CHADEMA na KUSADIKIKA...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Katikati ya miaka ya 60,Nguli wa utunzi wa Vitabu na Lugha ya Kiswahili,Hayati Shaaban Robert alitunga Riwaya ya Kusadikika. Humo,akamtumia Waziri Mkuu Majivuno wa Kusadikika kama mhusika mkuu. Yumo pia kijana Adili ambaye alishtakiwa Barazani/Mahakamani kwa kuwa Mwalimu wa 'ukweli'. Kesi ya Adili ilikuwa ya kuwaambia watu ukweli. Mwisho mwishoni Adili alishinda. Kesi hii ya Kusadikika naifananisha na kesi wanayosukumiwa CHADEMA. Akina Majivuno wa CCM hawapendi ukweli unaofundishwa na CHADEMA. Watafanikiwa?
 
Sasa hivi kilema cha Majivuno(CCM) kimejulikana.Hawezi tena kuuficha mwendo wake wa kuchechemea atembeapo. Viatu vyake alivyopewa avivae havimtoshi,vinampwaya! Majivuno anatakiwa aikubali taraka anayopewa na watu wake ili waweze kuchagua na kufuata chama kingine wakipendacho ili mapenzi yao yatimie.
 
Rafiki, hako ka-heading kako unaweza kufikiria kukabadili kidogo ile kaendani na ujumbe uliokusudia?

Asante
 
Katikati ya miaka ya 60,Nguli wa utunzi wa Vitabu na Lugha ya Kiswahili,Hayati Shaaban Robert alitunga Riwaya ya Kusadikika. Humo,akamtumia Waziri Mkuu Majivuno wa Kusadikika kama mhusika mkuu. Yumo pia kijana Adili ambaye alishtakiwa Barazani/Mahakamani kwa kuwa Mwalimu wa 'ukweli'. Kesi ya Adili ilikuwa ya kuwaambia watu ukweli. Mwisho mwishoni Adili alishinda. Kesi hii ya Kusadikika naifananisha na kesi wanayosukumiwa CHADEMA. Akina Majivuno wa CCM hawapendi ukweli unaofundishwa na CHADEMA. Watafanikiwa?

....hivi naweza pata wapi kitabu hiki...pamoja na kile cha Adili na Nduguze?
 
Usimwamshe aliyelala utalala wewe. Waache ccm walale hata hivo mda wao umekwisha. Its time for chadema kuchukua nchi
 
Katikati ya miaka ya 60,Nguli wa utunzi wa Vitabu na Lugha ya Kiswahili,Hayati Shaaban Robert alitunga Riwaya ya Kusadikika. Humo,akamtumia Waziri Mkuu Majivuno wa Kusadikika kama mhusika mkuu. Yumo pia kijana Adili ambaye alishtakiwa Barazani/Mahakamani kwa kuwa Mwalimu wa 'ukweli'. Kesi ya Adili ilikuwa ya kuwaambia watu ukweli. Mwisho mwishoni Adili alishinda. Kesi hii ya Kusadikika naifananisha na kesi wanayosukumiwa CHADEMA. Akina Majivuno wa CCM hawapendi ukweli unaofundishwa na CHADEMA. Watafanikiwa?
Ni kama vile mimba inapokua changa kwa mwanafunzi, ataibanabana huku akiwa amesahau kama inakua!!Ccm imepewa mimba na raia wake kwa sasa inahangaika kuwazalia maendeleo maana bado inabanabana
 
Back
Top Bottom