Elections 2010 Chadema na mbinu ya lawama kupata huruma



Hili bado halijaingia kwenye vichwa vya wana-mageuzi wa JF.

Maranyingi namna hii ya lawama ni kutaka kuwaaminisha wananchi kuwa wao wanaonewa hivyo waonewe huruma na kupewa kura na pia kujiandaa pindi watakaposhindwa wapata sababu ya kusemea


Wana saikolojia na sosholojia wanaita "PLAYING VICTIM" Ni kama mtu anayejitundika na kuacha ujumbe kwamba amefanya hivyo kwa kuonewa na jamii, hivyo jamii inamzika huku ikimwonea huruma na kujilaumu kwa kusababisha kifo chake!!!

Kuna kosa moja kubwa sana CHADEMA wanalo lifanya kutokujua nguvu ya CCM ipo wapi?
Kudai tu tume mara masajili, polisi ni vya CCM hivyo tunaonewa haileti mantiki, wananchi wakiwaamini hata mtawala amiliki nini mtashinda tu[/COLOR][/COLOR] paulss

Sina nyongeza, umeongea nilichotaka kukiongelea
 

hii inonyesha ni kwa kiwango gani hauna hoja, kwani ni lazima kujenga. Nchi za wenzetu manispaa ndizo hujemnga na wengine kupanga. Kwani ukiacha zile ccm ilizopora kutokwa kwa wananchi wamejenga zipi?. shukuruni kuwa upo uwezekano mkubwa wa kuiba kura this time, kwa jinsi ccm na viongozi wake walivyotegemezi kwa dola kwa kila kitu, siku ya kutoka madarakani, which is sooner thana later, ndio chama kinakufa the same day. Heri watoto ya yatima "wapinzani" wanajua how to survive.
 

unachokiita lawama ni mkakati maalmu kati ya ccm na tbc kuacha kuonyesha seras za chadema na badala yale kuonyesha yale mapungufu ya serikali yanyotamkwa na chadema, kitu ambacho hamtaki kukubali kuwa chadema ilikwisha maliza kazi katika operehseni sangara, ndio maana ccm inapata resistance kiasi cha kuomba msaada wa jeshi. Hii ni kama panadol kwa mgonjwa wa malaria. Tatizo la ccm ni ufisadi, hivi sasa hata wale waliokuwa wakijifanya kuwapinga mafisasdi wameungana kutetea vitumbua vyao ndani ya ccm ya kifisadi, wananchi wanaona.

Ufisadi una kanuni zake "penye riziki pana fitina" baada ya kuiba kura za wapinzani na kila mmoja kuanza upya kufyonza keki ya taifa atakavyo kama ilivyo ada mtaanza tena kupakana matope, fitina, majungu, na kushughulikiana na wananchi, ndio watakumbuka maneno ya chadema na dr slaa ready for 2015, the final demise of ccm and ufisadi in tanzania, wakati mtakapoanza kuparuana wenyewe kwa wenyewe kwa urais.
 
bora umekubali mwenyewe kwamba polls za chadema online ni 1.5% za watu mil 40.....unajua kwamba polls za hao wanasayansi unaowasema ni 0.01% za watu mil 40....je walijua hilo? kwa sababu polls za online ni watu 8000 na ushehe while za hao wanasayansi giza ni 2500....ushindwe na uregeeeeee
 
Mwanzoni nilidhani muda wa kampeni unapokuwa mrefu unai-saidia vyama vya upinzani kufika kila mahali hivyo kusaidia upinzani... lakini kwa bahati mbaya sana... vyama vya upinzani hasa CHADEMA wameanzisha hoja zingine ambazo zinakula muda mfupi waliokuwa nao.
 

I can't agree with you more! Chadema ni wazuri na warahisi sana katika kunasa kwenye mitego ya CCM! JK leo anawatisha wananchi juu ya umwagaji damu Chadema wanakesha kujadili UMWAGAJI DAMU alioungea JK badala ya kumwaga sera. Juzi kinana kawaingiza mkenge kwa kuyachambua matokeo ya REDET na sasa Chadema wako busy kuja na matokeo ya kura za maoni za kwenye internet zikiwamo za hapa JF.
 

mkuu hii ni nchi yetu si za wenzetu na huu ni udhaifu mwingine ukihojiwa udhaifu wako,unaanza kujilinganisha na mwingine, 'mbona" zinakuwa nyingi. hapa issue nikuwa ccm tayari wanazo bilakujali wamezipataje, wewe je?

