Chadema na nccr vyafunga ndoa

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Katika hali inayoonyesha kuimarika kwa demokrasia nchini,vyama vya chadema na nccr mageuzi vimekubaliana kwa pamoja kuzika tofauti zao na sasa kushirikiana katika baadhi ya mambo ya kisiasa hapa nchini.

Katika makubaliano hayo Mbatia amefuta kesi aliyomfungulia Halima Mdee baada ya kugaragazwa pale kawe na mwanadada huyo machachari katka siasa za Tanzania.



My take:Ni hatua nzuri kuelekea ujenzi wa demokrasia ya kweli na ya kukubali kushindwa hasa kwa mbatia.
 
@ JF

Wameanza kwa kufuta kesi ya uchaguzi Kawe,ili kuondoa makovu na

kuimarisha upinzani,Nini kifanyike zaidi ya hapo !!!!!

Na Je inawezekana katika maslahi ya Taifa !!


source ITV,STAR TV,MLIMANI TV
 
Wakitangaza leo katika ofisi ya NCCR mageuzi ilala jijini Dar es salaam, chama cha NCCR MAGEUZI kimefuta kesi iliyokuwa imefunguliwa na mwenyekiti wa chama hicho mh. francis mbatia dhidi ya halima james mdee mbunge wa kawe aliyekuwa akitoa matusi ya nguoni dhidi ya mbatia, taarifa nilizo zipata kutoka kwenye vyanzo vyangu vya habari ni kuwa kesi hiyo ilikuwa inamuendea vibaya Halima mdee kwa hiyo viongozi wa chadema wameamua kwenda kuwapigia magoti viongozi wa NCCR na kuwapa pesa kama fidia na kuahidi kuwashirikisha katika serikali yao kivuli ya upinzani waliounda ndani ya bunge, je uundaji wa ushirikiano wa namna hii? je utadumu?
 
Vyanzo vyako kazi kweli, Mhe. Francis Mbatia ni nani huko NCCR?
 
Crap! Crap! Kuupata umaarufu kwa mgongo wa JF si kazi nyepesi, wakati mwingine yakubidi u-act kaa mtoto vile!
 
kumbe ndiyo maana chadema walitaka kuvunja ndoa ya CUF na CCM wakaenda hadi Ikulu, waliposa lini NCCR?
 
Heading: Kufunga ndoa. Thread: kufuta kesi. Utumwa wa fikra ni mbaya kuliko utumwa wa mali. Heri ukose mali upate akili
 
Ndoa imefungwa bomani, kanisani au msikitini? Tangazo la harusi sikusikia? inapendeza kuoana kabila moja la upinzani.
 
Kudumu si hoja.Ila inategemea nini hawa NCCR wamelenga.Kitu ambacho nahisi IS STILL A COVERT ISSUE.
 
Halima James Mdee duh.... na Fransis mbatia mmmh.... jamaa atakua alikua anatetemeka akili.
 
Vyanzo vyako kazi kweli, Mhe. Francis Mbatia ni nani huko NCCR?

Watu wengine mmejaliwa roho ngumu?
Kumjibu mtu kama huyu inataka moyo! Maanake heading na alichokisema ni tofauti kabisa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom