Joss
JF-Expert Member
- May 28, 2009
- 765
- 192
Chadema imepiga hatua nzuri na imeonesha mwanga kwa wapenda mabadiliko, pongezi kwa viongozi na wanachama, jambo moja ambalo linanitia shaka na pengine wengi wetu mtakubaliana na mimi ni uwezo wa baadhi ya viongozi. Ninaposema uwezo wa viongozi simaanishi uzalendo kwa chama, hapana, hivi ni vitu viwili tofauti.
Wengi wetu tumejionea purukushani zilizotokea BAVICHA, Viongozi waliotimuliwa kama M/mwenyekiti au mtu kama aliyekuwa Katibu wa BAVICHA mkoa wa Tanga, ambaye amehamia NCCR, ama aliyekuwa mbunge mtarajiwa mbw. Mwampamba kweli ukisoma maandishi yao tu au hoja zao, huwezi amini walikuwa ni viongozi wa CDM. Hawa tumeujua uwezo wao kifikra baada tu ya purukushani hizo. Nachelea kujiuliza ni viongozi wangapi ambao wapo ndani ya CDM wenye uwezo kama huu?
Wito wangu kwa CDM ni kuwa waharakishe mpango wao wa Chuo cha uongozi, na pia wawapime wagombea ipasavyo ilikupata viongozi bora na si bora viongozi.