Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Nilikuwa Arusha kuhudhuria Kongamano na Mkutano wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS). Vyote vilifanyika kwa siku moja,yaani Jumamosi ya tarehe 16/8/2014 AICC. Pale Arusha,kulikuwa ni mahali pa kukutana na Mawakili Wasomi mbalimbali waliotawanyika nchini na kubadilishana mawazo.
Moja ya mazungumzo ilikuwa ni hali ya kisiasa hapa nchini.Mazungumzo haya yalifanyika wakati wa mapumziko ya chai au chakula cha mchana. Wakili Msomi mmoja akatoa hoja kuwa unapofanyika uchaguzi hapa nchini,wagombea wa upinzani hasa CHADEMA hupambana na wapinzani wa aina tatu. Kwanza, vyombo vya dola.Mgombea itampasa kupambana na changamoto na mikwaruzo mbalimbali kutoka vyombo vya usalama na kuvishinda kwa kulindwa na mapenzi ya wananchi juu yake.
Pili,mgombea atapambana na mgombea mwenzake wa chama tawala au kinginecho. Yampasa kujenga hoja ili akubalike zaidi ya mwenzake. Na tatu,Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mgombea husika lazima apambane na Tume kwa namna kama ya 'kulazimisha' matokeo kutangazwa. Pia,kupambana kuepuka kuibiwa kwa kura zake na kutangazwa mwingine badala yake.
Wakili Msomi huyo akamaliza kwa kusema kuwa Wabunge wote wa Majimbo wa CHADEMA wamepambana na 'wapinzani' hao na kuwashinda. Hivyo,si jambo dogo kuwaona Bungeni. Wamefanya kazi kwelikweli. Ni mashujaa. Hivyobasi,ni watu wapambanaji,shupavu na wa kupigiwa mfano. Ni chaguo hasa la wananchi. Akamaliza kwa kusema,mwaka 2015 itakuwa kazi pevu kuwapoka Ubunge wabunge wa aina hii.
Mjadala ulikuwa mkali kwa kila Wakili Msomi aliyekuwepo hapo mazungumzoni kuwa na mtazamo wake. Nami,nikabaki kujifunza jambo tu. Nilikuwa Junior Counsel kuliko wote kwahiyo nikabaki kuwa msikilizaji.
Waungwana,kuna ukweli wowote hapa?