CHADEMA kususa ziara na vikao

CHADEMA kususa ziara na vikao

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesusia ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika manispaa za Temeke, Kinondoni na Ilala na kuthibitisha kutoshiriki katika kikao cha bodi ya barabara kinachotarajiwa kufanyika kesho.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesusia ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika manispaa za Temeke, Kinondoni na Ilala na kuthibitisha kutoshiriki katika kikao cha bodi ya barabara kinachotarajiwa kufanyika kesho kwa kile wanachodai kushinikiza kuachiwa kwa madiwani na mbunge ambao wanashikiliwa na jeshi la polisi.

Akielezsea hatua hiyo Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob amesema kuwa hawaoni sababu ya kuendelea na vikao mbalimbali vya jiji wakati hawajui hatma ya wenzao ambao mpaka sasa wanashikiliwa na polisi na wengine wanaitwa kufika kituoni hapo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kusababisha fujo katika zoezi la uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam.

Kikao kikubwa cha kujadili mipango ya maendeleo ya jiji la Dar es Salaam kinatarajiwa kufanyika kesho ambapo mada kuu itakuwa ni ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
ccm walitangaza Zuio feki la Mahakama makusudi wakitengemea Ukawa watalipinga ili wawabambikiwe Kesi , hizo njama za kuwabambikia kesi Ukawa ni bora wangepeleka malalamiko Yao kwenye Taasisi za haki za binadamu Duniani pia wafungue kesi The Hague ili wale woote walioshiriki kuwanyanyasa washitakiwe na kuwa fundisho Kwa Udikteta unaoanza kushika kasi kwenye awamu hii ya tano.
 
Bila Meya?
Unaelewa chochote kuhusu ngazi za maamuzi?
meya wa zamani bado yupo madarakani anapiga pesa kimya kimya Kwa kisingizio cha kumsubiri meya mpya wakabidhiane Ofisi .
 
kwa figisufigisu zinazoendelea dar kuhusu uchaguzi wa umeya na kamatakamata kwa wabunge na madiwani wa ukawa. chadema na ukawa wanapaswa kuchukua maamuzi magumu ya kuushirikisha umma....
Pia waende kwenye Mahakama ya uhalifu wa kimataifa The Hague wawashitaki polis pamoja na Yule mama aliyetangaza Zuio la Uongo toka mahakamani.
 
Naona kwa mara ya kwanza Rais wa awamu ya tano atakuwa madarakani kwa muhula mmoja tu.Naona kama vile January atakuwa mgombea wa kijani na Edo upande wa wananchi.
Huo Udikteta wake ndipo unamwelekeza maana unyanyasaji ukizidi utapunguza wapiga kura
 
Sijawahi ona chama cha hovyo kama chadema,kuswekwa ndani mdee,na kususia ukaguzi wa miradi wapi na wapi.
Hizo manispaa mlizozitwaa mtaziongoza vipi huku mnasusa.
mnasusa vikao vya bodi ya barabara?hao wabunge wenu watapewa vipi barabara za majimbo yao wakiwa wamesusa
Chadema ni full maigizo,manyumbu yanafuata mkumbo,mbinu zoote za kutafutia cha kuandamana zimezibwa,sasa wanaegemea umeya
Chadema acheni kuishi kwa matukio,mnalia kunyongwa kwa demokrasia wakati chama chenu hadi sasa kimebaka demokrasia,hakuna katibu mwezi wa sita huu halafu mnataka tuwape nchi
 
kwa figisufigisu zinazoendelea dar kuhusu uchaguzi wa umeya na kamatakamata kwa wabunge na madiwani wa ukawa. chadema na ukawa wanapaswa kuchukua maamuzi magumu ya kuushirikisha umma....
Pumba..umma ufanye nin sasa hapo?akili ndogo
 
Nini kitatokea wakisusa? Je kuna athari yeyote naomba kupewa somo
 
Pia waende kwenye Mahakama ya uhalifu wa kimataifa The Hague wawashitaki polis pamoja na Yule mama aliyetangaza Zuio la Uongo toka mahakamani.

Hapana Wangeenda Mahakamani Kuomba Hakimu atoe amri ya Kukamatwa Huyu Malaya wa Kiwete aliyetumia Jina la Mahakama Kwa Uwongo. (Najua Kwanini Namtuhumu Kikwete kweye Kila Uhuni wa CCM, Mtakuja Kujua)
 
Wanatumia vyombo vya usalama vibaya
Hivi inawezekanaje vyombo vya usalama ambavyo vinaendeshwa kwa kodi zetu sisi wananchi bila kujali itikadi zetu za kisiasa, kutumika vibaya kiasi hiki na watawala wa CCM?

Hao polisi kama kweli wangekuwa wanafanya kazi yao kwa weledi kama ambavyo maadili ya kazi zao zinavyowataka kufanya, wangepaswa kwanza kumtia mbaroni huyo msimamizi wa uchaguzi wa Meya la jiji la Dar, mama Mmbando ambaye imethibitika pasipo shaka yoyote kuwa alitumia zuio feki la kuzuia kufanyika uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar siku hiyo ya Jumamosi.

Polisi wamhoji ili wajue hilo suala la kutumia zuio feki ilikuwa ni amri kutoka kigogo mmojawapo mkubwa kutoka ndani ya CCM au ilikuwa ukereketwa wake binafsi kwa chama tawala?

