akelu kungisi
Senior Member
- Apr 2, 2012
- 115
- 20
Mkuu hiki ni kibaraza cha ma "great thinkers", ukiwa hauna hoja nyamaza! Habari za supu na chai ni utoto usiopimika!
Naona unamwongerea Jenelari Urimwengu wa Lai, Mtumaalufu kweri kweri!Naamini ukosahihi mimi namheshimusana huyujamaa anahekima na akiwamshauli wa chadema vemasana.TATIZO LA WATANZANIA HATUPENDI KUSHAULIWA SISI HUJIFANYA TUNAJUA KILAKITU.WAULIZE WATUMAALUFU KAMA AKINA ZITTO,MNYIKA MBOWE,LISSU,JANUARI,NK. KAMAWANAWASHAURI
Naona unamwongerea Jenelari Urimwengu wa Lai, Mtumaalufu kweri kweri!
kwani hapo kosa lake nini? kwanza kakujulia hali akaenda mbali zaidi kufaham afya yako kwa kuuliza kama umepata kifungua kinywa.. sasa wewe povu limekutoka kweli
hili ni wazo na ushauri mzuri.kama chadema wana nia ya dhati ya kumkomboa mtazania na 'uhuni' wa ccm na serikali yake hawana budi kutumia hekima na busara za wazee kama ulimwengu.umeelezea vema huyu mtu ni hazina kubwa ambayo inaelekea ukingoni bila kuwa utilized vizuri kwa manufaa ya taifa kwa sasa na for the coming generations.ni mkweli asiye na chembe ya unafiki si mchumia tumbo ana uwezo mkubwa sana wa kufikiri na kuchambua mambo,ana maono ya mbali.tuna bahati kuwa na mtu kama huyu lakini tunakuwa 'wapumbavu' kwa kutotumia busara zake kwenye mambo mengi yanayolisumbua taifa hili
Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikiujiuliza swali hili " Hivi serikali ya ccm kwa nini imeshindwa kumtumia huyu gwiji wa habari na mambo mengi ya kiutawala, uchumi, siasa na uongozi? "
Kwa hakika Jenerali Ulimwengu ni mtu wa aina yake! Ukisoma CV yake na mambo yake unaweza kugundua kuwa is a gifted person. Na hata anapotoa ushauri wake, maranyingi unakuwa mzito mno, wenye maono ya mbali yaliyojaa hekima na busara.
Kinachonishangaza ni pale serikali inapomuona kuwa ni "threat"! Hii inanishangaza sana! ( Rejea sakata la kunyang'anywa uraia na Mr Clean). Maranyingi amekuwa akitoa ushauri kwa maandiko yake katika vitabu, magazeti, vijarida , midahalo ya wazi na kwenye vituo mbalimbali vya runinga! Ninafahamu wazi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe alikuwa akiandika sana makala zake katika gazeti la RAI enzi hizo likimilikiwa Jenerali Ulimwengu.
Ninadhani kwamba huu ni wakati muafaka kwa CHADEMA kuitumia hii hazina ambayo jioni yake inakaribia mno! CCM siku zote hawapendi mtu anayesema ukweli na kuwakosoa kwa makosa ya waziwazi mfano wa ujambazi wa KAGODA, MEREMETA, RICHMOND, na ushenzi mwingi amabao hausemeki.
Jenerali Ulimwengu ni muwazi daima, anaitumia elimu yake kuyaainisha matatizo yaliyopo na kuyatolea majawabu pamoja na kuielimisha jamii ya Watanzania kuhusu elimu ya uraia.
Ninadhani CHADEMA huu ungekuwa wakati muafaka kumuomba huyu mzee awe mmoja wa washauri wenu katika chama.
Nafahamu pia ninyi wakuu wa CHADEMA huwa mnachungulia humu JF, naomba yachukueni mawazo yangu kwa uzito unaostahili!