WAZIWAZI
JF-Expert Member
- Mar 10, 2014
- 1,815
- 1,576
Wana janvi mimi sio mpenzi wa cdm ila naumia kuona nchi yetu inakosa kiungo muhimu cha demokrasia ambacho ni upinzani wenye nguvu kwa chama kinackokuwa madarakani, sasa CCM wamekunja nne, hakuna asiyejua kuwa hata uchaguzi wa 2015 watashinda na wengine watabaki kushabikia tu kama tulivyoona cdm wanamshabikia Sitta kuwa mwenyekiti wakiongozwa na kijana msomi mwenye vimelea vya kiburi kamanda antpass Tundu Lisu alafu sasa hivi wanahaha.
Wazee wetu kipindi wanaanzisha mfumo wa vyama vingi lengo kuu ilikuwa ni kuwa na vyama 2 ambavyo vingejipambanua kwa hoja na hatimaye wananchi wapime hoja na kukipa kimojawapo dola. sasa kuna sintofahamu ya mstakabali wa nchi yetu maana tuna utitiri wa vyama na ukichungulia kwa jicho la kizalendo viongozi wa vyama hivyo ni waganga njaa tu.
Kwa nini CHADEMA?
Ni chama ambacho kilianza vizuri na graph ikiwa ikipanda siku hadi siku na kujipambanua kwa umaridadi na nadhifu hasa 2007-2010 kabla kundi ovu kupewa nafasi za juu nakuwa wasemaji wa chama hiki, kundi hili lilianza kujipenyeza taratibu kuanzia 2008 na baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 likajimilikisha chama na kuanza kuweka makundi ndani ya chama kwa kuita wanachama wenzao wenye mitazamo tofauti na wao wasaliti. Waovu hao wakateka kikundi cha cdm propaganda mitandaoni na kukilisha maneno na wao wakawa watumwa wa waovu.Leo hii ukitoa ushauri wowote juu ya wapi cdm imeteleza unatukanwa eti bk7 at work. Matokeo yake kila mtu hapa anafahamu kinachowapata ingawa mitandaoni kikundi chao kinaendelea kufanya propaganda hasi ya kujifariji kusiko na tija eti mpaka kieleweke tuna Mungu. Nawaombeni sana maridhiano tunayoyaona mnafanya na CCM dodoma na Ikulu ndio njia sahihi ya kusonga mbele na nyinyi rudini mezani mfanye maridhiano ya pamoja juu ya tofauti zenu nazani mtapata jibu na ndo malezi mazuri hayo ndani ya demokrasia.
Chadema ndo chama ambacho toka vyama vingi vimeanza ndo chama ambacho kilikubalika na rika zote wasomi, wafanyakazi na wakulima ila sasa japo chadema mtandaoni wanajifariji, ukweli chama kinapoteza wapenzi kwa kasi kumbwa mno ila bado mna nafasi nzuri ya kujirekebisha na hatimaye imani ikarudi kwa jamii mkasaidia jamii kuichangamsha serikali katika mambo ya kimaendeleo na hata kushika dola kwa njia ya kidemokrasia siku za usoni.
Wenu rafiki wa kweli
WAZIWAZI:A S 103: