CHADEMA kutoka kukosoa hadi kuhujumu!

CHADEMA kutoka kukosoa hadi kuhujumu!

Sidhani kama hili ndilo,lililokuwa moyoni mwako. Ila kama unataka kutafuta njia ya kukivuruga chama kwa kutukanana ndani kwa ndani tafuta njia nyingine.
Huyo fisadi Lisu aliyemkubali ni nani?? Kama ni fisadi, iweje serekali iliyounda mahakama ya kuwafunga imemshindwa?? Haki sawa haitolewi kwa maneno ya mtaani, hutolewa kwa maneno (Hoja) za kisheria pamoja na ushahidi usiopingika.
Mangapi yaliyosemwa wakati ule leo tunayaona sio kitu? Chadema haitakaa imsitiri fisadi.
Ati "watuombe wadau tuwashauri nini cha kufanya) wadau wewe na nani?? Tulia tu ndugu kaa la mkaa wa mawe halizimwi kwa pumba ya mpunga mkavu.
Hukuwepo wala hujui ni jinsi gani tumeifanyia kazi chadema bila kulipwa!
 
VITA YA UCHUMI BAINA YA TANZANIA NA CANADA IMEKOLEA, UKITAKA KUSHINDA VITA PIGANA VITA!!

Mtu mmoja mwenye akili aliwahi kusema kuwa, "Ukitaka kushinda Vita, shika Bunduki pigana Vita". Kwamba huwezi kuishinda Vita ukiwa kitandani umelala fofofo!! Huwezi, huwezi kamwe!!

Vita ya Kiuchumi baina ya Tanzania na Canada sasa imekolea. Ni wazi kuwa sasa Canada na Tanzania zipo ktk mtifuano mkubwa wa Kiuchumi na bahati mbaya sana siku za usoni tunaweza kuingia ktk mgogoro wa Kidiplomasia ikiwa hazikutumika akili sawasawa kote Tanzania na Canada. Lkn hii ni Vita, ikiwa tunataka kuishinda ni lazima tushike Bunduki tupigane Vita!!

Nimepata nafasi ya kuwasikiliza Watu wachache muhimu ktk Nchi hii wakizungumzia swala la Ndege yetu kushikiliwa huko Canada. Wote wanaosema jambo hili hawalisemi sawasawa, ama hawajui ama wanakosea kwa bahati mbaya (Thinking capacity kukwama) au wanakosea kwa maksudi kwa sababu za Kidiplomasia! Sababu hii ya Kidiplomasia inaweza kuwa na maana kuliko zingine zote.

Watu hawa wote wanasema kuwa Ndege yetu Bombadier Q400 imeshikiliwa Canada kwa sababu ya Deni la US Dollah 38.7 ambalo Serikali inadaiwa na Kampuni ya Stelling Civil Eng. LTD ya huko Canada lililotokana na Kampuni hiyo kunyang'anywa Kandarasi na kutimuliwa Nchini. Hizi ni fikra mbovu zaidi kuwahi kutokea ktk Vichwa vya watu wakubwa, ni aibu, ni fedheha mtu kama Zitto Kabwe kuwaza namna hii.

Hebu tufikiri pamoja:-

●Hukumu ya kushikilia Mali zote za Serikali ya Tanzania ktk Nchi hususani ya Canada ilitolewa Dec-2009/June 2010. NB, hakuna Mali yoyote kwa kipindi chote hiko iliowahi kushikiliwa kwa amri hiyo ya Mahakama hadi juzi.

●Mwaka 2016 mwanzoni Tanzania imefanya order ya kutengenezewa Ndege na Kampuni ya Bombadier Q400 ya Nchini Canada na September Ndege mbili zikakamilika na kurejea Nchini. Kumbuka amri ya Mahakama ilikwisha tolewa tayari iko kazini lkn Ndege hizo hazikushikiliwa.

●March 2017 Serikali ya Tanzania ikazuia Makontena 262 ya Mchanga wa dhahabu almaarufu Makinikia yanayomilikiwa na Kampuni ya Accacia (Barrick) ya Nchini Canada.

●May na June 2017, Serikali ya Tanzania ikatafakari kupitia riport za Uchunguzi wa shughuli za Madini Nchini juu ya uhalali wa uwekezaji, ulipaji Kodi na Mirahabaya Madini inayofanywa na Kampuni za Barrick na kuona dosari za kisheria na hujuma mbalimbali za Kiuchumi. July zikapitishwa Sheria kudhibiti Biashara ya madini.

● July 2017, Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ikaifikishia Accacia-Barrick ya Canada notice ya kuidai Tsh. Trion 425 kutokana na malimbikizo ya Kodi.

●July Serikali ya Canada kupitia Kampuni ya Stelling Civil Eng. Ltd ikaishikilia Ndege ya Serikali ya Tanzania kutokana na amri ya Mahakama iliyotolewa Dec 2009/ June 2010.

