CHADEMA kulitikisa taifa kwa mkutano wa kihistoria tarehe 24/07/2016 Jangwani

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinatarajia kufanya mkutano wa kihistoria ambao haujawahi kufanyika kwenye ardhi ya Tanzania. Mkutano huo mahsusi kumtambulisha katibu mkuu na kurungenzi zake, kutambulisha wabunge wao wapya waliochaguliwa nchi nzima, kutambulisha viongozi zaidi ya 300 waliokuwa Ccm kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana (2015) na kupokea wabunge 12 waliopewa adhabu za kinyama bungeni.

Mazungumzo yanaendelea kumkaribisha Julius Malema mbunge ambaye amepata misukosuko mingi bunge la Afrika ya Kusini ambayo inafananishwa na misukosuko wanayopata sasa wabunge wa upinzani Tanzania. Pia watahudhuria wawakilishi wa vyama vya upinzani wa nchi za Kenya na Uganda.

Mambo yakienda kama yalivyopangwa watapokelewa vigogo wengine kadhaa toka Ccm ambao watatangaza kumfuata rafiki yao Lowassa siku chache kabla ya mkutano mkuu wa Ccm uliopangwa kufanyika tarehe 23 mwezi huu.

Vituo karibu vyote vya TV vitakuwa live siku nzima na kwa kuwa matukio ni mengi ratiba itaanza asubuhi.
 
Nimeanza kuzigopa siasa za bongo.. Unaweza ukapandishwa cheo harakaharaka .. tusubiri tuone
 
...

Mambo yakienda kama yalivyopangwa watapokelewa vigogo wengine kadhaa toka Ccm ambao watatangaza kumfuata rafiki yao Lowassa siku chache kabla ya mkutano mkuu wa Ccm uliopangwa kufanyika tarehe 23 mwezi huu.a
Kama wanamfuata Lowassa, na wala siyo kuja kutekeleza/kufuata /kutii sera, katiba, kanuni, mipango ya Chadema ambayo imejikita kumkwamua mtanzania kutoka kwenye lindi la umasikini, utegemezi na mengine kama hayo!!! Hao kwa kweli ni 'liabilities' kwa chama wala si "assets ". Tutafakari!!
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinatarajia kufanya mkutano wa kihistoria ambao haujawahi kufanyika kwenye ardhi ya Tanzania. Mkutano huo mahsusi kumtambulisha katibu mkuu na kurungenzi zake, kutambulisha wabunge wao wapya waliochaguliwa nchi nzima, kutambulisha viongozi zaidi ya 300 waliokuwa Ccm kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana (2015) na kupokea wabunge 12 waliopewa adhabu za kinyama bungeni.

Mazungumzo yanaendelea kumkaribisha Julius Malema mbunge ambaye amepata misukosuko mingi bunge la Afrika ya Kusini ambayo inafananishwa na misukosuko wanayopata sasa wabunge wa upinzani Tanzania. Pia watahudhuria wawakilishi wa vyama vya upinzani wa nchi za Kenya na Uganda.

Mambo yakienda kama yalivyopangwa watapokelewa vigogo wengine kadhaa toka Ccm ambao watatangaza kumfuata rafiki yao Lowassa siku chache kabla ya mkutano mkuu wa Ccm uliopangwa kufanyika tarehe 23 mwezi huu.

Vituo karibu vyote vya TV vitakuwa live siku nzima na kwa kuwa matukio ni mengi ratiba itaanza asubuhi.
Daaa hii habari ni chungu sana kwa upande wa pili maana hata kule dodoma hawatakuwa na amani
 
Back
Top Bottom