CHADEMA mnasemaje kuhusu gesi ya Mtwara?

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
5,139
Reaction score
1,149
Kwa takriban wiki 3 au 4 sasa kumekuwapo na sintofahamu huko kusini mwa Tanzania eneo linaloaminika kwamba liko nyuma kidogo kimaendeleo hapa nchini,sintofahamu hiyo imetokana na kugundulika kwa gesi kwenye eneo hilo..gesi ambayo serikali kuu ingependa kuona inaifadisha nchi nzima ikiwemo mikoa ya kaskazini hususan Kilimanjaro na Arusha lakini kwa namna moja ama nyingine wakazi wa maeneo hayo ya kusini kulikopatikana gesi wamekua na mtazamo tofauti, wao wangependa gesi hiyo iwe yao peke yao!

swali langu kwa vyama vya upinzani hususan chama kikuu cha upinzani bila shaka CHADEMA,je wao wanawaambia ama wanawaahidi nini wana kusini kama kwa mfano leo wanaachiwa nchi waienedeshe wao CCM ikae pembeni kama mtazamaji...je watakubaliana na wana Mtwara gesi iwe yao peke yao na kuwaudhi watu wa kaskazini,ziwa,mashariki na kwingineko ambao rasilimali zinazopatikana kwao wamekua wakishare na watu wa nchi nzima wakiwemo watu wa Mtwara????

Nawasilisha but naomba tuwe fair tu kwenye kuchangia hapa,ushabiki kupita kiasi wa vyama tuuweke pembeni,tujikite zaidi kwenye facts.

asanteni sana.
 
Wana Mtwara hawajakataa gesi kutoka Mtwara, aidha hujawaelewa au unapotosha kwa makusudi! Na naamini unapotosha

kama wewe ni mwenyeji humu huwezi kutoa kauli uliyoitoa!pata habari picha

Wananchi wa Mtwara leo wameandamana katika mitaa mbalimbali ya Mji huo kupinga uamuzi wa serikali kusafirisha gesi hiyo kutoka Mtwara Mikindani hadi Dar Es Salaam. Kabla hapo, mapema mwa mwaka huu, Chama cha Wananchi CUF pamoja na Chama cha Wafanyabishara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) mkoani Mtwara vilipinga uamuzi huo na CUF kutishia kuitisha maandamano kupinga uamuzi huo.

Picha kwa hisani ya Sizinga wa JF
 
Chadema ina Sera ya Majimbo, Faida ya Maliasili inabaki katika maeneo husika, kiasi kidogo kinakwenda kwenye Serikali Kuu kwa ajili ya kuendesha Wizara za Serikali kuu, kama:- Jeshi na Ulinzi, Elimu, Fedha, na Mambo ya Nje. Kwa yale Maeneo ambayo yana Rasilimali chache yanapata asilimia kiasi kutoka kwenye Maeneo yenye Rasilimali nyingi.
 
mKUU KWANZA LEKEBISHA MTWARA HAWAJASEMA WANATAKA IWE GESI YAO PEKE YAO!
 
Kuhusu suala la gesi, Dr Slaa aliulizwa hilo swali jana alipokuwa MOSHI kwenye mkutano, ila akasema hayukotayari kulizungumzia kwa sasa, hivyo analiandalia statement iliyoshiba ndipo atoe kama msimamo wa chama juu ya gesi na watu wa Mtwara.
 
Sera ya majimbo ya chadema iko wazi na haihitaji kukaza shingo ili uelewe msimamo wa CDM ukoje katika gesi kwamba ibaki mtwara na viwanda vifuate gesi pale kisha iende sehemu nyingine
 
Acha u.j.i.n.g.a wewe unapotosha ili iweje? Wana Mtwara hawajasema gas ya Mtwara iwe yao peke yao. Madai ya Wanamtwara wanataka rasilimali ya gas iliyogunduliwa Mtwara iwe chachu ya maendeleo ya mkoa wa Mtwara ambayo uko nyuma sana kimaendeleo.

