Chadema na mbinu ya lawama kupata huruma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema na mbinu ya lawama kupata huruma

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Paul S.S, Oct 10, 2010.

 1. P

  Paul S.S Verified User

  #1
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Wakati zikiwa zimebaki siku 20 kabla ya uchaguzi Oct 31, tuna shuhudia vyama vikiendelea na kampeni zao za kusaka ridhaa kwa wananchi kwa amani na utulivu wa kuridhisha kuliko chaguzi nyingi zilizopita

  Pia tunashuhudia wananchi wakipata mwamko zaidi wa kushiriki siasa kwa kuhudhuria mikutano ya kampeni kuwasikiliza wagombea wakinadi sera zao
  Kikubwa zaidi ni jinsi vyama mbali mbali vinavyotumia mbinu mbali mbali kuwashawishi wananchi majukwaani na nje ya majukwaa na hasa vyama viwili CCM na CHADEMA vinavyoonyesha kuchuana hasa hasa upande wa bara.

  Ndani ya majukwaa CCM wamekuwa wakieleza mafanikio yao na mikakati yao mipya kwa ahadi motomoto, wakati CHADEMA wamekuwa wakikosoa mafanikio ya CCM na kunadi mikakati yao mitamu sana masikioni ya siku 100 nk, kimantiki sina matatizo na hilo
  Matatizo yangu yanakuja pale CHADEMA wanapokuwa walalamishi kupita kiasi ambapo ni dalili ya kwanza ya kushindwa

  Niajabu kuona online polls mbali mbali zipo in favour of CHADEMA lakini wamekuwa kimya na kujisifu ili hali wakijua matokeo hayo hayana credibility yoyote sababu ni asilimia 1.5 ya watz mil40 wenye access ya net ndio wame vote tena hata mara 100 kwa mtu mmoja,
  Lakini REDET wametoa matokeo ya kisayansi imekuwa nongwa CHADEMA hawalali wanali matokeo yamechakachuliwa
  Mkuu wamajeshi ametoa tamko linalo husu usalama wa nchi kama vyombo vya usalama, wao wanaanza kuhoji na kulalama
  Tume ya uchaguzi imetoa idadi ya wapiga kura, kosa lawama tu kwa chadema
  Mara usalama wanapanga kuchakachua matokeo,Hata hapa jf ukiwa tofauti na CHADEMA utasikia mara umetumwa nk.yaani lawama kila kukicha. na nikisema niorodheshe lawama za chadema ambazo hazina mantiki nitajaza page 10

  Maranyingi namna hii ya lawama ni kutaka kuwaaminisha wananchi kuwa wao wanaonewa hivyo waonewe huruma na kupewa kura na pia kujiandaa pindi watakaposhindwa wapata sababu ya kusemea

  Mimi nadhani fanye tu kampeni zenu watu walisha chuja siku nyingi mchele na pumba, hii kulia lia sana itawafanya mtakaposhindwa uchaguzi mrudi mbweteke kama ilivyokuwa 2005 na kusubiri huruma ya wananchi kuwapa tena kura 2015 badala ya kujenga msingi na mtandao wa chama hadi sehemu walipo wapiga kura wa ukweli yaani vijijini

  Kuna kosa moja kubwa sana CHADEMA wanalo lifanya kutokujua nguvu ya CCM ipo wapi?
  Kudai tu tume mara masajili, polisi ni vya CCM hivyo tunaonewa haileti mantiki, wananchi wakiwaamini hata mtawala amiliki nini mtashinda tu
  Swali mmefanya nini muaminiwe kiasi hicho ikiwa hata ofisi za chama chenu zimewashinda kujenga?

