CHADEMA Mbeya: Wanachama waliofukuzwa warudishiwa uanachama

CHADEMA Mbeya: Wanachama waliofukuzwa warudishiwa uanachama

Mwanah

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
353
Reaction score
101
Katika kuonesha CHADEMA ni chama makini wamemaliza tatizo lao kabisa .

CHADEMA Mbeya mjini ilikuwa na mgogoro mkubwa kati ya Baraza la vijana wilayani humo kiasi cha kupelekea wanachama wake na viongozi kadha kuvuliwa uanachama kabisa akiwemo m/kiti wa mkoa wa vijana wa chama hicho ndg Joseph Kasambala na wanachama wengine kama Patrick Ngajiro m/kiti wa BAVICHA Iwambi na Geofrey Sanga m/kiti wa BAVICHA huko Igawilo na wanachama wengine watatu ambao ni Sorwa Ngela na Mwambile(xb) na mwanachama mmoja kwa jina Mawalwiba ambaye pia alikuwa kampeni meneja wa mbunge Sugu wote walikuwa wamefukuzwa na sasa wamerudishwa rasmi jana chini ya usimazi na upatanisho ndg Kigaila.

Hivyo CHADEMA kwa sasa inaingie katika uchaguzi wa kata ya Iyera kwa nguvu noja hapo lazima ishinde uchaguzi huo.

Wale vigogo waliofukuzwa CHADEMA mkoa wa Mbeya wamerudishwa rasmi jana.Hatua hiyo ilifikiwa jana asubuhi nami ni mmoja wapo wa hao waliorudishwa pia yumo Joseph Kasambala wa BAVICHA.

Asanteni sana.
 
Katika kuonyesha CHADEMA ni chama makini wamemaliza tatizo lao kabisa .CHADEMA Mbeya mjini ilikuwa na mgogoro mkubwa kati ya Baraza la vijana wilayani humo kiasi cha kupelekea wanachama wake na viongozi kadha kuvuliwa uanachama kabisa akiwemo m/kiti wa mkoa wa vijana wa chama hicho ndg Joseph Kasambala na wanachama wengine kama Patrick Ngajiro m/kiti wa BAVICHA Iwambi na Geofrey Sanga m/kiti wa BAVICHA huko Igawilo na wanachama wengine watatu ambao ni Sorwa Ngela na Mwambile(xb) na mwanachama mmoja kwa jina Mawalwiba ambaye pia alikuwa kampeni meneja wa mbunge Sugu wote walikuwa wamefukuzwa na sasa wamerudishwa rasmi jana chini ya usimazi na upatanisho ndg Kigaila.

Hivyo CHADEMA kwa sasa inaingie katika uchaguzi wa kata ya Iyera kwa nguvu noja hapo lazima ishende uchaaaguuzi huo

ulikuwa na haraka haraka gani???? kwann usitulie uandike kitu cha kueleweka???? au kwa kuwa umeandika uzushi umeshindwa kutulia uutunge vizuri... swali lingine... mmewatumia weeeeee mlipopata mkawatupa sasa mnawahitaji mmewarudia tena...mkipata mnawatupa tena.
 
huyu naye amekubali kurudi??? anaenda kutumika tena bila kujijua, wakimaliza shida zao watamfukuza tena. lets watch and see
 
Hapo ndipo ninapoitofautisha Chadem na CCM,Chadema kiko makini kila kona!..........
 
Kutatua mgogoro ndani ya CHADEMA, tena Mbeya..................mmmmm,,,,,, siyo habari njema hata kidogo kwa vijana wa Lumumba.
 
Mtoa mada simuelewi elewi yeye akitoa mada anapotea hata akiulizwa swali huwa hajibu! Alikuja na mada jana kapotea mpaka leo!
 
hatimaye slaa atua uyole na kufanya mkutano nampongeza kwa hilo
 
Kumbukumbu zipo kumbuka ni mada 2 tofauti
 
yeye na sugu au na wenye bajaji maana nasikia sasahivi hawaiamini chadema ya sugu
 
Wale vigogo waliofukuzwa CHADEMA mkoa wa Mbeya wamerudishwa rasmi jana.Hatua hiyo ilifikiwa jana asubuhi nami ni mmoja wapo wa hao waliorudishwa pia yumo Joseph Kasambala wa BAVICHA.

Asanteni sana.
 
jaribu kutulia na uandike kitu kinachoeleweka
 
Ni vizuri kama wameelewa walipoteleza. Sio vizuri kufukuzana fukuzana pia ingawa inategemea kama ukiwa kuwadi out tu!!
 
Wale vigogo waliofukuzwa chadema mkoa mkoa wa mbeya wamerudishwa rasmi jana.hatua hiyo ilifikiwa jana asubuhi nami ni mmojawapo wa hao waliorudishwa pia yumo joseph kasambala wa bavicha asanteni sana

Wewe umerudi roho kwatu, au uko full equiped kuripiza visasi??
 
Mtulie mjenge Chama sasa, naamini mtasaidia kuibeba kata ya ihela.

pia muache kujiita vigogo japo mnamajukumu fulani ndani ya chama kujiita hivyo ni kukosa leadership skills. Hatutaki kutengeneza chama chenye matabaka makubwa.
 
Juliana Shonza na Mtela Mwampamba habari hii inawaumiza sana wanatamani wangekuwa wao waliorudishwa kundini ila wameishanyea kambi kurudi tena haiwezekani.
 
Back
Top Bottom