HOW iwe chachu ya maendeleo? Mitambo ya ku-process gas ijengwe Mtwara badala ya Bagamoyo na Dar. Mitambo ya kuzalisha umeme wa gas ijengwe Mtwara na umeme kuingizwa kwenye gridi ya Taifa badala ya Bagamoyo na Dar.
 
mkuu kwanza lekebisha mtwara hawajasema wanataka iwe gesi yao peke yao!
ccm ai itulambee chani tuvamakonde? 1.ihimbulenge machine la medi kuchitangalii mkupelekeja kudodoma 2.mkuhimbulanga reli ichisafirisha mtesa mkunadenga kudasalama 3.vadombwelenge taa ja mwanga nkali ja uwanja wa ndege kuntwara nkunapelekeja arusha 4.vapapulenge nkataba wa kudenga lami kati ya kuntwara na malawi vanang,o nkupelekeja bagamoyo bado tuvalola chi, nelo vahimbanga mapondo mmawelu vatwale gesi vaipelekeje kudasalama,mme ne muve neko mkodolanga chi meho mwachi chimunu mchikalango! Kwani vazee vachilowa tangu vala vahwile?mma!!! Kudobwa hambi ane nalu kukutu munyopa dau unji walepi mchila. Ebo
 
Kwa takriban wiki 3 au 4 sasa kumekuwapo na sintofahamu huko kusini mwa Tanzania eneo linaloaminika kwamba liko nyuma kidogo kimaendeleo hapa nchini,sintofahamu hiyo imetokana na kugundulika kwa gesi kwenye eneo hilo..gesi ambayo serikali kuu ingependa kuona inaifadisha nchi nzima ikiwemo mikoa ya kaskazini hususan Kilimanjaro na Arusha lakini kwa namna moja ama nyingine wakazi wa maeneo hayo ya kusini kulikopatikana gesi wamekua na mtazamo tofauti, wao wangependa gesi hiyo iwe yao peke yao!

swali langu kwa vyama vya upinzani hususan chama kikuu cha upinzani bila shaka CHADEMA,je wao wanawaambia ama wanawaahidi nini wana kusini kama kwa mfano leo wanaachiwa nchi waienedeshe wao CCM ikae pembeni kama mtazamaji...je watakubaliana na wana Mtwara gesi iwe yao peke yao na kuwaudhi watu wa kaskazini,ziwa,mashariki na kwingineko ambao rasilimali zinazopatikana kwao wamekua wakishare na watu wa nchi nzima wakiwemo watu wa Mtwara????

Nawasilisha but naomba tuwe fair tu kwenye kuchangia hapa,ushabiki kupita kiasi wa vyama tuuweke pembeni,tujikite zaidi kwenye facts.

asanteni sana.
Hakuna haja ya kuumiza kichwa, Chadema kinaongozwa na SERA, soma sera ya MAJIMBO utaelewa msimamo wa Chadema kuhusu gesi ya Mtwara.
 
ccm ai itulambee chani tuvamakonde? 1.ihimbulenge machine la medi kuchitangalii mkupelekeja kudodoma 2.mkuhimbulanga reli ichisafirisha mtesa mkunadenga kudasalama 3.vadombwelenge taa ja mwanga nkali ja uwanja wa ndege kuntwara nkunapelekeja arusha 4.vapapulenge nkataba wa kudenga lami kati ya kuntwara na malawi vanang,o nkupelekeja bagamoyo bado tuvalola chi, nelo vahimbanga mapondo mmawelu vatwale gesi vaipelekeje kudasalama,mme ne muve neko mkodolanga chi meho mwachi chimunu mchikalango! Kwani vazee vachilowa tangu vala vahwile?mma!!! Kudobwa hambi ane nalu kukutu munyopa dau unji walepi mchila. Ebo
Hahahahaahaa.........Japo sijaelewa lakini nafikiri umemnyoosha Mpotoshaji Kim Kadash
 
Mimi nadhani jambo hili linatakiwa kutolewa ufafanuzi wa kitaalam kwa wanamtwara ili wajue watanufaika vipi. Prof. Muhongo alieleza vizuri sana katika kipindi cha dk.45 ITV, pia naibu waziri alieleza vizuri sana katika kipindi cha Kipimajoto Ijumaa 12/01/2013.

