MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Wahenga walisema, kujiona mjuzi kwa kila jambo kunaweza kukukosesha nafasi ya kujifunza na kupata hekima.
Viongozi wa CHADEMA kila siku wanatuaminisha wao ni akili kubwa na kwa maana hiyo hawana lolote la kujifunza kutoka CCM kwa sababu CCM ni akili ndogo! Ukweli ni kuwa viongozi wa CHADEMA wana akili nyingi zinazoondoa maarifa ya kisiasa.
CHADEMA ni sawa na ndege mjanja anayenaswa na tundu bovu.
Kilichotokea bungeni ni classic example ya ndege mjanja kunaswa na tundu bovu.
Baada ya CHADEMA kuwasilisha majina mawili bungeni ambayo waliyapeleka kimkakati wakifahamu yatapita bila kupingwa ili mkakati huo wa kisiasa uwasaidie katika jitihada ya kuyakomboa majimbo ya Mkoa wa Mwanza ambayo ilikuwa ni ngome ya CHADEMA kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015. Ikumbukwe kuwa majina hayo niya wanaCHADEMA wanaotoka katika Mkoa wa Mwanza ambao kutokana na hali ya kisiasa kwa sasa CHADEMA hawawezi kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa kwa sababu hawana Mbunge. Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza CHADEMA, Susan Masele hana nguvu za kisiasa za kufanikisha mikutano ya hadhara.
Baada ya mkakati huo wa CHADEMA, CCM waliamua kutumia delay tactics za kuwapumbaza CHADEMA ili wasipate muda wa kutafakari na kufanya marekebisho. Tactics hizo ni kujifanya wameyakataa majina wakijua kuwa kwa sababu wanasheria wa CHADEMA ni wabishi bila maarifa basi watataka kuonyesha kama wao ni wajuzi kisheria/kikanuni zaidi ya CCM kwa maana kuwa watalazimisha majina hayo mawili pekee yakubaliwe kuingia kwenye karatasi ya kura. Kwa kufanya hivyo, CHADEMA walihalalisha majina hayo mawili bila kujua kuwa wanachofanya ni kuicheza ngoma ya mkakati wa CCM.
CHADEMA walirahisisha kazi ya CCM katika kufutilia mbali mkakati wa CHADEMA katika mapambano ya kisiasa katika Mkoa wa Mwanza. Kama CHADEMA wangeleta wagombea zaidi ya wawili, mkakati wa CCM ungekuwa ni mgumu kufanikisha.
Baada ya Mbowe na Lissu kujivika kitanzi cha kisiasa kwa kutetea kwa nguvu uamuzi wa CHADEMA, wabunge wa CCM kwa umoja wao wakasisitiza ‘’ngoma isilale’’ kwa maana kuwa zoezi la kupiga kura lazima lifanyike hata kama ni usiku wa manane kwa sababu walichokuwa wanakitafuta wamekipata. CCM hawakutaka kuwapa CHADEMA muda wa kwenda kutafakari kwa kina matokeo ya walichokifanya. Wahenga husema, usimwamshe aliyelala.
Kura zikapigwa na matokeo yake aliyekuwa mbunge wa zamani wa Jimbo la Nyamagana, Ezekiel Wenje na Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha wamejikuta wakikataliwa kuwa wabunge wa EALA kwa kupata kura nyingi za HAPANA. Huku mawakala/wasimamizi wao ambao ni Lema, Lissu na Waitara wakibaki kuduwaa baada ya kura kuhesabiwa. That was a political sucker punch!
Matokeo haya yanaufanya mkakati wa CHADEMA kufa kifo cha ‘’mende’’ kwa sababu safari ya Masha na Wenje kuukomboa Mkoa wa Mwanza kupitia mgomgo wa ubunge wa EALA imefika kikomo kabla hata haijaanza.
Kilichofanyika bungeni ni CHADEMA kupigwa bao la ‘’kisigino’’. Politics is about timing and who gets what, when and how.
Ikumbukwe kuwa kinachofanyika ndani ya Bunge huwa ni Alfa na Omega. Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania katika Ibara ya 100(1), hakuna chombo chochote nje ya bunge chenye mamlaka ya kuhoji kinachofanyika/kilichofanyika ndani ya bunge kuhusiana na uhuru wa mawazo, utaratibu na majadiliano.
Kwa mtaji huu siwezi kupingana na wale wanasema Uongozi wa juu wa CHADEMA umefika kikomo kifikra na kwa maana hii ni lazima upumuzishwe. Wanatakiwa viongozi wakuu wapya ambao sio wanaharakati.