Ndugu wadau, mimi nilikuwa mfuatiliaji sana wa Siasa za CHADEMA lakini ninachokiona sasa ni kama hawa ndugu zangu wameshindwa Siasa kabisa.
Mtawala amewazuia kufanya mikutano ya hadhara kinyume kabisa na Katiba ya Nchi, na wao wamekubali na hawajachukua hatua zozote zenye mashiko zaidi ya kusubiri kile kinachoitwa maridhiano.
Nilichojifunza ni kwamba, mtawala ameshajua udhaifu wa CHADEMA ulipo. Kwa hiyo anawaendesha atakavyo.
Tusishangae siku moja mtawala akiwazuia CHADEMA kuvaa sare za chama chao hadharani. Kwa hali kama hii, bila shaka watatii na kisha wataanza malalamiko na kelele nyingi kwamba wameonewa. Kitakachofuata, mtawala atawataka kuingia kwenye maridhiano eti ya kujadili kuvaa sare za chama chao. Bila aibu, watakubali kuingia kwenye maridhiano hayo.
Nawauliza ndugu zangu wa CHADEMA, ivi mtawala angewazuia kula Chakula mngekubali kirahisi namna hii?
Au mtawala angewaambia mtembee bila nguo kabisa mngekubali kirahisi namna hii?
Haya yote yanadhihirisha kwamba bado hampo serious na hamjakomaa kisawa sawa kushika dola.
Kama mnashindwa kupambana na adui wenu wa ndani, je, mkishika dola mtaweza kupambana na adui wa nje?
Si mtatishwa kidogo tu, kisha mnachuchumaa.
Kama mngekuwa serious kabisa, hamkutakiwa hata kidogo kukubali kutofanya mikutano ya hadhara.
Au hata sasa mlitakiwa kuwa mmeshaanza kufanya hiyo mikutano ya hadhara ili muone mtawala atachukua hatua gani dhidi yenu.
Kama hatua kali zingechukuliwa dhidi yenu kutokana na kufanya mikutano ya hadhara, mngeanza ku deal na hatua hizo ikiwa ni pamoja na kufanya maandamano ya Amani kupinga hatua hizo za mtawala.
Karibuni wadau.