MY TAKE:
Ni mjinga pekee ndie anaweza kukubaliana kuwa Ndege yetu imeshikiliwa Canada kutokana na Deni ambalo Serikali inadaiwa na Stelling Eng. Civil Ltd. Wakati Serikali ya Canada inashirikiana na Kampuni zake kutetea maslahi ya Nchi yao, Wananchi wa Tanzania wanapingana na Serikali yao kutetea maslahi ya Nchi yao. Ulazwe Pema Peponi Mwl. Nyerere, tumebaki tunasoma ktk Vitabu kuwa watu waliopinga Serikali ktk mambo ya kitaifa wakati wako walibakishiwa option mbili tu kuchagua ama kuishi uhamishoni ama Moyo kuuacha mwili. Sasa watu wa namna ya Tundu Lissu wachague moja kati ya haya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninachojua mimi chadema ndio inayohujumiwa, viongozi wake wanakamatwa hovyo, kufilisiwa na wengine wametoweka hatamifupa yao haijaonekana
 
Mengitis (maambukizi ya vimelea vya magonjwa katika viwambo vinavyozunguka uti wa mgongo na ubongo), pamoja na maelezo yote, sijaona maelezo ya namna CHADEMA wanavyohujumu.

Pili ni vizuri kujua si lazima CHADEMA kulizungumzia jambo unalolijua wewe au sawia na ufahamu wako, bali vile wanavyoona wao inafaa kwa maslahi mapana ya Taifa.
Tatu tueleze kwa kina jambo gani CHADEMA walilosema la uongo ukitupatia ukweli ili tuujue uongo wao.
Yaani umeandika pafupi, lakini pana madini, jamaa kaandika parefu lakini pumba tupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukizini na mke wa mtu ukikamatwa ugoni usilalamike kua niliyekutana nae njian ni juli bali elewa hata usio wafahamu wanaelewa mme wake, kwani aliekua anamdai wana mahusiano gani. Unayosema wayaseme wameambiwa siasa hadi mwaka 2020 watayasemea wapi? Umbukeni kevyeni msitafute wachawi mnajiroga wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanajifinya na kulia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nawakaribisha wadau wote wenye uzalendo
Serikali awamu hii imejikita kufukia mabaya yake yasionekane!Ndio maana suala la Ndege kukamatwa walitaka walifanye siri!!!
Tatizo naloona hapa ni kuwa wamechukia siri kutolewa na Lissu,na ndio maana wamekuja na matamko yasiyoeleweka!Hivi kama walijua kuna watu wanawahujumu,walikuwa wapi kusema?Mbona hayo yameibuka baada ya press ya Lissu?Ni dhahiri mnatumika kujaribu kupunguza impact ya press ya Lissu!Hilo pekee ndilo liko clear!
Tuna sheria,zipo wazi kuhusu wahujumu uchumi!Ndio maana Yona na Mramba waliingia jela!Nendeni mkamshitaki kwa kuhujumu uchumi,Msukuma atasaidia kwenye kutoa ushahidi!Hizi porojo mnazotoa humu ni useless!
 
  • Thanks
Reactions: 999
Ni wazi Chadema kama chama cha upinzani kina wajibu wa kuikosoa Serikali iliyopo madarakani ili wananchi waone kuwa hii sio serikali sahihi ili kwenye uchaguzi wananchi wakikatae chama tawala na kuchagua upinzani.

Hili sio kosa kabisa ni haki na ndio siasa yenyewe.

Chadema kupitia tundu lisu imebadili mbinu ya kukosoa serikali kutoka kwenye kuyasema maovu ya serikali na chama tawala hadi kufikia kufanya hujuma dhidi ya serikali kwa manufaa yao.Jambo hili sio baya yaani kuikwamisha serikali kutekeleza kile inachoamini ambacho chadema hawakiamini.

Kwa maoni yangu chadema inaruhusiwa kuikwamisha serikali ili isitekeleze sera za chama kinachoongoza na badala yake itekeleze yale ambayo chadema inayaamini lakini kwa manufaa ya nchi.

Chadema ya kipindi cha Dr Slaa ilikuwa inaikwamisha Serikali kwa kuibua maswala ya msingi ambayo yalikuwa ni ya kifisadi na hivyo yaliikwamisha serikali,yaliishurutisha serikali ,yalileta maendeleo na kuiongezea chadema uungwaji mkono.

Leo hii Chadema imeenda mbali sana kiasi cha kuweza kufanya mission za kuikwamisha serikali(bado sio tatizo)...lakini pia Chadema imeenda mbali kiasi cha kuihujumu serikali na nchi(hili ni tatizo).

