Chadema nendeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema nendeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Najijua, May 5, 2011.

 1. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  CDM wanaanza ziara ya operesheni sangara nyanda za juu kusuni wosia wangu kwao ni huu hapa

  Nendeni bila woga, nendeni kuwahubiria ukombozi wa taifa lao, nendeni kawaambineni TZ bila CCM amani inawezekana, kawaambieni waamke kutetea taifa na rasilimali zao,nendeni kawapeni ujasiri kuwa mabadiliko hata vijijini yanawezekana na sio mijini tu, nendeni kawaambien kwanini mpaka leo ni maskini wakati taifa lao lina rasilimali za kutoshamfano dhahabu, makaa ya mawe,mbuga za wanyama, na ardhi yenye rutuba ya kutosha

  Nendeni kawaambieni wasikubali kupokea T-Shirts na kofia bila suruali wala sketi tena wanakosewa heshima wanatakiwa kuvaa kwa miaka mitano,nendeni kawaambieni kiongozi kwa CCM ana anza maskini akimaliza muhula wake naye ni biliionea, nendeni kawaambieni watoto wao waliosoma vyuo vikuu kwa tabu, mlo mmoja kwa siku, kupigwa na virungu na bado hawapati ajira walio pata hazina tija wakati watoto wa vigogo wanapewa kazi nono kule BOT,ndani ya chama, ikulu na kwengineko, nendeni kawaambieni watoto wao ni ndoto kuwa viongozi wa taifa hili kwa kuwa tuu wao hawapo katika ukwasi na sio family friends kwa waliopo katika ukwasi.

  Nendeni kawaambien hatima ya nchii hii ipo mikononi mwao na wasihadaike na rusha roho na ngoma za siku moja wakati wanalia ukali wa maisha magumu, nendeni kawaelezeni safari hii wameambiwa ARI ZAIDI, KASI ZAIDI NA NGUVU ZAIDI, chaguzi zijazo ni wao kuamua kupunguza kasi ya kufanywa maskini, kupunguza kasi ya kufanywa madalali wa rasilimali za taifa lao

  Nendeni kawaelezeni wafanye maamuzi magumu na yote yanawezekana, Zambia, Malawi, Ghana, Nigeria na hata Ulaya wameweza na wao wanaweza, waache dhana potofu kuwa vyama vya upinzani ni Vita, waache dhana potofu eti CCM imewalea wakati haiwajali tena, kila siku ni afadhali ya jana na CCM yaom kila siku wanapokonywa ardhi zao na kila siku CCM wanayoipigania inawachangisha michango isiyo na tija wakati vigogo wanajilipa posho nono, kodi zinaongezeka wakati vigogo kila siku wanapanga safari za nje wakati mwingine hata kwenda kubembea Jamaica kwa kuwa fedha zao hazina kazi wakati madawa hakuna hospitalini


  Tupo nyuma ya CDM wakati wanapeleka habari hii, tupo tayari kuchangia kama kawaida yetu ili wapeleke habari njema, tupo tayari kuwalinda na kuwatetea daima, tupo nyuma yao wasikate tamaa
   
Loading...