Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
Kwako Mh Msigwa.
“JPM hana sababu ya kutoa sababu kwa nini amewateua KITILA NA ANNA, Sina uhakika kama waliwahi kuwa wapinzani au walikua na kazi Maalum?”
Hayo ni maneno yako Mh Msigwa, ni vijembe na uchokozi kwa viongozi wetu na chama chetu, na siku zote nyie CHADEMA ndiyo munatuanza, tukiwajibu, mnalalamika na kugeuza maneno kuwa “ACT inapambana na CHADEMA badala ya CCM”, Hivi kweli nisikujibu kwa kuchelea kusemwa kuwa napambana na wapinzani wenzangu? HAPANA, hakika, HAPANA, lazima ujibiwe tu.
Peter Msigwa hwenda kweli Mama Anna na Prof Kitila hawakuwahi kuwa wapinzani, sababu tafasiri ya upinzani kwenu ni kufanya mambo kama nyumbu au zwazwa, na kama uzwazwa na unyumbu ndiyo upinzani ulioumaanisha, hakika Prof Kitila Mkumbo na mama Anna Mghwira hawakuwahi kuwa wapinzani na nina hakika huenda wasiwe wapinzani abadani!.
Na kwa sababu hiyo, na kwa upinzani wa tafasiri yako nina mashaka na uzalendo wako pamwe na matilaba yako, na kwa vyovyote vile kama CHADEMA, viongozi wake ndivyo mlivyo, bi maana, viongozi wa twabia kama hizo na kama twabia hizo mwazilisisha kwa chipukizi wenu, na kama twabia hizo ndizo zinazounda misingi ya chama, ndugu yangu nakwambia, CHADEMA kitakuwa chama chenye uvunjifu mkubwa wa demokrasia, chenye kufanya ukatili mkubwa ili muradi kisalie kwenye mamlaka na chama chenye machafu mengi kuliko vyama vyote katika historia ya AFRIKA.
TWENDE SOTE NISIKUACHE MCHUNGAJI.
Mosi.
Wakati viongozi wa CHADEMA wanapinga udikteta wa Magufuli, wenyewe wanafanya udikteta mkubwa wenye kuzidi hata wa Magufuli. Mbowe kabadili kipengele cha ukomo wa uongozi kinyemela kwa minajili ya kuendelea kubaki kuwa mwenyekiti pamoja na kwamba wakati wake umekwisha, hivi, mtu kama huyu na chama kama hiki, kitashindwa kubadilisha katiba ili kisalie madarakani?
Nimesema upinzani wenu mnaotaka sisi ACT tuufuate ni wa kinyumbu na kizwazwa, sababu lile mnalolipinga ndilo hilohilo mwalifanya ndani ya chama chenu, sasa huu kama si unyumbu ni kitu gani? Je, mtakubali upinzani wetu kwa kutofanya yale tunayoyapinga?
Pili.
Wakati munampokea Lowassa, nyote mukaungana na Lowassa kuikosoa CCM kwa kutumia ujanjaujanja kukata jina Lowassa na hatimaye Magufuli akawa mgombea. Wakati mkiilaumu CCM kwa hilo, kipindi hichohicho, ndani ya chama chenu mkamfanya Lowassa kuwa mgombea wenu na mgombea wa UKAWA kwa njia za kitapeli ambazo hazivumiliki kabisa na waumini wa demokrasia, yaani aula ya ujanjaujanja uliofanywa na CCM kuliko utapeli uliofanyika CHADEMA.
Kati ya CHADEMA na Lowassa mmoja kati yao ni mtapeliwa na mmoja ni mtapeli, na mtapeli na mtapeliwa watajulikana kuendea uchaguzi wa 2020. Msigwa huu utapeli, ndio upinzani wenu munaojitapa nawo? Kama ndiyo heri Prof Kitila na Mama Anna wasiwe wapinzani.
Tatu.
Uchaguzi wa CHADEMA kanda ya Nyasa, ulikufanya wewe Msigwa kuwa mwenyekiti wa kanda. Hata hivyo, ni nani asiyejuwa kuwa Mbowe kuingilia uchaguzi ule na bahasha ya kaki ndiyo sababu ya wewe hivi sasa kuwa mwenyekiti wa kanda? Wakati CCM ikiwaamini vijana wake katika nyadhifa mbalimbali, ACT ikiwaamini vijana wake katika nyadhifa mbalimbali na kubwa tu, lakini CHADEMA inaipinga CCM na ACT katika hili kwa kukumbatia vizee ndani ya chama.
ACT imewaamini na kuwapa nafasi John Patriki, Edna Sunga, Ado Shaibu, na wengine kadhaa katika nyadhifa za kitaifa ndani ya chama, na CCM tunawaona Polepole, Makonda, Hapi, na Gambo, na wengine kadhaa, lakini nyinyi CHADEMA mumeipinga ACT na CCM kwa kumfanyia figisufigisu Sosopi asiwe mwenyekiti wa kanda. Upinzani huu ndiyo munajitapa nawo?? Kama ndivyo, heri Mama Anna na Prof Kitila wasiwe wapinzani.
Nne.
Vyama vyetu Tanzania vimeanzishwa kwa lengo kushika dola, lakini kwetu sisi ACT kushika dola ni njia kuu na msingi mkuu wa kufikia lengo la kuanzishwa chama chetu, na lengo hilo si lingine ni kuwaletea maendeleo watanzania na kuondowa kila aina uonevu na unyonyaji katika maisha yao ya kila siku.
Na hatuwezi kukaa chini tusubiri kukamata dola ndiyo tutimize lengo hilo, kutimiza hilo ni mchakato, mchakato huo tumeshaanza kuufanya sasa na tutauendeleza zaidi tukikamata dola. Maendeleo na kuondosha uonevu na unyonyaji ni mambo yenye maslahi na taifa, na chama chochote na mtu yeyote tutashirikiana naye midhali mambo haya mawili na yanayofananayo yatakuwa msingi wa mashirikiano yetu.
Ndiyo maana Mbowe alipoonewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam juu ya suala la mihadarati, chama chetu hakijamuacha, kilimtetea na kukemea uonevu ule. Hata, CCM na serikali inapofanya mambo yenye maslahi ya taifa nayo tutaiunga mkono na kushirikiana nayo. Hii ndiyo tafauti yetu na vyama vingine vya upinzani na ACT, sisi tumedhamiria kuleta mapinduzi ya kisiasa ili vyama vya siasa vijipe wajibu wa kuleta maendeleo na si kuhangaika kwa kuitafuta dola kwa udi na uvumba, sababu unaweza kuipata, kwakuwa huna malengo ya maendeleo, basi utaishia kufanya uovu kuuzidi wa CCM.
Mwisho.
Upinzani wenu wa kupinga kila kitu kutoka CCM na serikali, na kama mkikubali kitu basi hicho kitu kina maslahi ya moja kwa moja kwa Mbowe na genge lake, huu ndiyo upinzani wenu ambao mnataka ACT tuufuate, jambo hilo haliwezekani kulingana na misingi ya chama chetu, nyie endeleeni kumtapeli Lowassa fedha zake hadi afe kwa shinikizo la damu, ila juweni, kuna siku ya kula na kuna siku ya kuliwa, huenda leo mwaona mwamtapeli Lowassa, lakini jihadharini naye asije watapeli sababu nyote mmekutana WAPIGAJI.
Imeandikwa na
Dotto Rangimoto Chamchua.
[HASHTAG]#JiniKinyonga[/HASHTAG] [HASHTAG]#NjanoTano[/HASHTAG]
Simu 0622845394 Morogoro