Uwezekano mkubwa wa kuiba kura ndio nini,yale yale niliyosema mtu akiona dalili za kushindwa huandaa mazingira kwa sababu kibao
 


SOMA THREAD HII:- Nilichokiona kwenye mikutano ya Dr. Slaa
NIMEHUDHURIA mikutano ya kampeni za awamu ya pili za mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa. Kwa nguvu za kampuni ya gazeti hili la Raia Mwema, nimefika katika mikutano ya Ifakara mjini, Lupiro-Mahenge, Songea Mjini, Njombe-Mjini, na Iringa Mjini.

Ni baadhi ya mikutano tu. Kwa kuzingatia mikutano hiyo, nitajadili umuhimu wa nilichokiona ambacho kwa wengine hakionekani au hawataki kukiona na zaidi, hawataki kutoa tafsiri ya kimantiki.

Tangu kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu 2010, vyombo vya habari vimekuwa vikizungumzia wingi au uchache wa watu katika mikutano ya wagombea husika.

Ni kawaida kwa mwandishi wa habari gazetini kuandika mkutano ulihudhuriwa na maelfu au mamia ya wananchi.

Ni kawaida sasa kwa mwandishi wa habari wa televisheni kuonyesha picha za wingi wa watu waliohudhuria. Kwa kadri ya mwenendo wa kampeni, waandishi wamekuwa wakilenga mambo matatu makubwa.

Kwanza ni ujumbe wa mgombea husika kwa watu wanaomsikiliza. Pili, wingi wa watu. Tatu ikibidi vituko au mbwembwe zilizojiri eneo la mkutano.

Ni kweli, yote haya yamekuwa yakijitokeza kwenye mikutano husika. Ni muhimu kuripotiwa.

Binafsi, kwenye mikutano hiyo ya Dk. Slaa, sikushangazwa na wingi wa watu au ujumbe wa mgombea huyo kwa wananchi. Ni mambo yaliyoanza kujitokeza tangu kuanza kwa kampeni zake.

Nilichoshuhudia, pengine ambacho kinaonekana lakini watu hawataki kukiona, ni utulivu na usikivu wa wahudhuriaji kwenye mikutano ya maeneo niliyotaja hapo awali.

Kwa mtu makini, utulivu na usikivu wa asilimia 100 kwa watu zaidi ya 40,000 tena waliokusanyika pamoja kwa hiari yao, ni suala la kushitua.

Katika mikutano hiyo, nimeshuhudia umati mkubwa watu ukiwa katika utulivu na usikivu wa asilimia 100. Ni utulivu na usikivu ninaoweza kuita chemchemu ya fikra mpya kwa viongozi au watawala.

Nizungumzie mkutano mmoja kati ya mingi niliyopita. Huu ni mkutano wa Ifakara mjini. Nikiwa mkutanoni Ifakara mjini nilimwona mama muuza ndizi mbivu alizozipanga kwenye sinia.

Kwa wakati huo, mkutano ulikuwa ukiendelea, Dk. Slaa anazungumza.

Kwa kuwa utulivu na usikivu uwanjani pale ulikuwa kwa asilimia 100, huku sauti ya mtu mmoja tu ikisikika (Dk. Slaa), nilimsogelea yule mama, ambaye macho yake yalijielekeza kwa Slaa na sio sinia lake la ndizi alilokuwa ‘amelibwaga’ chini.

Nilipomsogelea, nikainama kukwanyua ndizi mbivu ili nile kama mnunuzi wake. Hapa, kipaumbele changu hakikuwa ndizi bali kupima utulivu na usikivu wake kwa mtu anayemsikiliza. Je, anaguswa na anachosikia?

