Umekariri siasa za kizamani za Lumumba sijui buku 7. Dunia ya sasa mambo yako viganjani na kichwani.Lema amegeuka chanzo kikuu cha mapato cha "Buk7" kwa vijana wa Lumumba. Sasa ni kumjibu kila asemacho na kukipinga. Leo Lema akisema vijana waache tabia ya kubet kesho tuu atavamiwa na kuambiwa Betting imewatoa vijana na serikali inaingiza kodi aache wivu. Buk7 wameishiwa.
Wewe Kinoamiguu ndio chizi kwa sababu maandiko unayoweza kuyaelewa ni yale yenye matusi tu.ungekuwa na akili japo kidogo ungesema LEMA katukana matusi gani haswa? unaishia kubwabwaja tu bila hata kufuata alama za uandishi?
chizi wewe
laana ni tusi? howWewe Kinoamiguu ndio chizi kwa sababu maandiko unayoweza kuyaelewa ni yale yenye matusi tu.
Jibu mambo ya msingi kuhusu PPE na vifaa kinga vya bodaboda badala ya kuleta Upumbavu wa matusi ya kichadema humu.
Tunawaambia kwamba hamna sera bali vituko na matusi tu.
Lema akiwa arusha si alitukana jukwaani akimwambia nabii yule eti... "Shit men"
"Bodaboda ni laana" sio tusi?
'Vicoba ni laana" sio kejeli?
Wewe Chakaza endelea kuwaza unyumbu ....
Kama Bodaboda ndio ndoto ya vijana wa kitanzania.Kwa akili yako bodaboda ndio ndoto kubwa ya vijana wa Tanzania na kwa nini serikali haina Mpango madhubuti wa ajira kwa vijana
Siku nilimsikia Kuhani Musa akiwaambia waaumini wake kuwa ni fedheha kulalia godoro moja mpaka linakuwa chapati, hakuwa anawatukana bali kuwachochea kuwa na uona mpana zaidi
Ama kwa bodaboda wa Arusha utawafananishe na wavuta bangi wa Dar es Salam waloijaza kitengo cha mifupa MOI na kusababisha upungufu mkubwa wa vyuma vya kuunga mifupa
Think bigger
True say. Jamaa hana point kabisa anaropoka tu. Afanye arudi alikotoka kama mwanzake LissuModerators at JamiiForums..naomba mnapobadili au kuondoa topic,muwe reasonable...hii ni mara ya tatu.
Naweka mnahamisha ..naweka mnafuta...why?
Kuweni fair na sio biased otherwise toweni "Ban" ili mtu anaachana nanyi na kuendelea na mambo Mengine kwingineko!
Mnaacha topic nyingi sana humu, tena zenye kutukana hadi Marehemu kinyume na maadili ya kitanzania!
Lakini mnaondoa baadhi ya topic zenye kuwahusu baadhi ya wale tunaoona kama mnawakingia ngao....kwa mfumo huu mtaiuwa hii platform yenu taratibu....
#Maxencemello na mwenzako lifanyieni kazi hili jambo..
Sisi ni watu wazima hivyo hatuko humu kama burudani.
" Lema Toa Elimu Badala ya kutukana!"
Ndugu Godbless Lema ambae ni Muishiwa Mbunge wa Arusha zamani.
(sio mheshimiwa)maana hana huo ubunge kwa sasa.
Anaendelea kuzunguka nchini akitukana makundi mbalimbali ya kijamii hususan Bodaboda!..kama kawaida yake.
Na sasa ameirudia tena kauli yake safari hii akiwa Mwanza!
Mwanza!
Ambako ni kitovu cha wavuvi katika ziwa Victoria.
Nimetafakari maneno yake kwamba ..
"Bodaboda walioko kazini sasa,na wanaoongezeka ni dalili ya umaskini nchini."
Kwamba watakufa kwa "Neumonia" ndani ya miaka ishirini ijayo...(kwa utabiri wake wa vifo vya wenzake).
Baada ya hapo nikatafari pia mazingira ya wavuvi wadogo wadogo wa nchi mbalimbali Duniani.
Ambao huingia ziwani na Bahari kuu zote usiku kucha na kurejea nchi kavu asubuhi.
Na hii ni Lifestyle yao ya kila siku miaka nenda miaka rudi.
