CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi

Kiukweli tulikuwa tunaidharau jf, lakini amini usiamini, mabandiko kama haya, yamesaidia saidia, huwezi jua!. Zamani nilikuwa napitia mabandiko yako kwa dharau na kujibu kwa kejeli, lakini baada ya uteuzi, sasa napitia mabandiko yako yote kwa makini zaidi, heshima na adabu haswa kwa kuzingatia wewe sasa ndio bosi wangu kwenye tasnia ya habari.

Karibu Boss, Mheshimiwa saba, Bi Juliana Shonza.

Paskali.
 
Paskali: lazima lakini na wewe ukiri kuwa kuna wakati wanaonewa. Ona hapa:

 
Mkuu pascal kama nakuona ulivyompole....Tuiombee JF idumu milele..

Asije na yeye akawa kama Nappe kutetea sheria kandamizi na uhuru wa kujieleza wakati yeye alijiachia humu JF hadi amefika ngazi ya uheshimiwa sana...

Mafanikio ya Shonza hayawezi kutosha bila kuihusisha JF, ana mada nyingi humu zilizochangia kumfikisha hapo alipo.

Tumwombee awe mshauri mzuri kwa Boss wake Mwakyembe asiwe na munkari sana na vyombo vya habari hasa mitandao ya kijamii.

Yote kwa yote tumtakie mafanikio mema azidi kusonga mbele kulingana na juhudi zake...!
 
Yule mchungaji anasema wao upinzani kazi yao ni kuitia chuki kwa wananchi kuichukia govt
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…