  paulss
   
 2. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo hamtaki kukubali ukweli, wala hamtaki kujibu hoja za Chadema. Pale mnapotakiwa kujibu mnapindisha ukweli, sasa kwa nini tusilalamike? Kuna vitu vingine viko wazi na ukitaka kudanganya watu wanaelewa lazima wakucheke. Kingine ccm bado hamjakubali kuwa watz wa leo wamepuvuka kifikra zaidi ya wale mliokuwa mnawadanganya miaka mitano iliyopita. Tunahitaji sera na majibu ya shutuma mnazopewa siyo huu upupu wa taka taka.
  Mkuu inavyoonekana bado uko enzi za mwalimu, yaani ofisi nazo unataka ziwe kama za ccm kila sehemu? Duh kweli mkuu bado, ukubwa wa pua si wingi wa kamasi mzee. Angalia mfano hai bungeni wabunge wa ccm kibao lakini wanaishia kulala na kutoa majungu, lakini wapinzani wako busy kujenga hoja kwa ajili ya hili taifa masikini. Tunahitaji vision siyo ofisi za chama.

  Mwisho wangu, kama hupigi kampeni, na huna maslahi kutoka upande wowote kama mimi, basi nauhakika utapenda mabadiliko makubwa katika nchi yetu ili hatimaye tujivunie nchi yetu sote kuwa tumeijenga kwa ajili ya vizazi vijavyo.Lakini kama unaishi kiujanja kwa kupindisha ukweli basi utakuwa mmoja wa watu watakaojilaumu hapo baadae kwa kitendo unachofanya bila kuona mbali.
   
 3. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  ujanja ujanja tu. Hata vibaka waniga wafanyayo viongozi wa ccm
   
 4. P

  Paul S.S Verified User

  #4
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  DICTATOR hii yote ni inferiority complex kwa chadema
  na kwanini hamjiamini hasa, yaani tayari mmeishashindwa kisaikolojia kilichobaki ni kama mnatafuta sababu, mkuu lawama za kijinga ambazo hazijengi zimezidi
  Hivi hizi habari za kuchakachua matokeo mmetoa wapi, kuna matatizo gani mkuu wa majeshi kutoa tamko, kuna tatizo gani kwa RIDET kutoa walichopata ktk tafiti zao, mkuu siasa sio kuoneana huruma mkuu kwa kuwajaza watu ujinga waamin chadema inatengenezewa mazingira ya kupokwa ushindi wao
  Nakubaliana na wewe wabunge wa chadema walifanya kazi nzuri bungeni kwa maana ya rahisi kujua yai bovu lakini si rahisi kulitaga yai zima
  Mkuu hatuangalii sera pekeyake kwani kuna chama chenye sera mbaya, nahakika hakuna isipokuwa kama unashindwa kujenga chama chako mwenyewe kwa kujenga walau ofisi zenu tu wakati mwingine inatia shaka, anyway tuachane na ofisi
  Mkuu napenda sana mabadiliko lakini kwa upande wa ubunge, upande wa urais bado mnahitaji kazi ya ziada kutushawishwi tuwaamini
   
 5. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  paulss, wake up!
   
 6. admissionletter

  admissionletter Senior Member

  #6
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wewe 'paulss' lawana za Chabema ni 'natural' sababu misingi ya upinzani Tanzania haikuanza kwenye 'equal footing' kwa wapinzani. Maana yake ni kwamba, CCM tayari walishahodhi nguvu zote pamoja na rasilimali ambazo hapo awali zilikua za serikali. Kwa upande wa rasilimali, kama kuna haki rasilimali zilizoangukia CCM wakati vugu vugu la vyama vingi lilipoanza, zingetakiwa vile vile zigawiwe kwa vyama vya upinzani kwa sababu zilipatikana kwa fedha zetu wakati huo wa chama kimoja - 'anyway' hilo hi somo lingine! Lawama za wapinzani zinatokana na kukosa 'trust' kwani hata vyombo vya serikali ambavyo vingetakiwa kuwa 'neutal' kipindi hiki, tayari vimeshaonesha wazi wazi kupendelea CCM. Mfano mzuri ni vyombo vya habari kama gazeti la 'Daily News' etc. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ni mteuliwa wa Rais. Kama hakutakuwa na mabadiliko ya Katiba yatakayowezesha kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi, Ofisi Huru ya Msajili wa Vyama Vya Siasa, etc hizo hofu 'suspicion' zitaendelea kuwepo. Kwa maelezo haya utakubaliana nami kwamba ni vigumu Tanzania kwa vyama vya upinzani kujenga hiyo Misingi imara na mitandao unaosema kwa 'simple reason' kwamba mazingira hayaruhusu. Yanayotokea sasa Tanzania yameshatokea nchi nyingine ambapo baada ya watu kuona hakuna misingi ya kuendesha upinzani, waliamua kutumia nguvu na kuingia mitaani kudai haki zao. Mabadiliko ya katiba yaliyofanyika Kenya ni matokeo ya jitihada za namna hiyo....
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Madhara ya kupungukiwa uzalendo na nchi yako ndo ayoooooooooooooo
  Lazima uwatete CCM kama wanakunufaisha thats common sense
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ufisadi uliokithiri ndiyo huwafanya CCM wasione zaidi ya urefu wa pua zao. Lakini watu kama akina paulss na wengine hutupiwa makombo tu (if at all) na kulazimishwa kulamba m***** ya hao wenye kuipeleka nchi hii pabaya! Wake up paulss. Komboa nchi yako!!
   
