(gas) yetu?mtawekeza kwenye mitambo ili tuvune wenyewe?au mtaboresha mikataba? na mambo mengine mengi ambayo Great thinkers watayaongeza
CDM iache kabisa kucheza Ngoma ya CCM,Eti Mh Zitto ni msaliti?hamuoni kuwa huo ni mkakati wa kitoto kabisa wa kuwagawa?na kuna watu humu JF wameaminishwa kiasi kwamba jina la Mh ZZK likitajwa humu wanajisikia kufakufa,hapana nadhani ni muhimu tuwejuu zaidi ya hapo Zitto ni Jembe la maana sana kama ilivyo kwa Mnyika,Msigwa na nina amini sana kwa aina ya siasa ambayo Zitto anafanya ( misimamo kwenye mambo ya msingi ya Kitaifa) ya kushindana kwa hoja.
CDM kama inavyojipambanua iwekeze katika kuonyesha kivitendo demokrasia ndani ya chama,tunapoelekea kwenye uchaguzi wa ndani natamani viongozi wote kwenye ngazi zote wapatikane kwa demokrasia na kusiwepo kunyosheana vidole pale mtu asiyetegemewa kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi yoyote ndania ya chama,wale ambo wamepost humu wakionyesha majina ya wapendwa wao nadhani ni mitazamo yao tu na kamwe isichukuliwe kama misimamo ya chama.
CDM haiwezi kuleta ukombozi kwa watanzania hata ikichukua dola kama ikiendesha mambo yake kwa kujilinganisha na CCM (ambayo kwa matazamo wangu wameshafanya kazi yao kuleta uhuru wa kisiasa wawaachie wengine waendeleze pale walipoishia),CDM ni chama cha .com lazima kiwe na vision na mtazamo tofauti kabisa na mkongwe CCM,lazima kiwaze na kuweka mikakati mikubwa na si kuzungumzia mambo kijumla jumla lazima muwe specific na kwenye M4C hayo ndio muwaeleze wananchi bila kusahau na kuwatia hasira kwa issue za ufisadi nk
Nina mengi lakini kwa sasa inatosha labda niwaombe wanajf wenzangu,tusiende nje ya msatari badala ya kuwa Great thinkers tunakuwa shallow thinkers kwa kuendekeza matusi na majungu ambayo kwangu mimi naona hayajengi zaidi ya kufanya watu makini kukimbia JF na kuacha kutoa hoja zao nzuri za kujenga CDM na kwa msatakabali wa nchi yetu.
Ciao