Na Mazingira ya kukesha majini kila usiku,wakinyeshewa na mvua kubwa na tufani za upepo.ni magumu kuliko Bodaboda ambao wanaendesha pikipiki zao nchi kavu.
Tena wakiwa wamevaa vifaa kinga kama Helmet,Jackets na hata Gloves kwa wale waelewa zaidi.
Sasa kwa uelewa wa Lema kuhusu vifaa kinga ....ingawa hawezi kuwa na takwimu zitokanazo na vifo vya Neumonia kwa Bodaboda Duniani.
Pia atueleze wavuvi wangapi wanakufa kwa :Neumonia" Tanzania na Duniani,kwa uelewa wake.
Aje atuambie ni kundi gani liko hatarini zaidi kati ya haya mawili.
Badala ya kutembea akibwabwaja bila kuwa na maelezo ya kitaalamu!
Badala ya Lema kubwabwaja bila kutoa njia mpya za kuikomboa kiuchumi hiyo jamii anayoibeza!
Ili kwamba labda Chadema wanayo njia tofauti ya kuwapanulia ajira...na aiseme ili tuichambue na kuielewa.
Anawatukana Bodaboda huku akiendelea kuwatumia kwenye misafara ya chama chake,huku akiwafitinisha na serikali iliyoko madarakani.
Anawatumia Bodaboda kama sera!
Lema anapaswa kuambiwa na aelewe kwamba...
Kila kazi ni hatarishi endapo haitakuwa na vifaa kinga kwa mtu anayetoa huduma husika.
Ndio maana hata madaktari wanakuwa na "PPE."
Wavuvi wanakuwa na "life Jackets" pamoja na vifaa vinginevyo ili kujikinga na baridi kali majini.
Ndio maana ya Bodaboda pia kutakiwa kuvaa "Helmet" imara na bora zenye kuwa pia na matundu ya kuchujia hewa.
Pamoja na "Jackets" imara ili kuwakinga na Upepo na Baridi.
Ndio maana wafanyakazi migodini wanapaswa kuvaa "Helmets","Safety boots" na "Safety Glasses."
Ndio maana hata Malaya na wazinzi wote wanapaswa kuvaa "kondomu" nk.
Kila kazi inaweza kupelekea ajali ambayo itasababisha kifo, pale ambapo vifaa kinga na vigezo sheria havitatimizwa au kutumika.
Kwa hiyo Lema anaporopoka maneno yake labda tuseme anawaongelea Bodaboda wake wa Arusha.
Ambao kwa ujumla ni watovu wa nidhamu ikiwemo kutotii sheria za usalama Barabarani zinazowapasa kuvaa vifaa kinga.
Badala ya kuvaa [emoji858] Helmet.. wao huvaa kofia maarufa Arusha kama "Boshore"
Badala ya kuvaa ma Jackets wao wengi huvaa sweta na kisha kutoboa "Exhaust" za Pikipiki zao na kugeuka kero kwa jamii Barabarani kutokana na kelele mbaya za pikipiki zao.
Lema wakanye wanao kabla ya kuwatukana!
wewe usiwe mpumbavu bhana. hakuna mtu aliyepinga usafiri wa bodaboda wala kwamba hazisaidii kutoa ajira. acha kuwapotosha watu.Kama Bodaboda ndio ndoto ya vijana wa kitanzania.
Je!
Walioko vyuo vikuu wanajiandaa kuja kuendesha Bodaboda.
Kwamba wote wapo pale kuchukua shahada za Bodaboda?
Makundi yaliyoko JKT na vyuo vingine vya ufundi nchini...
Je!
Wanasomea uzam8vu wa Bodaboda?
Je!
Kuna kazi isiyo na ajira kama vigezo vya usalama havikufuatwa na kutimizwa?
Je!
Huoni jinsi Bodaboda walivuosaidia kwenye sekta ya usafiri nchini.
Kwa maisha ya sasa,ingekuwaje bila Bodaboda?
Ni Mbowe na wewe ndio mnamudu usafiri binafsi labda na Chadema yote.
Watanzania wengine Bodaboda imekuwa mkombozi wao.
Sasa Chadema na viongozi wenu....
Kama mnapinga Bodaboda...
Nini njia mbadala mliyoibuni badala ya Bodaboda nchini?