Katika kusoma kwangu niliwahi kujifunza kuhusu faida na hasara za vyama vingi,ikiwa ni pamoja na uwezekano wa vyama vingi kuleta machafuko kwa kutumiwa na wabaya wa nchi.

Leo hii naweza kusema tunaanza kuuona ubaya wa vyama vingi ya kwamba vyama vingi vinaweza kutumiwa na maadui wa ndani au nje ya mipaka yetu kuleta machafuko na mkanganyiko usio wa lazima.

Chadema ya sasa baaada ya kuishiwa hoja imeamua kuhujumu nchi(sabotage) badala ya kuikwamisha serikali(compromise)

Tunaweza kushabikia uhujumu kama wazembe wasiojua tunataka tufike wapi kama nchi lakini kamwe hatuwezi kushabikia uhujumu kama tunajitambua tunataka nini kama nchi!

Swahiba wangu Tundu lissu ambaye nilimuona kama kijana mwenye character ya kikorofi ambayo ilihitajiwa katika uongozi wa zama hizi yuko vizuri ingawa amekosa muongozo.

Pia naamini lissu alikosea 2015 kwa kukubali kuwa upande wa fisadi aliyeingia chadema ,hili ndilo linalomuumiza TL na anashindwa jinsi ya kulirekebisha(alikosa muongozo)

Katika harakati za kuikwamua Chadema na haiba yake Lissu anajaribu kutumia weledi wake kwa nguvu zote kujiweka juu na hapo hapo kutaka kuisafisha Chadema jambo ambalo ni gumu na linalomfikisha hatua potofu.

Mwenendo wa chadema wa sasa ni ule wa kupambana kufa na kupona ili isife tofauti na miaka mitano au kumi iliyopita.

Mwenendo huu umewapa ukichaa flani chadema na kupoteza muelekeo,hapo ndipo ninaporejea kwenye mada kuu kwamba chadema inahama kutoka kwenye kukosoa tu na badala yake inaenda kwenye hujuma kwa nchi kitu ambacho sio sahihi kwa maslahi ya nchi.

Mimi siamini kabisa kwamba Chadema imekosa hoja nzito za kuisumbua serikali bila kufanya uhujumu.

Bado kama nchi tuna hoja almost zilezile despite ujio wa Magufuli ambaye amezipunguza kwa kasi ya ajabu.Kupitia hoja zile zile za zamani Chadema au lissu inaweza kukomaa na kuikwamisha(compromise) serikali bila kuihujumu na hivyo uwepo wa upinzani na Kina lisu ukaonekana kama ni neema kwa maendeleo ya watanzania na sio kikwazo.

Nikitolea mfano mpaka sasa sijaona universal covarage ya bima ya afya.

Mpaka sasa sijaona fisadi aliyehukumiwa kwenye mahakama ya ufisadi.

Mpaka sasa hatujasikia kuhusu milioni 50 kwa kila kijiji.

Mpaka sasa hatujaona GENERAL TYRE IKIFANYA KAZI...

Mifano ni mingi na tukiamua kujikita kwenye mifano hiyo tutakuwa tumeikosoa na kuikwamisha serikali vilivyo na hakutakuwa na haja ya kupiga simu canada ili tihujumu nchi na uchumi wake.

Bado chadema kama chama hakijaichachafya serikali ya ccm katika ahadi zake nyeti ambazo isipotekeleza itaondolewa na wananchi.

Chadema inapambana na mambo ambayo iliwahi kuyafanyia kazi na sasa yanafanyiwa kazi na CCM huku wao wakijaribu kuyapinga.

Wito wangu kwa chadema ni lazima warudi kwenye meza na kumkataa fisadi na baada ya hapo watuombe wadau tuwashauri nini cha kufanya wakiwa wasafi...Tutawafundisha ni jinsi gani ya kuikosoa Serikali bila kuhujumu maslahi ya Taifa.
Mbona umeandika andika vitu kama vya hewani vizivyo na mashiko. Ainisha hapa ni jinsi gani CHADEMA au lisu wamehujumu nchi. Inaonekana hata maana ya kuhujumu nchi hujui
 
Aliyesaini huo mkataba kumbe alikuwa Lissu
 
Hivi sasa kuijadili chadema na huyo vuvuzela ni kupoteza muda kidole kwenye triger anytime from now anything can happen tutaokota mzoga!
Kwani wewe hutakua mzoga mkuu? Hata wewe ni mzoga unaosubiria muda wake, hiyo tofauti ni kumtanguliza mwenzako na wewe njia ile ile.
 
VITA YA UCHUMI BAINA YA TANZANIA NA CANADA IMEKOLEA, UKITAKA KUSHINDA VITA PIGANA VITA!!

