Chadema kuwasilisha hoja binafsi bungeni-vyuo vikuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema kuwasilisha hoja binafsi bungeni-vyuo vikuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpaka Kieleweke, Jan 23, 2009.

 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Date::1/22/2009
  Chadema kupinga udahili mpya kwa hoja binafsi
  Exuper Kachenje

  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kitawasilisha bungeni hoja binafsi inayolenga kuilazimisha serikali kuhakikisha hakuna mtoto atakayekosa fursa ya kusoma kwa sababu ya umasikini wa wazazi wake.


  Hatua hiyo ya Chadema imekuja huku wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakipinga mchakato wa kudahili wanafunzi upya baada ya vyuo vikuu kufunguliwa.


  Karibu theluthi mbili ya wanafunzi waliorejeshwa nyumbani baada ya chuo hicho kufungwa kutokana na mgomo wa kupinga sera ya uchangiaji, hawataweza kuendelea na masomo baada ya kutokamilisha masharti ya kurejea chuoni, ikiwa ni pamoja na kulipa sehemu yao ya kuchangia gharama za masomo.


  Katika taarifa yake iliyoitoa jana jijini Dar es Salaam, Chadema imesema kuwa imesikitishwa na utaratibu wa kudahili upya wanafunzi wa shahada ya kwanza unaoendelea UDSM na hivyo itawasilisha hoja hiyo binafsi kupitia kwa Waziri Kivuli wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambaye pia ni mbunge kwa chama hicho, Susan Lyimo.


  "Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesikitishwa sana na utaratibu wa kudahili upya wanafunzi wa shahada ya kwanza unaoendelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Mlimani," inasema sehemu ya taarifa hiyo ya Chadema.


  Imefafanua kuwa utaratibu huo ni batili kwa kuwa unakiuka mchakato mzima wa udahili ambao hufanywa na vitivo vinavyotakiwa kuhakiki fomu za mwombaji na kuangalia vigezo, vikiwemo ufaulu wa mwanafunzi katika matokeo ya kidato cha sita au sifa zinazofanana na hizo.


  Imeongeza kuwa mwanafunzi akishapata udahili, husajiliwa na si kwamba kinachofuata ni udahili mwingine kama inavyofanyika sasa na kwamba hatua hiyo ni kinyume cha utaratibu na kinalenga kuwaumiza wanafunzi, hasa watoto wa masikini.


  Katika hatua nyingine, Kamati ya Uongozi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano imesema miswaada mitatu mipya itasomwa katika Mkutano wa 14 wa Bunge linaloanza Januari 27 mwaka huu.


  Katika taarifa yake kamati hiyo imebainisha kuwa miswaada hiyo ni pamoja na Muswaada wa Sheria ya Pembejeo (Fertilizers Act,2008); Muswaada wa Sheria ya Kanuni za Vinasaba vya Binadamu (The Human DNA Regulation Act, 2008) na Supplementary Appropriation Act, 2009 na hatua zake zote.


  Kamati hiyo imetaja miswaada itakayosomwa kwa mara ya pili kuwa ni Muswada wa Sheria ya Afya ya Jamii, Muswada wa Sheria ya Wanyamapori ya Mwaka 2008.


  Mingine ni Muswaada wa Sheria ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, Sheria ya Viwango wa Mwaka 2008 na muswada wa kufanya marekebisho kwenye sheria mbalimbali wa mwaka 2008.


  Aidha katika mkutano huo wa Bunge maazimio matatu yatapitishwa ikiwemo Azimio la Kuridhia Itifaki ya Kuanzisha Tume ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika Mashariki; Azimio la Itifaki ya Jumuia ya afrika Masahariki kuhusu kuanzishwa kwa Chombo cha Kusimamia Usalama na Ulinzi wa Anga-2007.


  Kamati hiyo imebainisha kuwa Azimio la Kuridhia Itifaki kuhusu Maendeleo ya Jinsia ya Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC) pia utapitishwa katika mkutano huo wa 14 wa Bunge.


  Tuma maoni kwa Mhariri  Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi la leo.
   
 2. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2009
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  I support this kwani ndio njia ya kuweza kuupata ukweli wa jambo hili japo leo nimesikia ku8wa dada Rose Kiriginyi anjaweza kupewa fursa ya kuwasilisha hoja hii kwenye Bunge na lengo ni kuifanya iwe ya CCM.........
   
Loading...