Chadema kuweka wakala kila kituo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema kuweka wakala kila kituo

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Lu-ma-ga, Oct 19, 2010.

 1. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Kufuatia taarifa za kukamatwa kwa karatasi za kupigia kura zilipigwa tayari huko Tunduma, sasa ni dhahiri kuwa vituo 52,000 vilivyotangazwa na NEC huenda kuna vituo ambavyo vinatarajiwa kupokea kura hizo haramu.
  Hili halina ubishi kwani ni lazima hizo kura zilizokwisha wekewa tick zipate vituo ili ziingie kwenye utaratibu wa kawaida.

  CHADEMA wanatakiwa kuhakikisha wanaanda mawakala 52,000 bila kujali gharama kwa kupoteza nafasi hii nyeti.ITAKUWA hasara kubwa sana kwa mstakari wa demokrasia Tanzania kama wataacha baadhi ya vituo kuweka wakala.

  Chadema waelewe kuwa watanzania sasa wameamua kufanya mabadiliko, na wajibu kwa watanzania ni kupiga kura na kulinda kura.Kwa upande mwingine chadema wanawajibu wa KUWEKA MAWAKALA 52,000 kusimamia zoezi hili nyeti.


  Kama itatokea chadema wasiweke wakala katika baadhi ya vituo ndani ya Tanzania wajue watakuwa hawajawatendea haki wapiga kura ambao kwa hiari ya wanaendelea kusikiliza sera za chadema na wamezikubali, na wako tayari kumpa kura nyingi DR.SLAA ili akabidhiwe ofisi kuu za magogoni hapo Nov mosi.

  Nimeongea na jamaa yangu huko Shinnyanga a.k.a shy town ameniambia kuwa watu wa shinyanga wanasema mwaka huu DR.SLAA ndiyo atajua nini maana shinyanga.Miaka yote CCM wamekuwa wakivuna kura nyingi ila wanasisitiza wanataka mawakala waaminifu.

  CHADEMA LAZIMA WAEPUKE HII LAWAMA YA KUTOWEKA WAKALA KWA BAADHI YA VITUO KWANI WATANZANIA HAWATAWAELEWA.

  CHAGUA CHADEMA CHAGUA MAENDELEO
   
 2. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 433
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ni vema watanzania wote waelewa tukajua uchaguzi wa mwaka huu ni kilele cha vita ya ukombozi wa mtanzania. kila Mtanzania, kila mchukia ufisadi na uhuni wa CCM hana budi kujipambanua katika mapambano haya. Maana yake ni hivi: Tukubali kusimamia kura zetu hata kama itakuwa kwa kujitolea bila malipo. Tunaijua sana jeuri ya CCM ya kuwalipa vema wasimamizi wao ambao pia ndiyo mawakala wa udanganyifu na wizi. Tufanye kama wenzetu, wale wazee waliokuwa wakimsaidia Nyerere walivyofanya kufunga kwa siku moja ili kulikomoa taifa letu dhidi ya unduli wa CCM. Sasa Chadema inao wakereketwa karibu kila kijiji na mtaa, tujitolee kujiandikisha tulinde kura zetu.
  Tunajua katika kipindi hiki kinachokamilika cha uongozi wa CCM, chama hicho kilikuwa kikipokea ruzuku nzito ambayo mara kadhaa imetumika vibaya kwa kufubaza demokrasia. walitumia ruzuku yao kunyamazisha walioonekana kukemea ufisadi wao, wapo walionunuliwa sawa na bidhaa sokoni tena wengine wasiotegemewa, wapo hata waliokodishiwa watu wa kuwadhuru kama wale waandishi na Mhariri waliomwagiwa tindikali na wapo waliokufa kwa namna tata. Shime wananchi tushikamane tuiokoe nchi kama ni malipo ni baada ya kudhibiti kura zetu zitakazokuwa nyingi safari hii, kura zitakazotupatia ruzuku kubwa kabisa itakayotuhakikishia malipo ya kifuta jasho kwa kazi hii kubwa na tukufu ya ukombozi.
  Vinginevyo CHADEMA ninayoifahamu haitamudu kuwaweka wasimamizi 52,000 hata kama kila mmoja atadai alipwe 5,000/= tofauti na mafidadi wenye uwezo wa kuwalipa wasimamizi wao kiasi chochote hata 20,000/= kila mmoja.
  MWISHO WA CCM UWE OKTOBA 31, CHAGUA CHADEMA KWA UKOMBOZI WA KWELI.
   
 3. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Najitolea kuwa msimamizi bure kama inawezekana. Nahisi nimechelewa lakini kama kuna uhaba basi Chadema tuwasiliane ili wanipe kituo. Niko dar kwa iyo mikoa ya dar na pwani najitolea bure. Ila mikoa ya mbali siwezi mana sitamudu gharama! Chadema nitafute kupitia email gsana6@gmail.com tuma ujumbe mimi ntawapigia kwa gharama zangu. Dr. Slaa anaweza.
   
 4. o

  omuhabhe Member

  #4
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naomba wale ambao tunaguswa na tatizo hilo tujitokeze mapema
  kufanya kazi hiyo bila malipo yoyote.na tule kiapo cha utii kwa
  uongozi wowote wa CHADEMA kabla ya siku hiyo.
  mimi ni mmojawapo wanipange natanguliza maslahi ya matakwa ya watanzania
  kwa machungu nilionao najitolea tu.
   
 5. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mimi mwenyewe najitolea kuwa wakala bila malipo jamni!! Mungu saidia CHADEMA
   
 6. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160

  Mkuu Lumaga,

  Mbona heading yako inakinzana na content?
   
 7. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  jamani tuendele kuchangia ili wasio na uwezo wa kusimamia bure waweze kulipwa na chama na kuondoa uwezekano wa kuwanunua.
  kama mtu ataamua kuusaliti umma kwa kumuamini akiwa amelipwa atalaaniwa na historia itamhukumu kwa hakika.
   
 8. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hapa cha muhimu si tu kuweka mawakala vituo vyote 52000,pia kuweka mawakala waaminifu katika vituo 52,000!!!!!!!!!!!!!!!
   
 9. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Haswaaa! na hawa wakujitolea mh?
   
 10. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Mimi niko dar, najitolea kuwa wakala wa chadema bure mapaka siku ya mwisho na nitatoa 50,000/ kwa ajili ya mawakala wengine 5 at the rate of @10000. Na wengine?
   
 11. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  tUNGEKUWA NA WATU WENGI KAMA WEWE TANZANIA INGEKUWA MBALI SANA, BIG UP GSANA
   
 12. M

  Mikomangwa Senior Member

  #12
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Natamani niwe wakala wa CHADEMA!

  Wana JF ambao ni wapenda haki na mabadiliko ambao hawanunuliki tujitokeze kusaidia Chama kwa kujitolea kukiwakilisha katika vituo vya kupigia kura. Nawaomba viongozi wa CHADEMA wabuni mbinu za kuwasiliana na kuwasaili wafuasi wao wenye sifa hiyo ili kuhakikisha kuwa vituo vyote vya kura vinamawakala waaminifu na wasioshawishika kwa 'short-lived' takrima. MIMI NIKO TAYARI KWA KAZI BILA MALIPO!!
   
 13. Capital

  Capital JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,036
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Tuendelee kuchangia kupitia MPESA na njia nyinginezo. Binafsi nimeshachangia mara mbili. Pia niko tayari kujitolea kuwa wakala, naishi \morogoro mjini. e-mail.kulumulumba@gmail.com

  Shime waTZ, saa ya ukombozi ni sasa, au la, tusahau!
   
Loading...