Ikionekana huyo mama ana kesi ya kujibu aburuzwe mahakamani ili suala hilo liwe fundisho kwa watumishi wote wa Umma ambao wana kawaida ya kuonyesha ukereketwa wao kwa CCM waziwazi wakiamini nchi yetu bado ipo katika mfumo wa chama kimoja, mfumo ambao Taifa letu lilishaondokana nao tokea mwaka 1992.
 
Hili suala la kuvurugika kwa uchaguzi wa Umeya wa jiji la Dar, kulikofanywa kwa makusudi na huyo RAS, mama Theresia Mmbando ndiyo utakuwa mtihani mkubwa wa kwanza wa Rais Magufuli, kama utumbiaji wake wa majipu huwa una upendeleo.

Baada ya mahakama ya Kisutu kuthibitisha kuwa zuio la uchguzi wa Meya wa jiji la Dar siku ya tarehe 27/02/2016 lilikuwa feki ni dhahiri hatua inayopaswa kuchukuliwa hivi sasa na vyombo vya dola ni kumkamata huyo mama Theresia Mmbando na kumweka ndani na baadaye kumfungulia mashitaka ya jinai mahakamani.

Kama huyo mama ataendelea kuwa 'uraiani' na ataendelea kuwa kazini ni dhahiri Umma wa watanzania utaanza kutia shaka kauli ambazo mara nyingi amekuwa akitoa Rais Magufuli kuwa yeye anamuogopa Mungu sana na hawapendi watu wanafiki, akimaanisha watu waongo waongo.

Vile vile mara nyingi Rais Magufuli amesikika mara kadhaa akisema yeye atawatumikia wananchi wote bila kujali itikadi zao za kisiasa.

Amekuwa akifafanua kuwa yeye yuko tayari hata kufanya kazi na vyama vyote vya siasa pamoha na vya upinzani.

Sasa ndiyo tunataka kuona uhalisia wa kauli yake ambayo huwa anaitoa kuwa yeye ni msema kweli na anamuogopa sana Mungu.

Hili suala la Umeya liko wazi kabisa kuwa figisu figisu zote zinazotokea ni kutokana na CCM kutotaka kukubali Umeya huo kwenda kwa Ukawa ingawa hesabu za wabunge na madiwani walionao hapa jijini haziwezi kuwabeba kupata Meya toka CCM.

Sasa hapa ndipo wananchi tutagundua kama kweli Magufuli ni msema kweli na anamuogopa Mungu kikweli kweli, basi tutarajie kauli toka kwake aruhusu uchaguzi huo ufanyike kwa haki bila figisu figisu zozote.

Iwapo Magufuli atalikalia kimya suala hili basi wananchi ambao tulishaanza kumpa sifa kemkem kuhuzu zoezi lake la utumbuaji majipu tuataanza kuwa na shaka kama zoezi hilo halitaweza kumkumba huyo mama Theresia Mmbando na tunaweza hata kuanza kuhisi kuwa pengine hata hilo zuio la uchaguzi wa Umeya lilikuwa na 'blessings' kutoka ofisini kwake.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesusia ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika manispaa za Temeke, Kinondoni na Ilala na kuthibitisha kutoshiriki katika kikao cha bodi ya barabara kinachotarajiwa kufanyika kesho.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesusia ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika manispaa za Temeke, Kinondoni na Ilala na kuthibitisha kutoshiriki katika kikao cha bodi ya barabara kinachotarajiwa kufanyika kesho kwa kile wanachodai kushinikiza kuachiwa kwa madiwani na mbunge ambao wanashikiliwa na jeshi la polisi.

Akielezsea hatua hiyo Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob amesema kuwa hawaoni sababu ya kuendelea na vikao mbalimbali vya jiji wakati hawajui hatma ya wenzao ambao mpaka sasa wanashikiliwa na polisi na wengine wanaitwa kufika kituoni hapo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kusababisha fujo katika zoezi la uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam.

Kikao kikubwa cha kujadili mipango ya maendeleo ya jiji la Dar es Salaam kinatarajiwa kufanyika kesho ambapo mada kuu itakuwa ni ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
WAKISUSA SAFI TU. MAANA SISI TUTAENDELEA MAANA HAKUNA NAMNA NYINGINE HAPO!!
 
2010 walidai wakaazi wa Arusha mjini ni wakorofi na wamechagua kiongozi kichaa,

Asante sana ni baada ya miaka mitano tumejua ukweli. Kwamba walikataa kuchagua kichaa ndo maana ikawa vile kama ilivyo kwa wakazi wa Dar es Salaam Leo hii.

Poleni sana wakaazi wa bandari Salama.
 
Miaka mitano itakatika hakuna mlichowafanyia wananchi.kazi kupiga siasa.
 
ccm walitangaza Zuio feki la Mahakama makusudi wakitengemea Ukawa watalipinga ili wawabambikiwe Kesi , hizo njama za kuwabambikia kesi Ukawa ni bora wangepeleka malalamiko Yao kwenye Taasisi za haki za binadamu Duniani pia wafungue kesi The Hague ili wale woote walioshiriki kuwanyanyasa washitakiwe na kuwa fundisho Kwa Udikteta unaoanza kushika kasi kwenye awamu hii ya tano.
Dogo acha ujinga...The hague?
 
Kama chadema hawakufanya maandamano kupinga kupokwa ushindi wa urais, huu unaweza ukawa ni muda muafaka??? Nijuzeni wadau
 
Back
Top Bottom