 9. P

  Paul S.S Verified User

  #9
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu nipo macho sana
  Mkuu nakuhakikishia hizo nguvu za CCM na equal footing haitakuwa na nguvu yoyote kama kweli CHADEMA itafanya ushawishi ambao hautaishia kulaumu tu na kungojea kudra za Mungu, kutumia nguvu nyingi wakati huu wa uchaguzi kwa kuwaambia wananchi mtawala kakosea hichi na hicho haitoshi mkuu,
  Huko kenya Kanu ilikuwa kama CCM lakini wapinzani walifanya kitu pamoja na KANU kuhodhi kila kitu, ingawa baadae hao waliokuwa wapinzani wakaja kuwa wabaya zaidi kuliko hata Kanu, na damu ikamwagika, kitu ambacho tunakiogopa hapa kwetu kuwa uongozi si kitu cha majaribio ni lazima wapinzani wajipange vizuri
  Ndio maana nasema kwa ubunge sawa lakini urais bado
   
 10. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  watu kama paulss natamani wangekufa wote maana kwa vichwa maji kama hivi nchi lazima ididimie
  nakuombea sana kama inawezekana wewe na wenzio wote mnaotupeleka pabaya watanzania mpumzike kwa amani
   
 11. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  CHADEMA HAILALAMIKI LALAMIKI KAMA UNAVYOSEMA ILA INATAKA FAIR PLAY WENZIO HAPO JUU WAMEAANZA KUELEWA SOMO
   
 12. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  paulss

  Kama unaweza kuyaita maswali haya ni ya kupuuzi basi hujui siasa ni ushabiki umeweka mbele

  1. Kuhoji idadi ya wapiga kura kwenye daftari la kudumu
  2. Jeshi kuingilia siasa

  Achana na mambo ya tafiti na polls ambazo mtu yeyote anaweza kuzitengeneza na kuziita ni za kisayansi, hayo mawili ni muhimu kuyajua kama wewe na mwanasiasa makini.
   
 13. P

  Paul S.S Verified User

  #13
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu ninauzalendo sana nchi yangu na nafaidika na CCM au naumia kama wewe na yule
  Mkuu mimi si fisadi ndugu yangu ispokuwa nauangalia huo ukombozi kwa njia nyingine tofauti na yako ambayo unadhani ndio sahihi kila mtz kuiamini, ur wrong
   
 14. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mkuu wanasia wa CCM ni wa kubumba, hata logical thinking zao hazifanyi kazi
  nadhani wana CCM wengi na wafuasi wao wana mtindio wa ubongo, hivyo uelewa wao ni mdogo sana kaka
  Mijitu mingine mikubwa na ukiitazama unaona kama vile akili zimo, ila utakuta inatetea upuuzi wa CCM
  Yaani majitu mengine bwana
  Mungu tusaidie maana, sijui!
   
 15. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Kuna biashara ya kuuza bangi humo ndani? Nionyesheni iko sehemu gani?
   
