CHADEMA msipuuze kuwekeza kwenye vijana

galaw

Member
Oct 1, 2016
13
75
Habari Watanzania.
Chadema wakati inapata kukubalika kwa watanzania moja ya mbinu yake ilikuwa ni kuwapa fursa vijina ambao kweli walidhihilisha ushupavu wao ktk siasa huku ccm waliamini ktk wazee na kuendelea kuwabinya vijana.
Hata hivyo kadri mda unavyokwenda kasi ile ya kuwaimalisha vijana ndani ya chadema inabaki stagnant kwani ni dhahiri vijana wengi waliopata fursa ndani ya chama na nje ya chama (chadema)wanashindwa kukua kisiasa wengi wao wanabaki kuwafanya siasa za jimbo badala ya kutanua wigo wao kitaifa.
Ifahamike ni lazma chama chochote cha siasa kuwa na matu ambao ni national figures ili kukikuza cham. Jambo hili limekuwa tatizo kubwa chadema kutotengeneza national figures nyingi iwezekanavyo kwani national figures ndani ya chadema ni chache na sura ni zilezile kwa mda mrefu bila kuongeza wengine kwa kuwakuza vijana kisiasa.
Chadema ifahamu ccm walibadilika na kuanza kuwapa fursa vijana na ss hv wanapuga hatua kwa kasi kuliko chadema iliyoasisi utaratibu huu.
Taifa hili asimilimia kubwa ya watu ni vijana na vijana wanafanya kazi ili kufanikia zaidi hvy chadema lazima iweke utaratibu wa kuwasupport vijana wote wanaonekana kuwa tija kwa chama na taifa kuliko kuwaacha kiholela kwn wanaweza potea ktkt.
Pia chadema iache utaratibu wa kuwakumbatia vijana viongozi wasio kuwa na uwezo wa kiungozi eti ilimradi wako karibu nao hii inaua ali ya watu walio na uwezo wa kiongozi na hawapati nafasi kwa sababu wasio na sifa wanakumbatiwa na viongozi wakuu wa chama.
Hata hivyo chadema lazma ikumbuke kukubalika kwake itategemea inavyoendelea kunitofautisha na ccm kwa kufanya vzr ndani na nje ya chama. Ikifika wakati wananchi wakashindwa kuitofautisha chadema na ccm ni hatari zaidi kwn wananchi hawataona sababu ya kuwapa nchi chadema sababu kuu ni kuwa maovu yaliyo ccm yako chadema. Chadema lazma ilejee kuendelea kujitofautisha na ccm kwa namna inavyofanikisha na kuamua mambo ndani na nje ya chama.
Chadema hakika imewafikia wananchi wengi na kwa maeneo mengi ya nchi isiishie hapo,chadema inapaswa kukaa kwenye vichwa na mioyo ya watanzania na ili hili lifanikiwe lazma kuwe na mikakati madhubuti. Ukweli ni kwamba nchi hii inahitaji upinzani imara zaidi ili kuzidisha kasi ya maendeleo ktk nchi.
Asanteni
 

Obuma

JF-Expert Member
Dec 28, 2015
2,731
2,000
Chadema kwa kweli imetoka mbali sana na imeonekana kujijenga vizuri ila kwa sasa inahitaji overhaul! Huwezi kuendelea na uongozi ule ule na watu wale wale na kwa mikakati ile ile ukategemea matokeo tofauti! Ni kama timu za mpira tu msimu ukiisha na mkaona hamjaondoka na kombe lolote na kikosi kimezeeka basi mnafanya overhaul na kuingiza wachezaji wapya na kocha mpya ili kubadili mbinu na kuwa na kasi mpya! Mimi ni muumini wa Mbowe sana ila kiukweli Mbowe ameshafanya ya kutosha na akili yake imefikia horizon!! Safu ya uongozi wa chadema inahitaji mabadiliko ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya sasa ya kisiasa! Wafuate mfumo wa wenzetu ulaya ukiona huna mchango chanya na ubunifu tena unakaa pembeni unakuwa mshauri
 

swissme

JF-Expert Member
Aug 15, 2013
13,660
2,000
vijana wa chuo tuliwaeleza wakawa wanatukana sasa wamekubali maneno ya chadema watakuja wale wenye huelewa tu hao wengine wanaosifia kukosa mikopo ya wanafunzi na wale waliokuwa chuo miaka 3 iliyopita sasa wanaisoma numbers.


swissme
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom