CHADEMA kutoka kukosoa hadi kuhujumu!

CHADEMA kutoka kukosoa hadi kuhujumu!

Ni wazi Chadema kama chama cha upinzani kina wajibu wa kuikosoa Serikali iliyopo madarakani ili wananchi waone kuwa hii sio serikali sahihi ili kwenye uchaguzi wananchi wakikatae chama tawala na kuchagua upinzani.

Hili sio kosa kabisa ni haki na ndio siasa yenyewe.

Chadema kupitia tundu lisu imebadili mbinu ya kukosoa serikali kutoka kwenye kuyasema maovu ya serikali na chama tawala hadi kufikia kufanya hujuma dhidi ya serikali kwa manufaa yao.Jambo hili sio baya yaani kuikwamisha serikali kutekeleza kile inachoamini ambacho chadema hawakiamini.

Kwa maoni yangu chadema inaruhusiwa kuikwamisha serikali ili isitekeleze sera za chama kinachoongoza na badala yake itekeleze yale ambayo chadema inayaamini lakini kwa manufaa ya nchi.

Chadema ya kipindi cha Dr Slaa ilikuwa inaikwamisha Serikali kwa kuibua maswala ya msingi ambayo yalikuwa ni ya kifisadi na hivyo yaliikwamisha serikali,yaliishurutisha serikali ,yalileta maendeleo na kuiongezea chadema uungwaji mkono.

Leo hii Chadema imeenda mbali sana kiasi cha kuweza kufanya mission za kuikwamisha serikali(bado sio tatizo)...lakini pia Chadema imeenda mbali kiasi cha kuihujumu serikali na nchi(hili ni tatizo).

Katika kusoma kwangu niliwahi kujifunza kuhusu faida na hasara za vyama vingi,ikiwa ni pamoja na uwezekano wa vyama vingi kuleta machafuko kwa kutumiwa na wabaya wa nchi.

Leo hii naweza kusema tunaanza kuuona ubaya wa vyama vingi ya kwamba vyama vingi vinaweza kutumiwa na maadui wa ndani au nje ya mipaka yetu kuleta machafuko na mkanganyiko usio wa lazima.

Chadema ya sasa baaada ya kuishiwa hoja imeamua kuhujumu nchi(sabotage) badala ya kuikwamisha serikali(compromise)

Tunaweza kushabikia uhujumu kama wazembe wasiojua tunataka tufike wapi kama nchi lakini kamwe hatuwezi kushabikia uhujumu kama tunajitambua tunataka nini kama nchi!

Swahiba wangu Tundu lissu ambaye nilimuona kama kijana mwenye character ya kikorofi ambayo ilihitajiwa katika uongozi wa zama hizi yuko vizuri ingawa amekosa muongozo.

Pia naamini lissu alikosea 2015 kwa kukubali kuwa upande wa fisadi aliyeingia chadema ,hili ndilo linalomuumiza TL na anashindwa jinsi ya kulirekebisha(alikosa muongozo)

Katika harakati za kuikwamua Chadema na haiba yake Lissu anajaribu kutumia weledi wake kwa nguvu zote kujiweka juu na hapo hapo kutaka kuisafisha Chadema jambo ambalo ni gumu na linalomfikisha hatua potofu.

Mwenendo wa chadema wa sasa ni ule wa kupambana kufa na kupona ili isife tofauti na miaka mitano au kumi iliyopita.

Mwenendo huu umewapa ukichaa flani chadema na kupoteza muelekeo,hapo ndipo ninaporejea kwenye mada kuu kwamba chadema inahama kutoka kwenye kukosoa tu na badala yake inaenda kwenye hujuma kwa nchi kitu ambacho sio sahihi kwa maslahi ya nchi.

Mimi siamini kabisa kwamba Chadema imekosa hoja nzito za kuisumbua serikali bila kufanya uhujumu.

Bado kama nchi tuna hoja almost zilezile despite ujio wa Magufuli ambaye amezipunguza kwa kasi ya ajabu.Kupitia hoja zile zile za zamani Chadema au lissu inaweza kukomaa na kuikwamisha(compromise) serikali bila kuihujumu na hivyo uwepo wa upinzani na Kina lisu ukaonekana kama ni neema kwa maendeleo ya watanzania na sio kikwazo.

Nikitolea mfano mpaka sasa sijaona universal covarage ya bima ya afya.

Mpaka sasa sijaona fisadi aliyehukumiwa kwenye mahakama ya ufisadi.

Mpaka sasa hatujasikia kuhusu milioni 50 kwa kila kijiji.

Mpaka sasa hatujaona GENERAL TYRE IKIFANYA KAZI...

Mifano ni mingi na tukiamua kujikita kwenye mifano hiyo tutakuwa tumeikosoa na kuikwamisha serikali vilivyo na hakutakuwa na haja ya kupiga simu canada ili tihujumu nchi na uchumi wake.

Bado chadema kama chama hakijaichachafya serikali ya ccm katika ahadi zake nyeti ambazo isipotekeleza itaondolewa na wananchi.

Chadema inapambana na mambo ambayo iliwahi kuyafanyia kazi na sasa yanafanyiwa kazi na CCM huku wao wakijaribu kuyapinga.

Wito wangu kwa chadema ni lazima warudi kwenye meza na kumkataa fisadi na baada ya hapo watuombe wadau tuwashauri nini cha kufanya wakiwa wasafi...Tutawafundisha ni jinsi gani ya kuikosoa Serikali bila kuhujumu maslahi ya Taifa.
Ndugu yangu CHADEMA safi isingempokea Sumaye wala Lowassa. Hii ni ya wababaishaji tu. Chama kilishapoteza mwelekeo tangu 2015 Agosti.
 
Ndugu yangu CHADEMA safi isingempokea Sumaye wala Lowassa. Hii ni ya wababaishaji tu. Chama kilishapoteza mwelekeo tangu 2015 Agosti.
Yaani Chama kinatoa matamko 10 hadi 20 kwa mwezi halafu yanakosa impact....hayaitikisi serikali.

Matamko yamekaa kidakudaku tu.

Yapo mambo mengi ambayo hajafanyiwa kazi na Serikali japo yaliahidiwa hatuoni chadema wakiyaongelea.
 
Hukuwepo wala hujui ni jinsi gani tumeifanyia kazi chadema bila kulipwa!

Kumbe ulikuwa ni chadema maslahi. Huwezi kula embe dodo kabla ya kuwiva uujue utam wake. Ngojea liive lidondoke chini ndo utam wa dodo. Ungelingoja chadema wachukue dola ndo uone ka uliifanyia kazi udai malipo.
 
Hiki kichaka cha uzalendo kinachotumiwa na wapiga makofi wa awamu hii ya tano kimeungua.Jibu ni hoja sio kuleta ujanja ujanja kwenye vitu vya msingi.Mbona hamsemi wamehujumu nini? Shida ni kiujiona nyiye niwatakatifu sana sasa nilazima yaelezwe madhambi(mapungufu) yenu ili watu wawajue.
 
Mkakati wa ccm uko wazi, ni kujaribu kufuta upinzani in a hard way, tofauti na ilivyokuwa huko Nyuma, sasa wao wafanyeje? Ni harali kama watatumia njia halali kukwamisha ccm. Ushauri serikali iache utawala wa chuki na kuwaonea wapinzani. Wote wafanyekazi kwa manufaa ya watz. Ccm wakifanya vibaya waondoke, wajipange upya. Ni makosa kutaka wabaki madarakani kwa kuhujumu upinzani. Hii ndiyo inaleta visa vya kuviziana
 
Back
Top Bottom