 16. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  I said, wake up! Naona huelewi kuwa tumechoshwa na ccm especially uongozi wake (Kikwete). ccm wangejirekebisha Chadema leo isingekuwa na mvuto kiasi hicho. For your information, wengi wetu humu tunaopinga ccm tuna kadi za CCM (yangu ni ya tangu 1977) na sio wanachama wa vyama vingine. We want change, whatever it is, tumechoshwa na sera za ccm za kuibia taifa, usultani na kudanganya wananchi kuwa ccm ndio mtetezi kumbe ndiye muuaji wao. Mwingine akija, Chadema, au CUF etc nao wakivurunda tutawapiga boot vile vile, mpaka wote waelewe kuwa wapo kwa ajili ya wananchi na sio vice versa.
   
 17. P

  Paul S.S Verified User

  #17
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Luteni with all due respect
  Daftari la kudumu la wapiga kura kwani lina matatizo gani mkuu tatizo ni kuwa ninyi mnahisi limechezewa kwa kuleta calculation zenu sijui mmezipata wapi
  Mkuu jeshi halijaingilia mambo ya siasa, unajua kufanya mambo kwa mazoea na kugeuza sheria ndio matatizo yake haya, mkuu wa majeshi ametoa tamko kama vyombo vya ulinzi na usalama sasa kuna tatizo gani ? au ulitaka aseme IGP ndio ungeridhika, kweli mazoea mabaya
  mkuu tatizo mnaendeshwa na hisia hata pasipo stahiki, ingawa najua mnamadai ya msingi ila si katika hili
   
 18. admissionletter

  admissionletter Senior Member

  #18
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama unapenda mabadiliko, fuata sera za mabadiliko na viongozi ambao unaona wanaweza kutekeleza sera hizo. Kama unahitaji Rais anayepigia kampeni wabadhilifu, ambaye ameshindwa kuonesha ni vipi tutaondoka kwenye umasikini wakati tuna maziwa makubwa kabisa katika Afrika, bahari, Ardhi nzuri, madini, Mlima Kili pamoja na 'AMANI' basi angalia ni yupi ataleta mabadiliko. Kama umeshajaribu kundi fulani la uongozi na halikutimiza matakwa yako basi jiulize ni wapi wengine wanaweza kutimiza vision yako ya maisha bora. Kama unaona ni sawa ndugu zako wasome shule za kajamba nani wakati watoto wa wenzako wanasoma academy kwa fedha zako, kama unaona sawa wewe na ndugu zako mtibiwe kwenye hospitali zenye harufu wakati wenzako wanatibiwa Afrika Kusini na India kwa fedha zako, kama unaona ni sawa kwenda kwenye kampeni na kuburudishwa na 'fiesta' ya bongo flavor halafu wewe unaenda kwenye dala dala wakati mwenzako anarudi nyumbani na gari yenye AC iliyopatikana kwa fedha ulizoibiwa wewe... basi uamuzi ni wako ndugu yangu...
   
 19. m

  mosesk Member

  #19
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanini wewe unaamini taarifa ya REDET ambayo imwewahoji watu wasiozidi 3000 kati wa nwapiga kura milioni kumi na tisa ambayo ni sawa na 0.016% mbona hiyo hushangai si afadhali ya JF ambayo idadi ya wanaopiga polls ni zaidi ya elfu sita. Tatizo la wakereketwa ni hofu, mabadiliko ni lazima mchachue kura msichakachue!
   
 20. P

  Paul S.S Verified User

  #20
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu admissionletter napenda sana mabadiliko ila nayaangalia kwa upande wa pili wa shilingi tofauti na wewe, naamini zaidi kuingiza wabunge wengi waupinzani bungeni ili Vyama vijijenge zaidi Siamini hata kidogo ktkt kumpa Slaa urais kwa sasa, hana timu ya kuongoza taifa hili kwa ahadi anazo zitoa
  Sababu siamini kabisa katika sera za kila mtu kumiliki gari lenye kiyoyozi
  cha muhimu nikuingiza wabunge zaidi ili wapate uzoefu zaidi na kujenga vyama kisha uraisi utakuja
   
Loading...