Sera ya Elimu ya CDM inasema kwamba, katika msamiati wa lugha ya Kiswahili hatuna neno IVI, bali HIVI. Ufisadi katika elimu, umesababisha kuwepo kwa wahitimu wapuuzi wasioweza hata kuongea lugha ya Taifa kwa ufasaha.
Kuhusu kilimo CDM inaamini kuwa, kubadili badili majina ya kampeni za kwenye makaratasi ambazo hazitekelezeki hakuleti tija kwa kilimo. Kilimo Kwanza, Kilimo UTI wa Mgongo sijui mbavu, hakuleti mabadiliko shambani. Mabadiliko shambani yataletwa kwa elimu stahiki kwa wakulima, pembejeo kwa wakati na tija ya soko kwa mkulima badala ya kumnyang'anya mazao yake mara anapovuna.