CHADEMA ni chama cha Amani na Ustaarabu

CHADEMA ni chama cha Amani na Ustaarabu

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,063
Siyo siri kuwa Chadema kimepitia katika dhuluma na manyanyaso yasiyo kifani kutokea kwa mamlaka:

1. Hivi karibuni mwenyekiti wake amekuwa kizimbani kujibu mashtaka yasiyokuwa na kichwa wala miguu.

2. Makamu mwenyekiti wake leo ni manusura (wa shambulio baya kabisa) ukimbizini Ulaya, kuyaepusha maisha yake kutoka hatarini.

3. Wangalipo wanachama wake wengi magerezani na mahakamani kwa kesi za kubumba.

4. Nk.

Hivi karibuni Mama Samia amepata kuongea na Mh. Lissu na baadaye na Mh. Mbowe. Matokeo ya maongezi hayo tayari yameonekana.

IMG_20220311_174018_960.jpg


Yumkini sasa Mama anayo picha sahihi ya Chadema ni nani dhidi ya picha zote kutoka kwa wafitini wa wao wote.

Kwamba Mama Samia amekubaliana kuendeshwa kwa siasa za haki zenye kuzingatia ustaarabu pasipokuwa vizingiti vyovyote?

Haipo shaka kuwa sasa:

"Siasa zitafanyika kwa kuzingatia sheria ambapo kila mtu atawajibika kikatiba na bila exception."

Yumkini kutokea hapa haki zote za msingi kama ambavyo imekuwa ikiombwa, zitaheshimiwa na wote. Kwamba hatimaye misingi yote ya haki, itatamalaki kwa mujibu wa katiba iliyopo.

Ikumbukwe Chadema haijawahi kuhitaji chochote nje ya katiba.

"Macho yote kwa Mama Samia, kuhakikisha utekelezaji."
 
Kuna ibada inaendelea mitaa ya Ubungo maziwa sijui ni kanisa gani, nimemsikia kiongozi wa ibada kwenye spika amesema kwa sauti ya juu "pipooooz!!!"
 
Mkuu, katiba mpya tuidai?, au basi?

Mkuu nini kisichoeleweka hapa? Chadema haijawahi kuacha kuzingatia sheria. Wewe hutaki kuzingatia sheria?

"Siasa zitafanyika kwa kuzingatia sheria ambapo kila mtu atawajibika kikatiba na bila exception."

Ieleweke mikutano ya siasa ni kwa mujibu wa sheria. Kudai katiba mpya ni kwa mujibu wa sheria. Ila kuyazuia hayo ni kinyume cha sheria.

Tatizo liko wapi mjomba?
 
Katiba mpya kwanza upole baadae

Wapi upole na katiba vinagongana au kwenda pamoja?

Katiba mpya itadaiwa kwa mujibu wa katiba:

1. Ni haki kudai katiba mpya
2. Ni haki kufanya mikutano ya siasa

Ni kinyume cha katiba kuzuia hayo.

Pande zote zimeridhia sheria kufuatwa. Wewe hutaki?

Kwani una undugu au ubia na waliokuwa wakizuwia harakati hizi hadi kupelekea mitafaruku iliyopelekea hata watu kupotezwa?
 
Kila la kheri zao...

Kwenye kudai katiba mpya kwa mujibu wa katiba hakuna kilichobadilika.

Kilichobadilika ni kuzuwia madai kama hayo kinyume cha katiba.

Tunasoma sawa sawa kweli?

Tulipo tunachosubiri ni matamko rasmi:

1. Katiba mpya tunatoka vipi?
2. Mikutano ya kisiasa tunatoka vipi?
3. Kuja kwa Mh. Lissu ni lini?
4. Tarehe ya mkutano CDM na Mama ni lini?

Kwa hakika tuko vizuri zaidi kuliko wakati wowote kabla.
 
Kuna ibada inaendelea mitaa ya Ubungo maziwa sijui ni kanisa gani, nimemsikia kiongozi wa ibada kwenye spika amesema kwa sauti ya juu "pipooooz!!!"

Usije kuta alikuwa Askofu Rashid? Huwa si nadra kwake kuonekana mitaa hiyo.

Usisahau huyo ni mtu wenu wala sisi huyo hatuna time naye kabisa!
 
Back
Top Bottom