CHADEMA masuala mengine aibu tupu

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2022
Posts
308
Reaction score
425
Sawa tunatambua hamna ofisi ya maana inayoendana na hadhi ya chama chenu. Lakini tunajua pia mnapata hela kupitia michango ya wanachama.

Haipendezi hadi leo mnatumia Gmail kwenye mawasiliano yenu. Hiki chama kina watu, takribani miaka 30 sasa, bado mnafanya mambo ya ajabu kama haya.

Kuchukua dola kunategemea mambo mengi sana, sio kura tu za Watanzania. Kuna mambo huwa tunatazama kuona namna gani mko 'serious' ili tuwape dhamana kubwa zaidi.

Ila mkishindwa mambo madogo kama haya mtapata sana taabu huko mbeleni.
 
Kwa hiyo hicho ndio kipimo chako na dhamana wanatoa wananchi Kwa Chama Chao wanachokipenda Chadema.Pia ninachojua mawasiliano ni mawasiliano na mawasiliano ambayo mtu anayaamini atayatumia bila mashaka.
 
Ukweli mchungu.Hii ni critisism ya kujenga ili muonekane mpo serious.
 
Nakuunga mkono. Hili si sawa. Mimi naipenda Chadema lkn kwenye Hili lirekebishwe please Erythrocyte
Pongezi kwa kusema ukweli.Hata jina tu linaonyesha maturity.Penye ukweli usemwe bila kujali itikadi ya vyama.
 
Kwa hiyo hicho ndio kipimo chako na dhamana wanatoa wananchi Kwa Chama Chao wanachokipenda Chadema.Pia ninachojua mawasiliano ni mawasiliano na mawasiliano ambayo mtu anayaamini atayatumia bila mashaka.
Yaani kama hadi leo bado unawaza tu kwamba mawasiliano ni mawasiliano bado una safari ndefu sana, pole sana.
 
CHADEMA ni chama kikubwa ni vyema sana kuepuka fedha ndogondogo kama hizi..
 
Nashangaa sana Chadema wanavyoweza kuendesha chama vizuri bila hata kulipwa ruzuki! Kweli Mbowe ni mwamba.
 
Hiyo Gmail inapunguza nini juu mawasiliano? Makahaba wa twitter mna matatizo sana
 
Nashangaa sana Chadema wanavyoweza kuendesha chama vizuri bila hata kulipwa ruzuki! Kweli Mbowe ni mwamba.
Mwamba na Mwizi at the same time. Mtu anakopesha chama hadi chama hakina chakumfanya.
 
Issue hapa ya msingi ni nini: security au uzalendo?
 
Yaani kama hadi leo bado unawaza tu kwamba mawasiliano ni mawasiliano bado una safari ndefu sana, pole sana.
Tuambie tatizo unaliona wapi,na kwanini kwakuwa uhuru wa habari hapa kwetu ulikuwa jinai,Hivyo ni Bora kutumiwa mifumo huru ya ulimwengu huu kuliko kutegemea Ile ya nyumbani ambayo inaweza kufanyiwa uharamia na watu wa nyumbani Kwa kuwa ndio wa toa huduma🚶
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…