Je, amefika uwanjani hapo kwa sababu kipaumbele chake ni kuuza ndizi? Na je, kama kipaumbele chake awali kilikuwa kuuza ndizi, kipaumbele hicho kimetekwa na hoja za Dk. Slaa?

Je, kipaumbele cha mama huyu muuza ndizi mbivu kimegeuka kutoka uuzaji ndizi eneo la mkutano hadi kusikiliza hoja za Dk. Slaa? Kwa nini haya yamtokee mama huyu? Haya ni sehemu ya maswali niliyotaka kuyajibu kichwani mwangu.

Nilipokwanyua ndizi ile ya kwanza, alinitazama na kisha kuendelea kumtazama na kumsikiliza mzungumzaji (Dk. Slaa). Nahisi aliniamini kwamba ni mteja nitakayemlipa bila matatizo.

Nilikula ndizi nne bila yule mama kunitazama (macho na masikio yake yakitekwa na Dk. Slaa). Bado uwanja ni tulivu na usikivu wa maelfu ya watu ni mkubwa, ukiniondoa mimi ambaye bila shaka nimepunguza kiwango kutoka asilimia 100.

Nilichukua ndizi nyingine. Nikamuuliza hivi unajua nimekula ndizi ngapi? Akajibu, wewe kula nitahesabu maganda; huku akiendelea kumsikiliza Dk. Slaa. Alijinijibu kwa haraka, nadhani alinichukulia kama mtu msumbufu na si mteja anayemtafuta juani kila kukicha.

Hatua yake hiyo ilinifanya niwekeze zaidi fikra zangu kwake na kiasi fulani nihusishe na ujumbe wa Dk. Slaa kwa wakati huo.

Kama ilivyo kawaida, masikio ya mwanahabari na macho yake hulazimika kufanya kazi ya ziada. Wakati nikila ndizi niligawa fikra zangu, nilikuwa nikisikiliza anachosema Dk. Slaa.

Kwa hiyo fikra zangu zilibanwa na matukio matatu kwa wakati mmoja. Kwanza, kuwasiliana kifikra ‘kimya kimya’ na huyu mama kwa kuzingatia utulivu na usikivu wake uliomfanya apuuze biashara yake kwa muda.

Pili, kuunganisha mawasiliano hayo ya kifikra na ujumbe wa Dk. Slaa ili nipate tafsiri sahihi kwa kutazama mwenendo wa nchi, siasa na mchakato wa kidemokrasia.

Tatu, kwa kuzingatia ujumla wa mazingira hayo, nini nafasi ya watawala walioko madarakani? Je, ni kweli kuna mkatiko wa mawasiliano kati ya watawala na walalahoi mfano wa huyu mama?

Naam, mkutano unaendelea. Sasa Dk. Slaa anazungumzia hoja mbili. Kwanza alikuwa akifafanua atapata wapi fedha za kufidia uamuzi wake wa kuondoa kodi kwenye vifaa vya ujenzi.

Uamuzi unaotajwa kulenga kumwezesha mwananchi mwenye uwezo wa kati au wa chini ajenge; tofauti na hali ilivyo sasa.

Lakini pia Dk. Slaa alikuwa akifafanua atapata wapi fedha za kugharimia elimu ya awali hadi chuo kikuu ili kumwondolea mzigo mzazi wa mwanafunzi au wanafunzi.

Masuala haya mawili niliyaunganisha na utulivu ulioshiba na usikivu wa yule mama muuzaji ndizi. Ni mama wa makamu anayeonekana kuwa na familia. Tena ni familia yenye wanafunzi.

Kuna mambo kadhaa niliyabaini kutoka kwa mama yule. Kwanza , licha ya kufanya biashara anaamini biashara husika haikidhi mahitaji lakini hana mbadala.

Katika mazingira hayo, ni dhahiri mbadala pekee anaohitaji yule mama ni kuchagua kiongozi bora. Kiongozi atakayelinda maslahi yake, familia yake, jirani zake, wana-Ifaraka wenzake, wakazi wenzake wa Morogoro na Watanzania wenzake nchini.

