mwiba, rejao, ritz, na yule sijui shoga nani tena... Hamuisaidii serikali iliyoko madarakani kwa style za propaganda uchwara... Watu watanzania wataihukumu ccm kutokana na deliverables;
1. Huduma bora za afya mnazitoa?
2. Maji safi na salama inapatikana?
3.elimu bora zinatolewa kwa watoto wetu?
4.mmeweka miundo mbinu bora kwa maendeleo ya taifa?
5. Mmesimamia vipi dhahabu, gas, almasi, uranium, nickel, tanzanite zetu kwa faida ya umma?
6.wakulima, wavuvi na wafugaji wamefaidikaje kutokana na juhudi zao za kujiletea maendeleo?
7.viwanda vyetu viko wapi?
8.wafanyakazi mishahara yao zinakidhi mahitaji yao
9.maliasili na vivutio vya utalii vimeinufaisha vipi nchi? Kwa kiasi gani? Kwanini?
10. Kwanini mnauza ardhi yetu?
11. Kwanini mnalindana ktk ufisadi wa wazi???....
12. Mmewasaidia vipi wakulima wa pamba, kahawa, korosho nk wasiendelee kunyonywa?
Hivi ndiyo vitu vinanvyopaswa kutolewa majibu na ccm ... Otherwise watanzania hawatawaelewa ifikapo 2015 kwani shule za kata zinasaidia kueneza elimu ya uraia kwa kasi hadi kule kunako nyumba za tembe....