Mbona jibu lipo wazi haihitaji hata kuumiza kichwa, angalia matokeo ya uchaguzi mkuu 2010, idadi ya wabunge, madiwani na halimshauri zinazoongozwa na vyama husika ndipo utapata jibu sahihi,
Jibu unalo mwenyewe,chenye wabunge wengi ndo mashuhuri maana wananchi wamekikubali
Reaction ipi wewe mbona unatapa tapa, hebu soma comment yako ya kwanza kwenye hii mada mpaka hii ya mwisho ujione usivyoeleweka katika kujenga hoja zako, mara useme CUF kinahimiza waislam tu ndio wajiunge nacho huku kikiwafukuza (umetumia neno swaga) watu wasio waislam, hapo hapo tena ukagundua kwamba kumbe kuna mpaka wachungaji ndani ya CUF, ukabadilisha haraka kwa kusema CUF inatumia wachungaji lakini wachungaji feki (sijui kwa kipimo gani) kwa kuwakodi wapande jukwaani,what is this? Kwanini usisimamie kwenye hoja moja na kuitetea vizuri kuliko kutanga tanga
Hakuna mwenye shida na mchungaji kuombea mkutano. Ni jambo la kawaida, zuri, na la kheri. Tatizo, ni reaction ya wafuasi na viongozi wa CUF juu ya hayo "maombi". Natumaini tuko pamoja sasa.
Hapa CCM wanachekelea kuona vyama vya upinzani vinajaribu kumalizana. Simple divide and rule.
Kenya ilikuwa hivyo hivyo mpaka vyama vya upinzani viliposhtuka ndo KANU ikatoka madarakani.
kwanini chadema hampendi kuwa tested?mnapenda kusifiwa tu,mtaitawala hii nchi kidikteta nyie watu tukiwapa ridhaa
na nikitaka kujua umaarufu wa chadema na ccm nitumie njia hiyo hiyo au linapokuja suala hilo web site ya tume inakua haina mpango?chadema kwa kujipenda hamjamboSwali rahisi hilo... Fungua website ya Tume ya uchaguzi afu angalia matokeo ya Urais mwaka 2010!!
Unajitetea kwa nukuu ya Regia,,,,,post yako ina mapungufu na maudhui yake yana chembechembe za Ukanda, Ukabila na Udini,,,,,na inaonesha hauko tayari kwa mabadiliko,,,it was good to compare CUF/CHADEMA Vs CCM na si vyama vinavyopigania kuingia Ikulu,,,
All in all, ngoja tukupe majibu yako uyatakayo; KWA SASA CHADEMA iko juu hata CCM haiwezi kujiringanisha nayo, si tu mijini hata vijijini
Nimekupata mkuu, point ni divide and rule.Mkuu unakosea kidogo, sema CCM wanachekelea kwa kuona CUF wanawashambulia CHADEMA. kwani CDM wamewashambulia CUF?
Ukiangalia vizuri, kila mmoja (CUF NA CCM) wanajitahidi kurukia hoja za Chadema, au angalau kuongea jambo linalohusiana na Chadema. Hawana zaidi ya hapo.
Kwa nini tunachoshana kwa mambo yalio wazi, hakuma asiyejuwa nguvu ya cdm sio ccm wala cuf wote wanajuwa na wivu umewajaa ndo maana wanakiandama na kujaribu kukizima kwa kila mbinu ikiwepo udini, ukanda, mauwaji, hivi sasa limekuja uongozi na yatakuja mengine na yatapita.
Nikweli kabisa maana wabunge wake ni Himo, arusha Mjini, moshi Mjini na..., Lakini cuf kina wabunge na halmashauri kadhaa Tanzania bara na visiwani.Hapo kwenye red tu ndio pana kaukweli fulani
CUF ni chama kisicho na sera kimebakia na bendera tu! Hakuna umaarufu hapo zaidi ya kufadhili UAMSHOKumekuwepo na mtazamo tofauti juu ya kipi chama mashuhuri na pendwa zaidi kwa watanzania miongoni mwa vyama vikuu vya upinzani Tanzania,hapa navizungumzia cdm na cuf,wapo wanaosema chadema nguvu zake zinaazia namanga na kuishia njia panda ya Himo na wengine wanasema cuf ni mashuhuri na inapendwa zaidi kwenye ukanda wa pwani na kusini mwa Tanzania,lakini wapo wanaodai cdm ina nguvu Tanzania nzima kasoro zanzibar huku wengine wakisema hapana cuf ina mtandao mpana zaidi na safu ya uongozi iliyoshiba wakati huku wakidai chadema ina mtandao mdogo na safu nyembamba ya uongozi,wewe mwana jf CHADEMA na CUF kipi mashuhuri kwa watanzania???matusi na hoja nyembamba havina nafasi,tumuenzi mwenzetu Regia mtema(R.I.P. SIS)-Tukosoane, Turekebishane, Tuwajibishane, ndipo Tusameheane".