CHADEMA kutikisa tena Kimara, Mtaa wa Mavurunza

amba.nkya

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
446
131
[h=2] Heshima mbele wanajamvi...

Tafadhari rejea Thread ya jana “Mlipuko wa CHADEMA watokea Mtaa wa Mavurunza, Kimara” ambao ulikuwa ni Mkutano wa maandalizi ya ujio wa Katibu Mkuu wa chama – Taifa, Mh. Dr. Wilibroad Slaa pamoja na viongozi wengine wa kitaifa kwenye Mkutano wa Kata siku ya Jumamosi ya 25 Februari 2012.
[/h] Taarifa kamili ni kwamba kutakuwa na Mkutano wa hadhara CHADEMA Kata ya Kimara, utakaofanyika kwenye eneo la wazi lililopo nyuma ya BS Grocery, Barabara ya Bonyokwa, siku ya Jumamosi ya tarehe 25 Februari 2012 kuanzia saa nane mchana. Barabara ya Bonyokwa inaungana na Barabara ya Morogoro kuanzia Kimara Mwisho kuelekea Segerea na Kinyerezi.
Kwa watakaotumia usafiri wa gari/daladala wanashauriwa washuke kwenye kituo cha kwa Mashaka na waulize BS Grocery ilipo.
Mgeni rasmi kwenye mkutano huo atakuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, Mh.Heche akimwakilisha Mh.Dr.Wilibroad Slaa ambaye amepata dharura. Vile vile, viongozi wengine wa kitaifa kupitia CHADEMA wanaotarajiwa kuambatana na Mh. Heche ni pamoja na makamanda wafuatao: Mh. Mnyika, Tundu Lissu, Mh. Zitto, Halima Mdee na Mr Sugu. Kabla ya Mkutano huo kutakuwa na shughuli za uzinduzi wa Matawi na kusimika misingi ya CHADEMA kwenye mitaa yote ya Kata ya Kimara.
Aidha, kwenye Mkutano huo wa hadhara Mh. Heche anatarajiwa kuzindua Tawi la Mavurunza pamoja na harambee kwa ajili ya ofisi ya Tawi hilo, kupokea wanachama wapya na kuhutubia wanachama, wadau na wananchi kwa ujumla akipewa support ya nguvu kutoka kwa makamanda atakoambatana nao. Hakika CHADEMA itatikisa tena Kimara, Mtaa wa Mavurunza
Hivyo, ukiwa kama mwanachama au mdau muhimu wa CHADEMA, unaombwa kuhuduria mkutano huo muhimu sana bila kukosa.

Nawasilisha……
 
Kimara+CDM = 1
Asilimia kubwa ya wakazi wa Kimara ni Wachaga...mikutano yote ya CDM lazima ifanyikie kule!
 
Kimara+CDM = 1
Asilimia kubwa ya wakazi wa Kimara ni Wachaga...mikutano yote ya CDM lazima ifanyikie kule!
sio kweli kabisa, kimara kuna mchanganyko wa makabira mengi sana. Kwa taarifa yako mimi sio mchagga lakini ni mwanachama. No research No right to Say, umiza ubongo, usilale
 
Kimara+CDM = 1
Asilimia kubwa ya wakazi wa Kimara ni Wachaga...mikutano yote ya CDM lazima ifanyikie kule!

Ndiyo tuseme hao wachaga wanadhamini mikutano ya Chadema tu? Ukabila si mzuri kwa Nchi inayokua kama Tanzania, mwingine akisoma hii thread yako, tayari kashajua wewe uko upande gani...
 
sio kweli kabisa, kimara kuna mchanganyko wa makabira mengi sana. Kwa taarifa yako mimi sio mchagga lakini ni mwanachama. No research No right to Say, umiza ubongo, usilale

Makabira = Makabila!
 
ngome ya chademu ni kimara,wakazi wake wengi wachaga,haina noma wakina kimario,masawe kwa wiiingi.Pombe kwa sana jamaa wa grosari watauza sana
 
Back
Top Bottom