Chadema Moshi wamwashia moto JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema Moshi wamwashia moto JK

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mrefu36, Aug 30, 2010.

 1. mrefu36

  mrefu36 Member

  #1
  Aug 30, 2010
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Send to a friend Monday, 30 August 2010 09:08

  Daniel Mjema, Moshi
  MGOMBEA ubunge Jimbo la Moshi Mjini kwa tiketi ya Chadema, Philemon Ndesamburo jana alizindua kampeni zake huku chama hicho kikimlipua mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete kikidai anatumia vibaya fedha za umma kukarabati Ikulu.
  Chama hicho kimedai kuwa katika kipindi cha miaka minne ya mwanzo ya utawala wake, serikali yake imekarabati Ikulu kwa zaidi ya Sh23 bilioni ukilinganisha na Sh9 bilioni alizotumia rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.
  Kauli hiyo, iliyoegemea zaidi kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ilitolewa juzi na katibu wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Basil Lema katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho.
  Uzinduzi wa kampeni hizo ulitawaliwa na kila aina ya shamrashamra, ikiwemo helikopta ya Ndesamburo ambayo ikizunguka angani mjini wa Moshi tangu saa 8:00 mchana hadi saa 10:00 huku ardhini yakifanyika maandamano makubwa.
  Maandamano hayo, yaliyojumuisha waendesha pikipiki, msafara wa magari na mamia ya wananchi, ulianzia eneo la Majengo na kupita katika mitaa kadhaa hadi viwanja vya Manyema vilivyopo kata ya Bondeni.
  Akihutubia umati mkubwa wa wananchi na wafuasi wa Chadema, Lema alisema katika mwaka wa kwanza tu kuingia Ikulu, Rais Kikwete alikarabati makazi hayo ya rais kwa Sh6.1 bilioni ambazo ni fedha za walipa kodi.
  “Lakini mkumbuke kuwa katika kipindi cha mwisho cha miaka mitano, mtangulizi wake(Mkapa) alikarabati Ikulu kwa Sh 9 bilioni, lakini Rais Kikwete alipoingia tu Ikulu akaamua kukarabati Ikulu hiyo hiyo kwa Sh 6.1 bilioni,” alidai Lema.
  Lema alianisha matumizi hayo ya ukarabati wa Ikulu kuwa ni Sh6.1 bilioni (mwaka 2006), Sh5.59 bilioni (mwaka 2007), Sh 5.712 Bilioni (mwaka 2008) na Sh6.1 bilioni anazodai zilitumika kukarabati jengo hilo mwaka 2009.
  Katibu huyo alisema kulikuwa hakuna ulazima wa kutumia kiasi hicho kikubwa cha fedha za umma, hasa ikizingatia kuwa ndio kwanza majengo hayo yalikuwa yametoka kukarabatiwa kwa Sh9 bilioni.
  Halikadhalika katibu huyo alidai kuwa mwaka 2007 pekee, serikali ilitumia Sh447 bilioni kununua magari ya serikali, fedha ambazo zingetosha kuwalipa walimu mshahara wa kima cha chini wa Sh500,000.
  Lema alifafanua kuwa fedha zilizotumika kukarabati Ikulu kwa miaka minne ya Rais Kikwete zingeweza kujenga zananati 600 za kisasa kwa thamani ya sh40 Milioni kwa kila Zahanati inayojumuisha pia nyumba ya mganga.
  “Ukubwa huu wa matumizi ya serikali ndio unawafanya Watanzania waendelee kuwa masikini na njia pekee ya kuondokana na matumizi ya aina hii ni kuiingiza Chadema kwenye mamlaka ya kuongoza dola mwaka huu,” alidai.
  Ndesamburo, ambaye amekuwa mbunge wa jimbo hilo tangu mwaka 2000, alisema endapo atachaguliwa tena kwa kipindi cha tatu ataweka kipaumbele katika sekta za afya, miundombinu ya barabara za lami, elimu na usalama mjini.
  Ndesasumbo alisema endapo wananchi wataipa Chadema ridhaa ya kuongoza Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, atahakikisha hakuna mwanafunzi anayefaulu kwenda sekondari ambaye anashindwa kufanya hivyo kwa kukosa ada.
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Washeni tu moto ndugu chadema mkiuchochea vizuri sisi tuko tayari kuwachoma nao ccm pale october msikatishwe tamaa na akina makamba wapiga vijembe na wanaotumia ubabe kuendesha mambo.......
   
 3. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli, kwa kweli naaaaa paaaata kigugumizi, Mze Ndesamburo unahitaji heshima. Umeshirikiana na manispaa ya Moshi mmeubadilisha ule mji kabisa, ni msafi kila kona. Watoto wa ndugu zetu hapo Moshi mjini hawakosi ada, umesaidia mno, kuanzia elimu, afya, miundombinu, you name all. Keep it up mzee!!
   
 4. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli moshi ccm wanapaogopa kuliko ukimwi.
   
 5. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Moshi ni mji wa watu waliosoma na kupata maendeleo kwa haraka sana.
  Ni wafanyabiashara wenye vipaji vingi,wametawanyika dunia nzima,ni wapi utawakosa wachaga humu duniani?Kitu cha ajabu hutawaona wanajihusisha na mambo ya siasa,wako bisy zaidi na biashara zao.Lakini safari hii mhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!! nina wasiwasi mkubwa.
  Hata hivyo wengi ni fuata upepo tuu kama wale wa kule jimbo la siha ambao walimpitisha Mbunge wa ccm bila kupingwa.huu ni woga.ndio maana wakajitokeza watu kugombea kupitia chadema,nccr,tlp na cuf.
   
 6. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Najua CCM ni watu wa Fitna sana....Ila kwa mji wa Moshi sina wasiwasi kabisa....hata kama wasipokuwa watu wa kulipa fadhila bado hawatakua na sababu wa kutomchagua Ndesa kwa mambo aliyoyafanya pale Moshi...
   
Loading...