CHADEMA kukutana Mlimani City ni matumizi mabaya ya Ruzuku ambazo ni kodi za watanzania ina maana hawana Ofisi mpaka wafanyie kikao Mlimani City?!!

CAG wako huyo kashindwa kufuatalia bei za ndege zinazo nunuliwa kama mapalachichi ya ngara , kashindwa kufuatilia hela zinazo mwagwa mtaani kila anapodhulu mkuu wetu wa nchi . utasikia mpen huyo mama million mbili , wapeni wasabi million 100 ,mpen mtoto million 5 ,hivi zinatoka wapi ? Ndege etu sa hivi inashikiliwa Canada hatujui mpka mda hatima yake .Halafu jitu limoja linasikika kutoka pangoni CAG afuatilie ruzuku ya chama pinzani. Hivi ww umelogwa na pesa za mgao?
 
Sasa kwani na wao wana moyo wa plastiki mpaka waogope kupanda ndege?akili zimekuishia,kwani unafikiri yeye kwenda na gari anapenda?moyo ndio shida.
Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Sisi kama wananchi?! Wewe na nani?!
 
Tuache Matusi tujadili hoja

Rais akisaidia Wananchi wewe unaumia nini?

Ndege zikinunuliwa ni kwa ajili ya kuinua uchumi wa Tanzania

Lkn hii fedha inayotafunwa na chadema ni sahihi ?
 
Ila CDM hawana sababu yoyote ya kwenda huko kushirikiana na bloodsucker na atawananga kweli live wakitoka huko waanze kulalamika, maana jiwe lazima atumie opportunity ya kuwepo kwao kuwananga na kujikweza na kuwaonyesha wafadhili wa n'je kuwa tz hakuna political crisis , sijui wanaenda kufanya nini?
 
Tumekusikia bwana mkubwa bila kusema Chadema hamlali walioiba hela za EPA mbona hamwambii CAG awakague
 
Rais Mstaafu Benjamin W Mkapa amekiri kabisa kuwa CCM iliiba fedha za EPA kugharamia uchaguzi.

Pia CCM haohao wanatumia magari ya Umma kwenye chaguzi na CCM haohao wanatumia mali za Umma kufanyia mikutano yao ya chama tena bila aibu wanatumia hadi Ikulu mahali ambapo Mwasisi wa Taifa hili alipaita Patakatifu.

Then chadema kutumia euzuku ya chama kugharamia ukumbi unaita matumizi mabaya ya dedha za Umma???

Punguza mahaba na CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…