Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 49,681
- 39,012
Wanaukumbi.
Kwenye sakata la sukari nchini CHADEMA wanatuchanganya wananchi kutokana na kauli zetu.
Kila siku mnakuja na kauli tofauti leo mnapinga hiki kesho tena mnakikubali mlichokipinga. Tumsome Mwenyekiti wa CHADEMA na hii kauli yake;
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Freeman Mbowe ameitaka serikali kusitisha kutoa vibali kwa wafanyabiashara wakubwa vya kuagiza sukari kutoka nje ya nchi ili kulinda viwanda vya ndani ambavyo vimetoa ajira kubwa kwa watanzania.
Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mwamala, Bukene, Choma, Igurubi na mjini Igunga mkoani Tabora katika mikutano ya hadhara, mwenyekiti huyo wa CHADEMA amesema hatua ya waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda kutoa vibali kwa wafanyabiashara wakubwa kuagiza sukari nje ya nchi huku akijua kuwa fika kuwa viwanda vya sukari vya hapa nchini vinayo akiba kubwa ya sukari kwa mahitaji ya ndani inalenga la kuviua viwanda hivyo.
Akiwa katika kijiji cha Choma wilayani Igunga, mwenyekiti huyo wa Chadema ameilaumu serikali kwa kushindwa kusimamia bei ya mazao ya wakulima ikiwemo pamba na tumbaku na kusababisha wakulima kuwa maskini huku mwenyekiti wa taifa wa baraza la vijana wa Chadema ( BAVICHA ) Patrobas Katambi akisema laiti utajiri wa raslimali za gesi na madini uliopo nchini ungetumika vizuri, hakuna mwananchi ambaye angebaki katika lindi la umaskini uliotokea.