CHADEMA: Mbona Hili Mnalipuuzia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA: Mbona Hili Mnalipuuzia?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shinto, Aug 3, 2011.

 1. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wafuasi wengi wa Chadema kwa nje huwa wanajiweka karibu na falsafa za Mwalimu Nyerere. Ni mara nyingi tumekuwa tukiwasikia jinsi wanavyousifia utawala wake na falsafa zake ukilinganisha na marais waliomfuatia.

  Lakini kuna fundisho moja kuu la Mwalimu ambalo Chadema wanaamua kulipotezea kwa makusudi kwa sababu ya maslahi! Nalo ni swala la UBAGUZI. Mwalimu aliwakemea sana Wazanzibar pale walipokuwa wanabagua watanganyika chini ya kivuli cha Uzanzibar. mwalimu aliwakumbusha kuwa huo uzanzibar unapatikana ndani ya Muunganao tuu...nje ya muunganao kuna Mpemba na Muunguja. Ndani ya waunguja kuna divisions nyingine tele.

  Likewise, Chadema sasa wamekuwa vinara wa kuwabagua wazanzibar chini ya kivuli cha Utanganyika, Lakini ukweli ni kuwa ndani ya chadema hakuna huo utanagnyika unaosemwa! Kuna Zitto Camp vs Mbowe Camp, Kuna Chadema mama (Moshi , Arusha) na Chadema wa kudandia (Mwanza Shinyanga nk.). Hili hata kama likifunikwa kiasi gani litakuja kufumuka tuu.... Chacha Wangwe alifunua hili..likazimwa kiana yake, Sasa Shibuda naye yuko mbioni kuasua hili bubble!

  Chadema, dhambi ya ubaguzi haina mwisho............itaendelea kuwatafuna tu!
   
Loading...