CHADEMA na Utata wa kimantiki

..labda wengine mmesahau kilichotokea kwa ripoti ya kamati ya Jaji Mkuu Francis Nyalali.

..halafu kuna vitimbi alivyofanyiwa Jaji Robert Kissanga.

..mwisho uchakachuaji uliofanywa ktk ripoti ya Prof.Samuel Mwita Wangwe kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki.

..utaratibu wa kuunda Tume za Raisi hapa kwetu umekuwa na matokeo mabaya ndiyo maana wanaharakati wanapendekeza utaratibu tofauti.
 
Chadema siku zote wanapenda amani, hawakuwahi kutafuta vurugu. Wametoa maoni yao Bungeni kwa njia ya hotuba ya msemaji wao - Lissu, hawakusikilizwa.
Sasa wanajaribu second option, ya kumshawishi JK kwa faida ya watanzania kwamba asisaini mswada huo ili kupata mwafaka wa Kitaifa na kisha kupata katiba ya kitaifa.
Ifahamike, mchakato huu uliokwishapingwa na wasomi, wanaharakati na chama kikuu cha upinzani hauwezi kuacha kuleta vurugu JK asipowasikiliza. Chadema wanasaka amani. Utata wa kimantiki sijauona.
Mamlaka ya JK yanayopingwa ni yale aliyopewa na mswada mpya wa mabadiliko ya katiba, siyo mamlaka aliyopewa na katiba hii mbovu.
JK bado ni rais hata kama urais wake umepatikana kwa njia tata kwa mujibu wa katiba yetu mbovu.
Huwezi kumkana baba yako aliyekuzaa hata kama baba yako huyo alimbaka mama yako. Huna namna, japo kuwa hupendi ubakaji. Katiba mbovu ndo imeshamweka japo kwa kubaka demokrasia, sasa unapotaka chadema wasiende kumwona Rais, unataka waende msituni kupambana? Hiyo njia hatuipendi kwa faida ya watanzania. Hakuna utata wa mantik
i.

You're one of the great thinkers in this 'jamvi', weldone. Nadhani mtoa thread ameelimika kiasi cha kutosha, anayeweza kupinga ukweli huu labda awe na akili zenye gamba gumu kama la kobe a.k.a. CCM ambalo halivuliki kwa sababu gamba lake ndiyo nyumba yake.

 
Kuna wakati ni vigumu kumuelimisha asiye tayari kuelimika.,lakini nitajitahidi hasa kwa wale waliotayari kuelewa uhalisia wa mchakato wa katiba.,naanza kwa utambuzi wa ninaotarajia kuwaelimisha.,nikianza na wewe hasa ktk kauli yako ya JK kuongoza nchi "hovyohovyo" nipe vigezo vikuu vitatu.
Kila mtu hujiita msomi humu jamvini lakini kwa usomi ulionao wewe inaonyesha ni kihiyo au ulikuwa unakariri sana kiasi cha kutoelewa kabisa. kama hujui hata utaratibu wa kuandaa katiba bora naomba uache kusoma vitabu vya falsafa anza kusoma vitabu vya sheria ya katiba (constitutional law) Huko utapata pia kujua mchakato wa katiba bora unakuaje.
 
pole sana ww ndiye mwenye utata wa mantiki coz ww unatanguliza ushabiki kuliko uhalisia.CHADEMA kinatambua yote ndiyo maana kimeunda kamati ndogo ambapo kikwete akiendelea na msimamo wa kifalme basi kwa jinsi CHADEMA ilivyo na ushawishi kwa Umma bac nchi hii lazima inuke wananchi wako tayari kwa lolote litokanalo na tamko la CHADEMA.Angalia kwanza timu ya hiyo kamati {magwiji wa sheria}inayomwendea rais hapo ndipo uamini CHADEMA kina safu ya kushika dola.Najua ww utakuwa CUF kila cku dua yako ni kuona eti CDM inafunga ndoa na CCM kama nyie wa CUF.TAMBUA CDM ni chama makini hatutegeki hata kidogo MSWAADA HUU LAZIMA URUDI KWA WANANCHI.
 
