Chadema na ajira kwa vijana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema na ajira kwa vijana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by koo, Apr 18, 2011.

 1. koo

  koo JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  TATIZO LA AJIRA NCHINI

  Nimejaribu kufanya utafiti mdogo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita na kugundua uwepo wa gonjwa kubwa sana la uhaba wa ajira nchini. Kuna kila sababu ya wananchi wa taifa hili kuishi kwa furaha na amani wakifurahia matunda ya raslimali ambazo mungu kalijalia taifa. Kwatakribani miezi mitano sasa imepita tangu uchaguzi mkuu upite na wanasiasa hasa wa chama cha mapinduzi walikuja na orodha ya sababu ya kukosa ushindi wakishindo moja ya sababu walizo taja nipamoja na hasira za vijana kwa kukosa ajira.
  Ukichunguza kwa makini utagundua walikua wanakejeri vijana kwani swala la ajira wanalichukulia kama ukoma wanalizungumza kwa woga na hawataki kusema nini wamejiandaa kufanya kupunguza kero hii kwa vijana wakitanzania wenye taaluma mbalimbali ikumbukwe mwaka 2005 vijana wengi waliahidiwa ajira milioni moja na chakushangaza haijatoka takwimu yoyote kuhusu niajira ngapi zimetengenezwa mpaka sasa. Nidhahili swala hili linaogopwa na serikali kwa hofu kwamba wakilizungumza watashindwa kulitetea wanahofia kuamsha hasira wanayohisi vijana wanayo na wanajua nisababu gani zinawapa vijana hasira kwakukosa ajira katika nchi yao. Kunasababu kuu mbili nilizoziona kama chanzo cha woga wa serikali kujikita katika sera ya ajira.
  1) Ajira nyingi zinazopaswa kuwa nafasi za watanzania zimekaliwa na wageni kutoka nje ya nchi ambao serikali haina ubavu kuwaondoa ili nafasi hizo zichukuliwe na vijana wa kitanzani. Hii inatokana na ukweri kwamba kampuni nyingi kutoka nje ya nchi zina hisa na viongozi wetu na hao viongozi wamepata hisa hizo kwanjia ya kifisadi hivyo kukosa sauti katika kukemea maovu ikiwa nipamoja na swala la ajira, pia wanahofia kama watanzania wataajiri katika kampuni hizo watajua siri nyingi za ukwepaji kodi na ufisadi unaofanywa na viongozi nahivyo kuwaumbua.
  2) Uhaba wa mawazo ya ubunifu katika kukuza mianya ya ajira. Serikali imejikuta ikibuni miradi midogo midogo ambayo inanufahisha vigogo na kutengeneza nafasi chache za ajira ambazo haziendani na mahitaji. Hii inatokana na kukosa ubunifu, kuwa na ubinafsi wakuangalia maslai binafsi na kutokua na vipaumbele katika kupangilia maswala ya uwekezaji. Serikali imejikuta ikiwa nichombo cha kudesa mambo yaliyo shindikana katika nchi nyingine nakuja kuyatekelza kwa wananchi wakiwa na lengo la kushindwa ili hasara itakayo patikana iishie mifukoni mwao. Mfano swala la miradi ya kuzalisha nishati ya umeme haikupaswa kuwa chanzo cha utitili wa miradi midogo midogo yenye lengo lakuvuna pesa ukiangalia gharama za hiyo miradi utakuta ukiunganisha na kutengeneza mradi mmoja wa uhakika hata wakuzalisha mgw 8000 unakua umetengeneza ajira nyingi pia umeondoa tatizo la umeme kwa uhakika.
  WITO
  Napenda kuchukua fursa hii kukiomba chama cha CDM kuanzisha mchakato wa kuwasaidia vijana kujikomboa katika taifa lao. Najua mengine yanaweza kuchukua muda mrefu kutekelezeka lakini hili moja linaweza kupatiwa ufumbuzi mapema na ningeomba lifanyiwe maandamano nchi nzima ili kuwawezesha vijana kushiriki katika kujiletea nafasi za ajira swala lenyewe ni:-
  NAIOMBA CDM IFANYE UCHUNGUZI NCHI NZIMA KWA NAFASI ZOTE ZA AJIRA ZINAZOPASWA KUSHIKWA NA WATANZANIA KWA MUJIBU WA SHERIA LAKINI KIFISADI ZIMEKAMATWA NA WAGENI KISHA KUANDAA MAANDAMANO NCHI NZIMA KUSHINIKIZA KUONDOLEWA KWA WAGENI HAO ILI KUKUZA WIGO WA NAFASI KWA WAZAWA.
  Kwa uchunguzi mdogo kuna zaidi ya nafasi 15,000 katika sekta ya utarii zimekamatwa na wageni wakati kuna wazawa wenye sifa hizo pia kuna nafasi 70 katika kampuni ya ulinzi ya Security Group. Katika migodi ya madini kunanafasi zaidi ya 12,000 zilizo kamatwa na wageni lakini zinapaswa kukamatwa na wazawa pia katika sekta hiyohiyo kunauwezekano wakutengeneza nafasi zingine 23,000 ambazo watanzania wanafanyishwa kazi kama vibarua wakati wanapaswa kuajiriwa. Pia makampuni mengi ya usafirishaji yanayo milikiwa na watanzania wenye asiri ya kiasia yanawatumikisha wazawa pasipo kuwapa ajira rasmi inakuaje dereva anaendesha gari la miziko kwa miaka mitatu akiwa kibarua? Ndugu zangu CDM natumaini mtakua na nafasi kubwa sana yakuchunguza hili swala nakupata majibu muafaka sioni sababu yakuhairisha maandamano mala kwa mala wakati matatizo nimengi vijana tuko chini yamiguu yenu kwakua hatuna kimbilio linguine tunaomba msaada wenu katika hili.
  Kama sekta zote zitafanyiwa mapitio hakuna haja yakua na vibarua ajira zote zinapaswa kurasmishwa ili kupunguza wimbi la uhaba wa ajira serekali imekua kimya tumeizoea sitegemei CDM pia itakaa kimya.
   
Loading...