CHADEMA, lengo la chama cha siasa si kushika dola, ni kushika mioyo ya wananchi walio wengi

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,904
Leo nimeamua niwape somo la siasa bure CHADEMA

Kuna dhana ya miaka ya zamani sana iliyokuwa ikisema lengo la chama chochote cha siasa ni kushika dola lakini wanasayansi wa siasa za kisasa wanapinga wazi kauli hizo kuwa chama cha siasa kama lengo lake ni kushika dola uwezekano wa kufanikiwa ni mdogo.

Wanasayansi wa siasa za kisasa wanabainisha kuwa lengo lolote la chama chochote cha siasa iwe ni kushika mioyo ya wananchi walio wengi ambao mbeleni ndio wawezao kukipa kura na kukiingiza madarakani kupitia sanduku la kura.

Vyama ambavyo lengo lake hulenga tu kushika dola huwa havishughuliki na wananchi walio wengi hujikita zaidi kushughulika na walio wachache.Na kwa sababu hiyo huwa havifanikiwi kushika dola.

Mfano Alkaeda,ISIS, vyama vilivyohusika na Arab springs na Alshabab ni makundi au vyama ambavyo lengo lake ni kukamata dola katika nchi mbalimbali.Lakini pamoja na kuwa na lengo hilo kwa kuwa hawakulenga kushika mioyo ya wananchi walio wengi kushika dola imekuwa haiwezekani na ni shida kwao kutokana na ukosefu wa kuungwa mkono na walio wengi ambao hawakuwalenga toka mwanzo.Ndio unaona nchi nyingi kama Libya,misri,algeria,uturuki,yemen nk kote vyama hivyo vilivyokuwa lengo lao ni kushika dola tu havipati mafanikio nchi hazitawaliki mambo hayaendi na wao hawashiki nchi kama akina Gadafi walivyokuwa wakiweza ambao walilenga kushika mioyo ya walio wengi.

CHADEMA inafanya kosa lile lile inasema lengo lake ni kushika dola lakini ukitizama mikakati yake unaona imejikita kabisa sio kuingia na kukubalika kwa walio wengi bali kukubalika na walio wachache

mifano
1.Bungeni walisusa bunge wakitaka maslahi yao wao wachache yasikilizwe.Walitaka bunge lionyeshwe live ili wao wachache waonekane.Wakati lengo la bunge na wanachoendea bungeni ni kuwakilisha hoja za walio wengi waliowatuma kwa mawaziri husika ili kero zitatuliwe.Kwa hivyo kwa kufanya hivyo kunawafanya wao kukosa kuingia na kuiteka mioyo ya watanzania walio wengi ambao mahitaji yao sio bunge LIVE wanahitaji huduma nzuri za afya,maji,elimu nk

2.Muda mwingi CHADEMA wanashindana na watu wachache (viongozi wa serikali,Bunge na mahakama) badala ya kujikita kwa wananchi walio wengi kuwasaidia kimaendeleo ili wawapende.Muda mwingi na nguvu nyingi zinatumika kushindana na raisi,polisi,viongozi wa serikali,viongozi wa bunge kama Tulia,Mahakamani kila siku kushindana na mahakimu na majaji.Muda mwingi wanahangaika na wachache!!!!!!!

3.Ukiangalia mkakati wao wa utetezi wa kutetea watu unaona wakifanya utetezi wanatetea zaidi walio wachache mfano wezi,wakwepa kodi na wanaotumbuliwa na Magufuli,Majambazi ambayo Raisi kaagiza yashughulikiwe papo kwa papo,Mabalozi wa nje ambao hawaruhusiwi kuzurura huko na huko bila kibali cha wizara ya mambo ya nchi za nje!Ukiangalia makundi wanayoyatetea ni ya wachache hayagusi walio wengi

4.Ukiangalia pia mkakakati wa maandamano,ubabe na vurugu pia una walakini.Jamii ya watanzania walio wengi hawapendi maandamano,siasa za ubabe wala vurugu.Ni watanzania wachache mno wenye kupenda hayo mambo.Hapa pia unaona wazi kuwa CHADEMA wanalenga zaidi kwa walio wachache kuliko walio wengi katika mikakati yao ya maandamano,ubabe wa kisiasa na vurugu.Hivi hata kwa akili za kawaida hawajawasoma watanzania walio wengi kuwajua wakoje?

Nikitizama CHADEMA kama mlipa kodi ambaye kodi zangu zinatumika kwa ruzuku naona CHADEMA wanatumia mkakati uliopitwa na wakati wa kuamini kuwa Lengo kuu la chama cha siasa ni kushika dola kwa namna yoyote iwe kwa maandamano,vurugu,migomo nk Hawako sahihi
 
Hivi ni sababu zipi zaweza kufanya tuichague chadema kuingia madarakani na si chama chengine?
 
Ukitaka kujua sababu waulizeni wanaowatuma kuja hapa jukwaani kuanzisha mada za kijinga kila siku dhidi ya CHADEMA na sio hivyo vyama vingine.
Sikutarajia hata hili nalo hamlijui. Sasa mnajua nini?
Ukweli ni kwamba mnaifanya CHADEMA izidi kusemwa kila siku. Uzuri zaidi nyie ndo mnaongoza kila siku kuiweka hewani CHADEMA mkiamini mnaiua, kumbe mnaifanya CCM iendelee kusahaulika!
Siku akili ikiwarudia mtakuwa mmechelewa. Kila uchaguzi CHADEMA inaongeza wapiga kura wanaoiunga mkono na pia Wabunge wanaongezeka. Sijui huwa wanaihonga tume ya uchaguzi?
 