Hatuwezi kukubali mabadiliko na kisha kupinga chanzo cha mabadiliko hayo, ukifanya hivyo utajiingiza ktk utata wa kimantiki- ni kauli niliyowahi kuisoma katika moja ya vitabu vya falsafa nilivyowahi kuvisoma.,ni kauli inayotokana na mmoja wa magwiji wa falsafa duniani na waasisi wa somo hillo.,socrates..,ni wazi kuwa alikuwa anamaanisha ni vigumu kwa watu wenye ufahamu wa mambo kupinga mamlaka na nafasi ya JK kama Rais na kisha kukubali kuwa anayo nafasi ya kufanya maamuzi juu ya mchakato wa kikatiba.
hakika huu ni utata...!

akili yako fupi kama maisha ya funza... Ume quote maneno mazuri, lakini umey2mia mahala Sipo... Kwanza kabisa CDM hawajai kukataa kuwa VASCO DA GAMA ni Presid. Walichokataa ni mfumo ( let say TUME YA UCHAGUZI ) uliomuweka Kikwete madarakan ndo c sahihi... Go back jipange then rudi tena..
 
Chadema siku zote wanapenda amani, hawakuwahi kutafuta vurugu. Wametoa maoni yao Bungeni kwa njia ya hotuba ya msemaji wao - Lissu, hawakusikilizwa.
Sasa wanajaribu second option, ya kumshawishi JK kwa faida ya watanzania kwamba asisaini mswada huo ili kupata mwafaka wa Kitaifa na kisha kupata katiba ya kitaifa.
Ifahamike, mchakato huu uliokwishapingwa na wasomi, wanaharakati na chama kikuu cha upinzani hauwezi kuacha kuleta vurugu JK asipowasikiliza. Chadema wanasaka amani. Utata wa kimantiki sijauona.
Mamlaka ya JK yanayopingwa ni yale aliyopewa na mswada mpya wa mabadiliko ya katiba, siyo mamlaka aliyopewa na katiba hii mbovu.
JK bado ni rais hata kama urais wake umepatikana kwa njia tata kwa mujibu wa katiba yetu mbovu.
Huwezi kumkana baba yako aliyekuzaa hata kama baba yako huyo alimbaka mama yako. Huna namna, japo kuwa hupendi ubakaji. Katiba mbovu ndo imeshamweka japo kwa kubaka demokrasia, sasa unapotaka chadema wasiende kumwona Rais, unataka waende msituni kupambana? Hiyo njia hatuipendi kwa faida ya watanzania. Hakuna utata wa mantiki.
Mbona hamkwenda kumuona rais alipokataa bajeti zenu mbadala?
 
jamani wengine hapa tuna upeo mdogo wa kufikiri may be tunaomba msaada kwenye tuta tupate kuelewa..
kuna watu humu ndani wamekomaa kwa nini Rais awe na sauti ya mwisho kututengenezea katiba mara ooh katiba itatengenezwa sijui na akina nani! naomba niulize swali waungwana, hivi kwa mfano ndo procedures zote zimepita na wananchi wamepiga kura ya maoni wameikataa katiba, hapo bado Rais anaweza kuja na kuihalalisha ikawa katiba halali kwa Tanzania?si ana sauti ya mwisho?anajiamulia afanye nini au kipi kiwepo/kisiwepo kwenye katiba mpya?na kama jibu ni hapana atakubali yaishe nani atakuwa ameamua kuhusu mustakabali wa katiba, Rais au Wananchi? na Wananchi si ndo watakuwa wameshirikishwa?au mnaogopa kuwa hata asilimia kubwa ya wananchi wataisapoti even though haitakuwa in ur favour?lastly, kwa nini tuishi kwa hisia badala ya kuacha muda uongee kuliko kuendelea kutulisha maneno ooh Rais atafanya hv mara atamchagua fulani kwenye kamati etc etc
 
Back
Top Bottom