Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 54,406
- 43,740
Wanaukumbi.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho sasa hivi kipo chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr. Slaa, kinazidi kupoteza dira na mwelekeo wake wa asili, na hivyo kuharibu sifa za chama hicho kama kilivyosifiwa na Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake.
Badala ya kuwa chama cha siasa kinachotumia hoja na ustarabu kutafuta ushawishi kwa umma, Chadema ya sasa imegeuka kuwa chama cha kiharakati kisichoheshimu hata mamlaka ya nchi kwa mtindo huu Chadema hakiwezi kufika popote kama chama cha siasa, lazima Mbowe na Dr. Slaa waambiwe ukweli, kimsimamo wapo tofauti na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe, ambao ni miongoni mwa makada wachache wazalendo na watiifu.
Zitto, ambaye ana kundi kubwa la vijana pamoja na baadhi ya wazee amekuwa akitengwa kushiriki kwenye kazi za chama kama vile operesheni za vuguvugu za M4C, operesheni Sangara, toka kumalizika kwa uchaguzi mwaka 2010, Zitto amekuwa akitofautina na misimamo kadhaa ya chama chake, ambayo inaonekana siyo ya kisiasa ni ya kiharakati zaidi. kama suala la kumtabua rais Kikwete kama rais halali wa Tanzania, na mwaka 2010 Dr. Slaa, hata wabunge wenzake walipoweka azimio la kususia hotuba ya rais bungeni kutoka nje, Zitto aliamua kujitenga nao, viongozi wa Chadema nao wanazidi kumtenga Zitto, hata majuzi walipopata mwaliko Ikulu kutoka kwa rais Kikwete, kujadili masuala ya katiba walienda peke yao, suala la ukaguzi wa mahesabu ya vyama vya siasa ambalo linafuatliwa na Kamati ya Bunge ya Mahesabu ya serikali PAC, Chadema wanaona kama ni suala la Zitto.
Chadema sasa imeshindwa kuwajenga vijana kuwa na moyo wa uzalendo wa nchi yao, na badala yake imekuwa ikiwahamasisha kuvuruga misingi ya uzalendo na kutotii sharia na mamlaka zilizopo, pia wengi wa wabunge wa Chadema ni watiifu kwa Mbowe na Dr. Slaa, ni wale wanaodaiwa kuingia ndani ya chama kwa lengo la kusaka ubunge tu, na maslahi huku wakiwa hawana historia yoyote ya mchango wao wa kujenga chama.
Hali hii ndiyo imefanya Chadema sasa ionekane machoni mwa jamii ya watanzania kama chama cha vurugu na ubabe, hali inawafanya pia wananchi wasite kukiamini kwa kukikabidhi madaraka makubwa ya kuongoza dola.