CHADEMA mnampuuza Mbowe!

kwa kuwa umejivika uenezi wa chadema utuwekee tamko la Mbowe ndo tutaichangia thread
 
Watake radhi wana harakati. Hata siku moja dhamira yao sio hiyo!
 

Ha ha ha aaaa! You made my day. Hivi jamaa kuna ubaya gani posho zao zikafika hata at least buku 10? Watu mchana kutwa wanajaza server hawaonei huruma?
 
Mkuu Nape Nnauye,
Naona umeshaanza Kuhaha kusaka ajira Mpya CHADEMA kwa kutaka kusafiria Nyota ya Mbowe.
Hii inatokana na Kasi ya Mwigulu katika kutekeleza Majukumu yako so Very soon Ndani ya CCM wewe utakuwa Jobless
 
Last edited by a moderator:
kuna UZI ulianzishwa humu kukuuliza "Nape mbona kimya sasa hivi?"
naona umeamua useme lolote kuvunja ukimya.
 
Kwa bahati mbaya Nape ni kipofu wa historia ya uhuru wa Tanzania na baya zaidi ni kipofu wa historia ya CCM ambayo ilitokana na TANU. Kwa hiyo Nape ni kipofu mara mbili na nasema hivyo kwa hoja.

TANU ilipozaliwa ilifanya siasa za barabarani yaani "activist politics". Kwa lugha ya kileo ndicho Nape anochokiita UANAHARAKATI. Je ni kwa nini TANU ilifanya siasa za UANAHARAKATI? Lengo la TANU lilikuwa kumkomboa mtanaganyika toka kwenye makucha ya utawala dhalimu wa kikoloni. Kwa ufafanuzi zaidi pitia hotuba za Mwl. Nyerere alipokuwa anazungumza na wakuu wa vyombo vya habari baada ya kujing'atua na kubakia mwenyekiti wa CCM. Sitaki kusema kuhusu udhalmu wa wakoloni-hayo unayajuwa!!

Je kwa nini CHADEMA wamekuwa wanafanya siasa za UANAHARAKATI? Hi ni kwa sababu baada ya kuondoka yule "mkoloni mweupe",baadaye akajitokeza "mkoloni mweusi" na katika mwishoni mwa miaka ya themanini na miaka ya tisini(wakati wa trade liberalization) au ubinafsishaji-upeanaji, "mkoloni mweusi" ama yeye mwenyewe na au kupitia wapambe wake alijipa fursa ya kumiliki kinyemela kile kilichokuwa mali ya umma.Katika maeneo mengine "mkoloni mweusi" alishirikiana na "mkoloni mweupe" aliyerudi kupitia mlango wa uwani kwa kujiita "mwekezaji(INVESTOR). Mbaya zaidi ni kuwa "mkoloni mweusi" kwa kujali maslahi binafsi na au kikundi kidogo cha wachache ameendelea kumpa ulaji "mkoloni mweupe" kwa kumpa mikataba isiyozingatia masalahi ya taifa kama ile ya madini na kufua umeme. Mkoloni Mweusi hapa ni viongozi wetu(viongozi wa serikalini, CCM, Makada wa CCM wanaojiita "local investors".Sasa udhalimu huu ndio ulizaa siasa za UANAHARAKATI za CHADEMA.Inawezeka CHADEMA wanazifanya siasa hizi kwa bahati mbaya kwa sababu ya msukumo wa hali halisi ya mazingira ya Tanzania ya sasa bila kujuwa historia hii au wanafanya wakiwa nayo kichwani.Kama wanafanya kwa sababu ya la kwanza au la pili na au yote mawili ni sawa kabisa.Haya ndio yanayowasukuma CHADEMA kufanya siasa hizo ambazo zilipaswa kufanywa na TANU(baadaye CCM). Kazi ya Ukombozi wa bara la Afrika ikiwamo Tanzania bado haijaikamilika. Tunahitaji ukombozi wa awamu ya pili wa Waafrika na kwa ajili ya uzi huu Tanzania. Na CCM kama mwasisi wa harakati za ukombozi wa bara la Afrika ndiyo ilipaswa kufanya UANAHARAKATI huu wanaoufanya CHADEMA. Swali ni je kwa nini CCM ghafla CCM baada ya kulamba sukari ya mabadiliko ya kiuchumi iliyoyaendesha yenyewe kwa hila iliachia nafasi hii ikaliwe na CHADEMA? Nani wa kumlaumu? CCM miliwapa CHADEMA shati kwa zawadi ya krismasi halafu mnawalaumu kwa kulivaa shati mlowapa? Naomba Nape uniambie povu nililotoa lina ujazo kiasi gani? Kama utashindwa kukadiria basi lazima utakuwa kipofu wa historia ya Tanzania na TANU
 
This is true, Nape ni mwenzetu humu, tupo naye kwa ID yake ya nape mnauye, ila pia yupo yupo!.
Mwenye ngozi ngumu ni hapa JF ni Pascal Mayalla wengine ngozi ya u-bwbw
Naomba kuthibitisha ana ngozi ngumu!.
P
 
R I P KAMANDA KOKOTE ULIPO MUNGU ATAKUSAMEHE YOTE YALE YA KIBINADAM ULANIWE SANA POMPEO NA GENGE LAKO KWA MAUWAJI MLIOYAFANYA KWENYE UTAWALA WENU
 
Mzee wa ngozi ngumu kumbe ulikuwaga member active?

Rudi bhana tulisongeshe gurudumu la data na vifurushi😂😅😂 usiogope tutakuheshimu kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…