1. Kuna kiasi kikubwa cha gesi kinachosemekene kitabakia huko kwa ajili ya matumizi ya Viwanda vya Cement, Mbolea nk.
2. Pia gesi inaelekezwa DSM kwasababu tayari mitambo ambayo ipo tayari kutumia gesi hiyo kuzalisha umeme megawat kama 700 hivi.

3. Kuna viwanda vikubwa 34 DSM ambavyo vipo tayari kuconsume gas hiyo

4. Kwa tathmini iliyofanyika gharama za kujenga bomba kupeleka gas DSM ni ndogo ukilinganisha na gharama za kujenga mitambo mipya Mtwara.

5. Mtwara wamepewa umeme megawat 18 wameshushiwa service charge lakini mpaka sasa matumizi yao hayajafika hata megawat 10

6. Kuna asilimia fulani ya mapato yatakayotokana na mauzo ya gas itaingia kwenye halmashauri za mtwara kwaajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

My take;

1. Mtwara wakubali gas kwenda DSM kwani hata mitambo ikijengwa Mtwara still hawatapata ajira hapo kwani watahitajika watu wenye elimu za juu (experts) ambao huenda wasipatikane eneo ambalo gas inapatikana.

2. Wakiruhusu gas kuondoka na viwanda kujengwa hapo watapata ajira kwa wingi kwani kiwanda kinaajiri watu wote Wasomi wa elimu ya juu hata watu wa kawaida, so watakuwepo wataalam na wabeba mizigo, mama ntilie ataiza, wakulima watauza mazao yao, mzunguko wa pesa utaongezeka mtwara.

3. Wanamtwara wakumbuke kuwa hawana jeuri ya kuzuia gas kuondoka Mtwara, wasibabaishwe na kuandamaniswa bila sababu kwani hata gas isipoenda Dar hawatanufaika, ni bora iende nao wapate manufaa kidogo wakati majadiliano yanaendelea.

Nawasilisa.
 
walishasema walipokuwa kwenye mikutano ya m4c mtwara.sehemu ya matokeo ndio hayo.
 
My take;

1. Mtwara wakubali gas kwenda DSM kwani hata mitambo ikijengwa Mtwara still hawatapata ajira hapo kwani watahitajika watu wenye elimu za juu (experts) ambao huenda wasipatikane eneo ambalo gas inapatikana.

2. Wakiruhusu gas kuondoka na viwanda kujengwa hapo watapata ajira kwa wingi kwani kiwanda kinaajiri watu wote Wasomi wa elimu ya juu hata watu wa kawaida, so watakuwepo wataalam na wabeba mizigo, mama ntilie ataiza, wakulima watauza mazao yao, mzunguko wa pesa utaongezeka mtwara.

3. Wanamtwara wakumbuke kuwa hawana jeuri ya kuzuia gas kuondoka Mtwara, wasibabaishwe na kuandamaniswa bila sababu kwani hata gas isipoenda Dar hawatanufaika, ni bora iende nao wapate manufaa kidogo wakati majadiliano yanaendelea.

Nawasilisa.

Mkuu kumbe haujui kuwa kunafaida kubwa sana kwa wao kujengewa nitambo mtwara
1. wakulima na wafanyabiashara watanufaika na wageni watakaoenda mtwara kufanya kazi
2. barabara zitajengwa na kuiprove miundo mbinu ili hao wafanyakazi wawe confotable
4. mkoa utachangamka na kuwa highly populate
5. NK
 
Is ok, but kumbuka lengo si kuleta maendeleo mtwara pekee, gesi inatakiwa kuboost uchuni wa taifa zima kama ilivyo kwa rasilimalinyingine za nchi. Hizo faida zote ulizozitaja hapo juu bado zitakuwepo mtwara hata gesi ikisafirishwa kwenda Dar kwasababu gesi nyingi bado itabaki mtwara na viwanda vitajengwa pamoja na miundombinu mingine. Jambo kubwa la kulitilia maanani kwa sasa ni kwamba hiyo gesi ikibaki mtwara kwa sasa haina matumizi Dar es salaam ndio sehemu pekee ambapo mitambo ya umeme (Kuunganishwa kwenye grid ya Taifa na viwanda vipo tayari kutumia gesi hiyo kama nilivyoeleza kwenye post yangu. Gharama ya kujenga mitambo mipya mtwara ni kubwa kilichopitishwa kwenye bajeti ni ujenzi wa bomba.

