Chadema- mambo ya kufanya 2015


S

Somi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2009
Messages
871
Likes
348
Points
80
S

Somi

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2009
871 348 80
baada ya dk slaa kunyang'anywa uraisi kwa hujuma ya ccm ya kugeuza matokeo na viti vingi vya ubunge chadema kupokonywa isivyo halali inabidi chadema ijipange kuanzia leo kwa ajili ya uchaguzi wa 2015.
mambo ya muhimu:
.ijijenge kipesa iwe na ela za kutosha kukabiliana na ccm na mbinu zao chafu za kifisadi katika kuiba kura.
kwakuwa na ela nyingi itaweza kuwalipa mawakala waweze kulinda kura kikamilifu bila kudanganywa, na itaweza kuwalipa makatibu wake kila mahali nchi nzima waeneze sera zake kata kwa kata mtaa kwa mtaa kijiji kwa kijiji. ccm imejijenga sana tangu zamani toka ngazi ya kijiji na mjumbe wa nyumba kumi ndio maana kampeni ya chadema ya miezi 2 haitoshi kuwafikia wananchi wote ni hasara kwa chadema faida kwa ccm
kwakuwa asilimia kubwa ya wa Tz uelewa wao ni mdogo kisiasa na hawajui haki zao za mzingi inabidi wapewe elimu ya kutosha ili wafumbuke macho kutoka usingizini ingawa mwaka huu inatia moyo idadi kubwa ya watu wameweza kuamka na kujua haki zao kama wa tz
pesa zinaweza kupatikana kama ifuatavyo:
.kuwekeza ktk miradi mbalimbali kama majengo,kilimo n.k
.michango ya wanachama na watu mbalimbali
.viongozi wa chadema kwenda nje ya nchi kukutana na viongozi mbali mbali wa mataifa ya nje na mashirika ya kimataifa na kuwaomba misaada hata kwa kumuona obama ,cameron na wengine.

na matumaini makubwa wabunge wa chadema waliopatikana wataenda kunguruma bungeni ipasavyo kufichua maovu ya kifisadi na matatizo mengine kwenye serikali.
 

Forum statistics

Threads 1,236,570
Members 475,187
Posts 29,262,472