Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,238
Ikifika mwaka 2015 itakuwa ni miaka 20 kamili imepita tangu kufanyika kwa uchaguzi wa kwanza ulioshirikisha vyama vingi mwaka 1995 tangu kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi uliokuwa umepigwa marufuku miaka 30 kabla, yaani mwaka 1965. Kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 inaonekana mchuano utakuwa kati ya CHADEMA na CCM.
Kwenye mazoezi na mechi za utangulizi (Chaguzi ndogo) CCM inaonekana kuzidiwa kwa kupunguziwa viti ilivyokuwa inavishikilia kuanzia ngazi ya vitongoji hadi kwenye ubunge na CHADEMA ikiongeza idadi ya viti vyake sehemu mbalimbali za nchi.
Lakini kwenye uchaguzi wa mwakani ni uchaguzi ambao hautatoa nafasi kwa chama chochote kile kutumia viongozi wa kitaifa au maarufu kufanya kampeni nchi nzima. Uchaguzi wa serikali za mitaa kampeni zake hufanyika kwa siku saba tu. Na chaguzi hizo kwa uzowefu hukabiliwa na dosari nyingi (irregularities) sana na rafu (Rigging) za kutisha. Na ili kukabiliana na dosari na Rafu hizo CHADEMA inatakiwa kuwa na mtandao mpana wa chama ulio Imara.
Toka leo hadi uchaguzi wa mwakani inahitaji juhudi za ziada kujenga mtandao Imara wa chama. Na ujenzi wa mtandao huo huitaji sana fedha ambazo naamini CHADEMA hawanazo. Ule mpango wa kuichangia CHADEMA kwa njia ya simu sijui umeishia wapi? Ilitakiwa kila mwezi angalau wananchi wengejulishwa ni kiasi gani kimekusanywa ili kujenga hamasa na kufanya wanachama wenyewe wajitathimini ni kwa kiasi gani wanachangia chama chao. Bila fedha (Halali lakini) hakuna siasa endelevu kwa vyovyote vile.
CHADEMA inahitaji zaidi ya watu lakini moja kuwa wagombea kwa upande wake kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na maelfu mengine kwa ajili ya mawakala. Nguvu kazi hiyo na wagombea hao ni lazima wawe wametayarishwa tangu mwaka huu na wala si mwakani wakati wa uchaguzi.
Kuna kazi ya msingi ya kufanya kabla ya uchaguzi wa mwakani kama ndiyo msingi wa ushindi kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015. CHADEMA Msituangushe.