NB: Si rahisi kuhamisha viwanda vilivyopo Dar vikaenda mtwara Industrial development haitegemei single factor (Power) kuna mambo mengine mengi.

Tunapaswa kuangalia maslahi mapana ya Taifa na si maslahi ya mtwara pekee kwani hii ni rasilimali ya Taifa si rasilimali ya Mtwara, naamini kwa kiasi cha gesi inayobakia Mtwara kasi ya maendeleo bado itakuwa kubwa tu, wala tusilipeleke jambo hili kishabiki.
 
Mkuu maslai ya taifa yapo palepale kinachotakiwa ni mgawanyo wa maendeleo sasa ges bado itazalisha umeme tutatumia nchi nzima hiyo hakuna ubishi, kama viwanda vitajengwa mtwara bado nchi nzima itanufaika, tatizo huwa mnavuta na kuacha empty eneo ambalo linazalisha wanauchungu na korosho pia mkuu, ukiuliza kwa nini mtwara na lindi haziendelei au ziko nyuma kimaendeleo hv mkuu unajua majibu yake? hayo majibu ndo wanamtwara hawayataki tena!
 
Kwa takriban wiki 3 au 4 sasa kumekuwapo na sintofahamu huko kusini mwa Tanzania eneo linaloaminika kwamba liko nyuma kidogo kimaendeleo hapa nchini,sintofahamu hiyo imetokana na kugundulika kwa gesi kwenye eneo hilo..gesi ambayo serikali kuu ingependa kuona inaifadisha nchi nzima ikiwemo mikoa ya kaskazini hususan Kilimanjaro na Arusha lakini kwa namna moja ama nyingine wakazi wa maeneo hayo ya kusini kulikopatikana gesi wamekua na mtazamo tofauti, wao wangependa gesi hiyo iwe yao peke yao!

swali langu kwa vyama vya upinzani hususan chama kikuu cha upinzani bila shaka CHADEMA,je wao wanawaambia ama wanawaahidi nini wana kusini kama kwa mfano leo wanaachiwa nchi waienedeshe wao CCM ikae pembeni kama mtazamaji...je watakubaliana na wana Mtwara gesi iwe yao peke yao na kuwaudhi watu wa kaskazini,ziwa,mashariki na kwingineko ambao rasilimali zinazopatikana kwao wamekua wakishare na watu wa nchi nzima wakiwemo watu wa Mtwara????

Nawasilisha but naomba tuwe fair tu kwenye kuchangia hapa,ushabiki kupita kiasi wa vyama tuuweke pembeni,tujikite zaidi kwenye facts.

asanteni sana.
kwa kuwa wanachadema tumewaelewa wana mtwara kwamba wanachotaka ni kusafirisha gesi ikiwa tayari imetengenezwa tutaakikisha mitambo ya michakato ya gesi inawekwa mtwara na ikibidi mitambo ya umeme ijengwe mtwara ili usafirishwe umeme kupitia grid ya taifa kwenda mikoa yote ya tanzania
 
Wana Mtwara hawajakataa gesi kutoka Mtwara, aidha hujawaelewa au unapotosha kwa makusudi! Na naamini unapotosha
anapotosha kwa makusudi na hili ndilo wanvyofanya wanamagamba,wanapotosha ili wapate sababu ya kuwatukana watu wa mtwara,wanachosema mtwara kigine ccm wanasema vingine awajui kwamba kwa kufanya hivyo ni matusi kwa watu wa mtwara kwamba awataki watanzania wengine wasitumii gesi,hayo ni matusi, wanamtwara wanachosema mitambo yote ya michakato ya gesi ijengwe mtwara alafu gesi ipelekwe kila mkoa ikiwa tayari,na mitambo ya umeme ijengwe mtwara alafu ipelekwe katika kila kijiji,hivi hilo hawa magamba inaitajika nini kuliewa hilo?,mbona mtoto wangu wa darasa la nne amewaelewa ao watu wa mtwara,hata wewe ulietoa hoja hii umeshindwa kuelewa hilo?
 
Back
Top Bottom