Mtu mmoja mwenye akili aliwahi kusema kuwa, "Ukitaka kushinda Vita, shika Bunduki pigana Vita". Kwamba huwezi kuishinda Vita ukiwa kitandani umelala fofofo!! Huwezi, huwezi kamwe!!

Vita ya Kiuchumi baina ya Tanzania na Canada sasa imekolea. Ni wazi kuwa sasa Canada na Tanzania zipo ktk mtifuano mkubwa wa Kiuchumi na bahati mbaya sana siku za usoni tunaweza kuingia ktk mgogoro wa Kidiplomasia ikiwa hazikutumika akili sawasawa kote Tanzania na Canada. Lkn hii ni Vita, ikiwa tunataka kuishinda ni lazima tushike Bunduki tupigane Vita!!

Nimepata nafasi ya kuwasikiliza Watu wachache muhimu ktk Nchi hii wakizungumzia swala la Ndege yetu kushikiliwa huko Canada. Wote wanaosema jambo hili hawalisemi sawasawa, ama hawajui ama wanakosea kwa bahati mbaya (Thinking capacity kukwama) au wanakosea kwa maksudi kwa sababu za Kidiplomasia! Sababu hii ya Kidiplomasia inaweza kuwa na maana kuliko zingine zote.

Watu hawa wote wanasema kuwa Ndege yetu Bombadier Q400 imeshikiliwa Canada kwa sababu ya Deni la US Dollah 38.7 ambalo Serikali inadaiwa na Kampuni ya Stelling Civil Eng. LTD ya huko Canada lililotokana na Kampuni hiyo kunyang'anywa Kandarasi na kutimuliwa Nchini. Hizi ni fikra mbovu zaidi kuwahi kutokea ktk Vichwa vya watu wakubwa, ni aibu, ni fedheha mtu kama Zitto Kabwe kuwaza namna hii.

Hebu tufikiri pamoja:-

●Hukumu ya kushikilia Mali zote za Serikali ya Tanzania ktk Nchi hususani ya Canada ilitolewa Dec-2009/June 2010. NB, hakuna Mali yoyote kwa kipindi chote hiko iliowahi kushikiliwa kwa amri hiyo ya Mahakama hadi juzi.

●Mwaka 2016 mwanzoni Tanzania imefanya order ya kutengenezewa Ndege na Kampuni ya Bombadier Q400 ya Nchini Canada na September Ndege mbili zikakamilika na kurejea Nchini. Kumbuka amri ya Mahakama ilikwisha tolewa tayari iko kazini lkn Ndege hizo hazikushikiliwa.

●March 2017 Serikali ya Tanzania ikazuia Makontena 262 ya Mchanga wa dhahabu almaarufu Makinikia yanayomilikiwa na Kampuni ya Accacia (Barrick) ya Nchini Canada.

●May na June 2017, Serikali ya Tanzania ikatafakari kupitia riport za Uchunguzi wa shughuli za Madini Nchini juu ya uhalali wa uwekezaji, ulipaji Kodi na Mirahabaya Madini inayofanywa na Kampuni za Barrick na kuona dosari za kisheria na hujuma mbalimbali za Kiuchumi. July zikapitishwa Sheria kudhibiti Biashara ya madini.

● July 2017, Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ikaifikishia Accacia-Barrick ya Canada notice ya kuidai Tsh. Trion 425 kutokana na malimbikizo ya Kodi.

●July Serikali ya Canada kupitia Kampuni ya Stelling Civil Eng. Ltd ikaishikilia Ndege ya Serikali ya Tanzania kutokana na amri ya Mahakama iliyotolewa Dec 2009/ June 2010.

MY TAKE:
Ni mjinga pekee ndie anaweza kukubaliana kuwa Ndege yetu imeshikiliwa Canada kutokana na Deni ambalo Serikali inadaiwa na Stelling Eng. Civil Ltd. Wakati Serikali ya Canada inashirikiana na Kampuni zake kutetea maslahi ya Nchi yao, Wananchi wa Tanzania wanapingana na Serikali yao kutetea maslahi ya Nchi yao. Ulazwe Pema Peponi Mwl. Nyerere, tumebaki tunasoma ktk Vitabu kuwa watu waliopinga Serikali ktk mambo ya kitaifa wakati wako walibakishiwa option mbili tu kuchagua ama kuishi uhamishoni ama Moyo kuuacha mwili. Sasa watu wa namna ya Tundu Lissu wachague moja kati ya haya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungelipa ingekusaidia kidogo.
 
Mbona umeandika andika vitu kama vya hewani vizivyo na mashiko. Ainisha hapa ni jinsi gani CHADEMA au lisu wamehujumu nchi. Inaonekana hata maana ya kuhujumu nchi hujui
Kaa chini utulie na kuisoma na kuichambua mada vizuri utaelewa !
The forum is for Thinkers not Readers
 
Back
Top Bottom