Nguvu ya usikivu na utulivu kutoka kwa mama yule na maelfu ya wakazi wengine uwanjani pale ilinielekeza niibue tafsiri mpya.

Tafsiri hiyo ilizingatia masuala ya msingi, ikiwa ni pamoja na ukweli kuwa, wananchi walifika eneo la mkutano kwa utashi binafsi na si kwa ushawishi wa lifti au kingine chochote.

Na kubwa zaidi, hata waliofika kwa ajili ya kufanya biashara ndogo ndogo walisahau biashara zao. Kwa kuzingatia mazingira haya, tafsiri niliyoipata ni kwamba viongozi walioko madarakani hawako salama hata kama watashinda uchaguzi kwa haki au mizengwe!

Haina maana kwamba hawako salama kwa maana ya uhai wao, la hasha. Hawako salama kwa kuzingatia mfumo wao wa kiuongozi. Mfumo wa uongozi unaomtenga mama yule na wenzake kutia mkono ili naye anufaike na raslimali za Tanzania.

Mfumo wa uongozi unaotanguliza kujuana katika mgawanyo wa raslimali na kulindana katika makosa ya ufisadi wa mali za umma. Hakika, kama mfumo huo hautavunjwa baada ya uchaguzi mkuu, mama yule na wenzake wakaendelea kusahaulika, viongozi hawatabaki salama. Siku zao zitaanza kuhesabika.

Nguvu ya utulivu na usikivu ya mkusanyiko wa watu zaidi ya 40,000 niliyoshuhudia Ifakara ndiyo iliyojitokeza Lupiro-Mahenge, Njombe, Songea na Iringa.

Kwa heshima zote, nawasilisha ujumbe kwa watawala kwamba; utulivu na usikivu ule wa hoja ni shinikizo kwenu kubadilika; kinyume chake siku zetu zitaanza kuhesabika.

Ukweli ni kwamba, yeyote atakayeshinda Uchaguzi Mkuu 2010 na kuingia Ikulu, awe Dk. Willibrod Slaa wa CHADEMA, Jakaya Kikwete wa CCM au Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, usikivu na utulivu ule katika mkusanyiko wa maelfu ya walalahoi ni changamoto mpya kwao.

Kama leo mkusanyiko wa walalahoi zaidi ya 40,000 katika kila mkutano wanakua watulivu, ipo siku utulivu na usikivu ule utafanyiwa kazi na walalahoi hao hao. Siku hiyo itafika kama watawala watazidi kujenga wananchi wa mfano wa mama muuza ndizi.

Siku hiyo ikifika, watoto wa mama muuza ndizi na watoto wa majirani zake na wengine nchi nzima wataungana kutaka kujiondoa kwenye lindi la umasikini kwa kutumia nguvu na akili zao kwa taratibu zao. Atakayeshinda asiruhusu hilo.

Hii ni changamoto inayoshinikiza kufumuliwa kwa mfumo wa uongozi wa kulindana katika ufisadi, kuenzi urafiki katika kugawana madaraka. Ni changamoto inayohitaji kufumua mfumo wa chama kwanza, Taifa baadaye.
Sidhani kama yule mama ni mwana-CCM lakini nina hakina ni Mtanzania.

Kuendeleza kauli za chama kwanza mtu baadaye, ni kuzidi kuwatenga katika ufalme watu mfano wa yule mama anayeshinda juani kusaka tonge.
Nihitimishe kwa kumnukuu mwanzilishi wa taasisi ya kudhibiti uzito kwa watu (Weight Watchers Organization), Jean Nidetch, aliyewahi kusema: “It's choice -not chance - that determines your destiny.” Kwamba ni uamuzi na si fursa inayoangaza hatima yako.

Kazi kwako. Nikipata nauli nitahudhuria mikutano ya wagombea wengine na nitakueleza nitakachoona bila wao kuona.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika​
 
Mimi sijaona kuwa CHADEMA ni walalamishi kinacholalamikiwa ni mbinu chafu. Kwa mfano hayo matokeo kwa SINOVET na REDET mbona hayasemi au hayatafiti hali ya kisiasa visiwani? Ni kutokana na ukweli kuwa matokeo yao yatapingwa na ccm na Huenda tafiti zao zikapigwa marufuku.

