Stabilaiza
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 1,843
- 1,143
Utawala wa nchi hii umekuwa wa tofauti kabisa. Mtu analala na kuamka hajui kama atashinda na kuamka salama. Maisha ya wananchi yamekuwa ya wasiwasi na hasa wanasiasa wa ukweli, wa vyama vya upinzani.
Ni wakati wa Chadema kukaa macho muda wote ili kuwatetea wananchi wanaoonewa na utawala huu ambao unaongozwa kama Nyerere alivyowahi kutahadharisha. Kwamba huwezi kutenganisha maendeleo na demokrasia. Kwamba katika nchi zinazoendelea, na hasa za kutoka Afrika, utawala haufuati sheria, wanatawala kidikteta. Hawa madikteta wanapenda kuonea raia.
Ni wakati wa kila mmoja wetu, wakiwemo Chadema kupaza sauti kubwa kulaani na kupinga uonevu huu wa waziwazi unaofanywa na utawala wa Magufuli. Tunamfahamisha Magufuli kuwa nchi hii siyo mali yake. Kabla yake nchi ilikuwepo na itaendelea kuwepo bila yeye. Asitawale nchi kama anaendesha familia yake.
Rais lazima awajibike kwa wananchi na siyo kutumia vyombo vya dola kunyanyasa raia. Kuwajibika kwenyewe ni kuwa sisi wananchi hatutaki udikteta katika nchi yetu. Tunataka demokrasia ya kweli idumu. Nchi yetu imekuwa salama wakati wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete. Magufuli asituharibie. Kila mwananchi wa nchi hii anahaki ya kuishi kwa uhuru bila kuonewa na serikali ya Magufuli.
Ni wakati wa vyombo nyeti vya serikali kufanya kazi yake barabara na kumwonya kuacha maramoja kuwanyanyasa wananchi. Wamwambie waziwazi kuwa nchi hii ni kubwa kuliko yeye.
Chadema pazeni sauti kama chama kumtetea kila mwananchi anayeonewa. Kwa leo fanyeni press conference ya dharura kulaani na kupinga uonevu wa serikali ya Magufuli dhidi ya Mh. Tundu Lissu. Huyu ni mwananchi kama walivyo wananchi wengine.
Anastahili kupata haki kama raia wengine. Fanyeni press conference hii kabla jua halijakuchwa. [HASHTAG]#Free[/HASHTAG] Tundu Lissu now and unconditionally.