Chadema ni Washindi Siku Zote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema ni Washindi Siku Zote

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Goodrich, Apr 2, 2012.

 1. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Naona baadhi ya wana JF wanajaribu kujiuliza kilichoiangusha CCM Arumeru. Ukweli ni kuwa hata hizo kura chache walizopata CCM wamejitahidi sana. Mara nyingi ushindi wa CCM hutokana na hujuma, kununua mawakala, rushwa, kucheza na daftari la kura, vitisho na matumizi makubwa ya nguvu na rasilimali za serilali/umma. Arumeru Chadema wameweza kudhibiti mambo hayo japo sio kwa 100%. Ushindi wa Chadema hautokani na kupiga kura, bali kulinda kura. Ni kwa mantiki hiyo, naweza kusema kuwa Chadema huwa wanashinda siku zote. Walishinda Uraisi, walishinda Ubunge kwa Pinda, walishinda Segerea, walishinda Kibaha kwa Koka, walishinda zaidi ya 70% ya majimbo ya Tanzania na hata Igunga naamini walishinda. Tatizo ni kulinda kura. Ili hili lifanikiwe, sasa tuelekeze nguvu kwenye Katiba mpya, itupe tume huru ya uchaguzi. Viva CHADEMA.
   
Loading...