Kwamfano muda wa kupiga kampeni mwisho ni saa 12:00 jioni lakini kunawakati mgombea wa ccm alifanya kampeni mpaka saa moja usiku na zaidia na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa je CHADEMA au vyama vingine vikipinga kosa hili utauita ulalamishi usio na msingi? Unajua lakini utamaduni wa siasa?
 

Mkuu kunatofauti kubwa sana kati ya tafiti na online polls
online polls zinaweza kuwa na vote nyingi kwakuwa hazina usimamizi na zinalenga kundi fulani la jamii, mfano wenye kuvote jf lazima uwe na access ya net pia wanaweza kuvote hata mara 100.
lakini tafiti za kisayansi zinaweza kuwa na sample chache lakini zinafuata international standard kwa kuhusisha watu wa makundi yote ktk jamii toka kila pembe ya nchi kwa kuwafuata walipo
 
Jatropha
hiyo makala ya Dilunga wa raia mwema nilisha isoma, mwandishi ametumia utaalam na ubunifu mkubwa na wa kuvutia kuwasilisha ujumbe wa kile alichotaka tukiamini
Lakini ktk post hiyo Maggid alihoji vitu vya msingi sana kuhusu hiyo makala na akaishia kutuhumiwa tu ametumwa
naomba rejea tena post hiyo na usome na post zilizo jibu, hata mimi nilicomment humo
 

Kama CCM wanacheza faulo unategemea Chadema wakae kimya? REDET nchi nzima haiwaikubali kazi yao sasa Chadema wakae kimya?

Wanajeshi wanapoingilia kazi ya NEC unategemea Chadema wakae kimya?
 

tatizo lako facts zako nyingi zinztegemea coverage ya wanahabari ambao wako ndani ya mkakati wa CCM kuonyesha kuwa Dr Slaa analalamika sana, mbona Dilunga anasema kuwa Dr Slaa alifafanua namna Serikali yake itakavyopata fedha za kuizba pengo baada ya kufuta kodi katika vifaa vya ujenzi na watoto kusoma bure. Mbona masuala hayo hayakuwa covered hata kidogo. Hivyo utakabaliana na mimi kuwa na wewe pia umetumbukia katika mtego wa CCM na vyombo vya habari kumshusha Dr Slaa.

Juzi nilitazama mikutano ya Dr Slaa kule Kigoma, TBC walionyesha ile sehemu tu ambayo ina watu wacahache na wanafunzi, lakini katika mkutano huo huo ITV walionyesha mahudhurio halisi ya mkutano huo.

Mwanahabari mmoja amenithibitishia kuwa katika baadhi ya vyombo vya haari ukitaka kupoteza kibarua chako onyesha mahudhurio halisi ya mikutano ya kampeni ya Dr Slaa. Hivyo clip nyingi wanazotumia ni kumuonyesha yeye mwenyewe anapokuwa akiwasilisha less importanta issues
.
 
Kama CCM wanacheza faulo unategemea Chadema wakae kimya? REDET nchi nzima haiwaikubali kazi yao sasa Chadema wakae kimya?

Wanajeshi wanapoingilia kazi ya NEC unategemea Chadema wakae kimya?

Mkuu nani kakwambia hawaikubali, kwanini mnataka kuwaaminisha watu waamini utetezi wenu.
REDET kila chaguzi hawajawahi kuwa tofauti na matokeo
Nimeisha eleza hapo juu kukariri mambo kwa mazoea ndio ubaya wake huu.
usalama wa nchi upo chini ya vyombo vya usalama wa nchi sio NEC
 

Ndg paulss, hayo ni mawazo yako, kama unataka mtu aandae maswahiba (Timu) ndo agombee urais, basi wewe si mzalendo. Wewe unataka mtu aendelee kuharibu? nani kakudanganya uongozi ni uzoefu? Achana na umaskini wa kufikiri.
wewe ni sawa tu na mtu anayejiita Dr fulani(CCM) anayepigia piocha ya JK magoti kama ndo Mungu wake. Yaani, ubwege kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…