Kama laana sio tusi nenda kamwambie mzazi wako, awe baba au mama yako.....laana ni tusi? how
laana ni tusi how
eleza kinagaubaga tusi lenyewe ni lipi bila kujiuma uma huku ukikimbilia kujificha kwenye matusi?
hiyo ccm yenye sera zimesaidia nn tangu uhuru zaidi ya wizi na ujambazi kma EPA, KAGODA, ESCROW, RICHMOND nk
Kwa ujumla wanakera!Zaman nilikua Kila thread nikianzisha ilifutwa for sure [emoji2]
Nikaanza kuwaza ntakua na mawazo ya Kiana harakati..
Nowadays nimekua neutral sana itakua sbb ya ubusy na kazi na majumumu ya kifamilia[emoji1672]
unatumia nguvu nyingiii. kunielewesha ambayo nayajua tayari. inachosha. twambie bodaboda wametukanwa vipi? vicoba wametukanwa vipi? kipi ni tusi pale na ukweli ni upi hapoKama laana sio tusi nenda kamwambie mzazi wako, awe baba au mama yako.....
Umwamnie hiviii.....UMELAANIWA!
Kama ana akili uone utakachopata toka kwake!
Laana ni bahati mbaya au maneno mabaya ya maapizo yanayotamkwa kumuelekea mtu fulani yeye mwenyewe au kitu fulani kinachomuhusu, kwa mfano; kazi, shamba, watoto, masomo n.k kwa makusudi ya kumdhuru mtu huyo au kitu kinachomuhusu. Kwa kifupi laana ni kinyume cha baraka.
Laana inaweza ikasababishwa kwa makusudi maalumu (mfano: laana ambayo ni matokeo ya dhambi za wanadamu) au pasipo kujua (mfano: laana ya kujitamkia sisi wenyewe), kwa njia zote hizi mbili laana inafanya kazi iwe kwa makusudi au pasipo kujua.
Laana, ili itende kazi ni lazima iwe imeunganishwa na nguvu fulani zisizo za kawaida, nguvu za ziada “supernatural powers”, nguvu hizo ni lazima ziwe zinazidi nguvu za mtu au kitu kinacholaaniwa. Nachomaanisha hapa ni kwamba, mdogo hawezi kumlaani mkubwa; shetani hawezi kumlaani Mungu, na mtu aliyesimama katika kweli na haki ya Mungu hawezi kulaaniwa na shetani kutokana na ile nguvu ya Mungu iliyomo ndani yake.
Kwa maana hiyo, kwa maneno yetu wenyewe au ya watu wa karibu nasi na matendo ya maisha yetu ndiyo sababu kubwa ya laana katika maisha yetu na vizazi vyetu vijavyo. Kwa sababu kila tunachokitamka na tunachokitenda kinafuatiliwa kutimilizwa na falme mbili tofauti; ufalme wa Mungu na ufalme wa shetani. Ni hakika na kweli, ufalme wa shetani hufuatilia hasa mambo ambayo ni hasi kuyatimiliza katika maisha yetu, kuwa mwangalifu sana.
@Kinoamiguu Wewe unabwabwaja kama Lema anae "kunoa miguu!"wewe usiwe mpumbavu bhana. hakuna mtu aliyepinga usafiri wa bodaboda wala kwamba hazisaidii kutoa ajira. acha kuwapotosha watu.
kama kweli wewe na wenzio mnajali hao bodaboda je mna mpango wowote wa maisha yao ya uzeeni baada ya kustaafu?
vipi kuhusu bima? je wakipata madhara kazini mnawafidiaje?
kama kweli mnawajali mbona wanaendesha bodaboda za mikopo kwann msiwakopeshe ili waendeshe maisha yao vyema
Unashndwa kutofautisha MATUSI vs UKWELI. unaishia kubwabwaja tu hapa kama kasuku
Huwezi kuelewa tusi maana wewe Kinoamiguu tayari ni tusi.unatumia nguvu nyingiii. kunielewesha ambayo nayajua tayari. inachosha. twambie bodaboda wametukanwa vipi? vicoba wametukanwa vipi? kipi ni tusi pale na ukweli ni upi hapo
Na hicho ndio hasa kinatengenezwa ili kujaribu kutafuta uungwaji mkomo toka kwa umma!Anaharibu kuwafitinisha kundi kubwa la wananchi Ili waigeukie Serikali kiumane!