CHADEMA: Kutoka 'kusemwa' hadi 'kusema'

CHADEMA: Kutoka 'kusemwa' hadi 'kusema'

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,143
Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kimeipigania mno hadhi yake ya sasa.Sasa ni chama kikuu cha upinzani Tanzania kikiunda pia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni chini ya Kamanda Freeman Aikaeli Mbowe(MB). Sasa CHADEMA kinajiimarisha zaidi kikijiandaa kuing'oa CCM madarakani kwa njia ya uchaguzi wa 2015.

Hapo mwanzo,kuanzia hasa 1992 hadi 2009, CHADEMA kilionekana kama chama cha udini,ukanda,fujo na mabaya mengineyo. Ikasemwa kuwa CHADEMA ni chama cha wachaga-au watu wa Kaskazini ya Tanzania hasa mikoa ya Kilimanjaro,Arusha na Manyara. Uchaguzi wa 2010 ukatoa taarifa rasmi isiyo na ubabaishaji. Taarifa ikaonesha kuwa CHADEMA ni chama cha umma wa watanzania. Badala ya Kanda ya Kaskazini kuwa na Wabunge wengi,ucahaguzi wa 2010 ukaumbua wengi. CHADEMA ikang'ara zaidi Kanda ya Ziwa.

Kimsingi, tuhuma zote dhidi ya CHADEMA zimekabiliwa ipasavyo. Ima kwa kuzitolea maelezo au kwa kuzipuuza kimatendo. Sasa CHADEMA ni msemaji wa waytanzania wengi wanyonge. Litokeapo lolote la kuathiri ustawi wa wananchi,CHADEMA husubiriwa kwa hamu kutoa kauli. Kiu ya watanzania huamia kwa CHADEMA ili kujua inasemaje juu ya tatizo au taarifa hiyo.

Kila mtanzania anaijua mifano kadhaa ambapo CHADEMA ilisubiriwa kutoa kauli na ikafanya hivyo ikikonga nyoyo za wangoja. Mifano ya hapa mwishoni ni sakata la gesi Mtwara na suala la kusitishwa kurushwa hewani moja kwa moja matangazo ya Bunge.

CHADEMA ipo makini katika kusema. Inasema katika aina mbalimbali:kimatendo na kimatamshi/matamko. Wapo Makamanda wa anga, wa nchi kavu na hata Mahakamani. Kila Idara imekamilika...EVERY CHANCE IS USED TO ITS UTMOST.

Kimsingi,watanzania wapo tayari kwa mabadiliko.Wanataka kubadili sera na utawala. Wanachukizwa na mazoea na utawala wa aina ile ile iliyoshindwa kutukwamua kwa miaka 51 tangu Uhuru. Sasa wapo tayari.Tayari kupiga kura za ushindi.

Kila la kheri CHADEMA!
 
Kila la heri shari hujitenga! Wanazidi kujipanga kuchukua uongozi zaidi wa kiutawala!
 
Chadema ni maji ya mafuriko!hayazuiliki kwa mbinu kama wanazotumia ccm ambazo nazifananisha na kingo za udongo kuzuia mafuriko!HEKO CHADEMA!
 
Yap ni kweli unayoyasema....
Chadema inanipa raha sana hasa pale inapokuwa inajibu shutuma dhidi yake kwa maneno yenye hekima halafu inazipuuza kwa matendo...safi sana CDM

Go CDM....
 
Back
Top Bottom