Daudi Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 327
- 204
Na ndicho kinafuata,wakishapata idadi wanayoitaka ni katiba kurekebishwa hadi miaka saba ya uchaguz badala ya mitano na hatimae wataondoa ukomo wa uraisi na hapo ndiyo umilele uliotamkwa utatimia. Hakutamka bahati mbaya. Hili gulio lina malengo ya mbali sana. ILA UPINZANI UKIFA TUTASAGA MENO WATANZANIA. Hizi shangwe na ushabiki ni za muda tu.muda si mrefu tutaongea lugha moja.Chama cha Siasa kina lengo moja tu-nalo ni Kupata madaraka. Swali je makada wa CDM kununuliwa na CCM kunaisaidia CDM kushika madaraka? Kama hili halisaidii ina maana CDM inadhoofishwa (kiuwezo na kimuonekano) na CCM. Hivyo CCM wanauwa ndege wawili kwa jiwe moja (1) wanawapata hao tunaosema "wameiva" na (2) wanaivuruga na kuidhoofisha CDM. Kuendana na hili CCM wengi wameanza kuimba wimbo wa MBOWE aondolewe na hili linaweza kuleta sintofahamu ndani ya CDM kama hawakuwa makini.
Upinzani dhaifu au bila upinzani CCM watafanya yale yale yaliyomfanya kiongozi wao aseme CCM inahitaji upinzani na tutaendeshwa kama tairi bovu. Watatafuna nchi kama hawana akili nzuri.
hiki ni kilio cha samakKama machali wanampa ukuu wa wilaya, Shonza - unaibu waziri siku wakimpata Lissu watampa uwaziri mkuu au urais kabisa! Ccm wanajua upinzani kuna watu makini sana ila kiburi tu!