Kama lengo la Chama cha siasa sio kushika dola, kwa nini mabosi wako wapo tayari kuua ili wabakie Madarakani?
Kama lengo ni kukubalika kwenye mioyo ya Wananchi kwa nini Chama tawala kilikataa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar na kuyafuta?
Ulitumia akili kutafakari kabla hujaleta huu upuuzi wako hapa jukwaani?
Ni aibu kubwa Vijana aina yako kuwa sehemu ya Watanzania.
 
Chadema wana kazikubwa ya kukijenga chama na kuongeza wanachama badala yakuendekeza mapambano na vombo vya serikali. Pia kwa majimbo waliyoychukua wathibitishie wananchi kwamba wana uwezo na walete mabadiliko badala kupoteza muda mwingi kuendekeza malumbano na vombo vya dola namaandamano yasiyo na tija. Bado chadema haina matawi ya kutosha nchini na hii ndio nguvu ya chama.
 
Chadema wana kazikubwa ya kukijenga chama na kuongeza wanachama badala yakuendekeza mapambano na vyombo vya serikali.

CHADEMA hawajitathimini kwa nini uchaguzi walishindwa na wananchi waliowapigia kura ni je ni kweli walikuwa na mapenzi ya dhati kwa CHADEMA au la.

Kwa tahmini yangu ni kuwa CHADEMA zile kura walizopata zilitokana zaidi na pesa walizotoa kuwarubuni viongozi wa makundi mbalimbali kama wa kidini,wa jamii na makundi mbali mbali nk ambao nao walitumika kama magari ya kusambaza pesa na propaganda ya CHADEMA kwa makundi yao na makundi madogo madogo na ya vijiwe mbali mbali kama vya wavuta bangi,kwenye mabaa,stendi za mabasi,vituo vya boda boda,vya wanywa viroba,vikundi vya akina mama,vijana,vijiwe vya waosha magari,machinga nk.

Baada yua kupokea mzigo wa pesa ndipo wakakipigia kura CHADEMA.CHADEMA haikupendwa sababu ni chama kilicho ndani ya mioyo ya watu bali kwa kuwa kilimwaga pesa.(HAPENDWI MTU NI POCHI TU.)

CHADEMA hakina wanachama wengi bali kina wafuasi wafuata pesa ambao kila siku kama hawazioni wanazidi kujiondoa CHADEMA kimya kimya.

Sasa hivi ndio kingejitahidi zaidi kujitathmini badala ya kuhangaika na vitu visivyo na tija.Ukweli ni kuwa CHADEMA kina wanachama pesa.
 
Ukitaka kujua sababu waulizeni wanaowatuma kuja hapa jukwaani kuanzisha mada za kijinga kila siku dhidi ya CHADEMA na sio hivyo vyama vingine.
Sikutarajia hata hili nalo hamlijui. Sasa mnajua nini?
Ukweli ni kwamba mnaifanya CHADEMA izidi kusemwa kila siku. Uzuri zaidi nyie ndo mnaongoza kila siku kuiweka hewani CHADEMA mkiamini mnaiua, kumbe mnaifanya CCM iendelee kusahaulika!
Siku akili ikiwarudia mtakuwa mmechelewa. Kila uchaguzi CHADEMA inaongeza wapiga kura wanaoiunga mkono na pia Wabunge wanaongezeka. Sijui huwa wanaihonga tume ya uchaguzi?
Si kila mtu ni mshabiki wa chama cha siasa.
 
CHADEMA hawajitathimini kwa nini uchaguzi walishindwa na wananchi waliowapigia kura ni je ni kweli walikuwa na mapenzi ya dhati kwa CHADEMA au la.

Kwa tahmini yangu ni kuwa CHADEMA zile kura walizopata zilitokana zaidi na pesa walizotoa kuwarubuni viongozi wa makundi mbalimbali kama wa kidini,wa jamii na makundi mbali mbali nk ambao nao walitumika kama magari ya kusambaza pesa na propaganda ya CHADEMA kwa makundi yao na makundi madogo madogo na ya vijiwe mbali mbali kama vya wavuta bangi,kwenye mabaa,stendi za mabasi,vituo vya boda boda,vya wanywa viroba,vikundi vya akina mama,vijana,vijiwe vya waosha magari,machinga nk.

Baada yua kupokea mzigo wa pesa ndipo wakakipigia kura CHADEMA.CHADEMA haikupendwa sababu ni chama kilicho ndani ya mioyo ya watu bali kwa kuwa kilimwaga pesa.(HAPENDWI MTU NI POCHI TU.)

CHADEMA hakina wanachama wengi bali kina wafuasi wafuata pesa ambao kila siku kama hawazioni wanazidi kujiondoa CHADEMA kimya kimya.

Sasa hivi ndio kingejitahidi zaidi kujitathmini badala ya kuhangaika na vitu visivyo na tija.Ukweli ni kuwa CHADEMA kina wanachama pesa.
Vipi waathirika wa tetemeko la aridhi mmewasaidiaje.Acha porojo kijana.
Hapa ulaji na upigaji tu kwa mwendokasi.
 
Back
Top Bottom