jaruri
JF-Expert Member
- Jul 16, 2014
- 717
- 459
Nimemsikia mwanasheria mkuu wa CDM akisema kuwa wao kama chama walimuunga mkono mgombea wa urais kupitia chama tawala nchini kenya na kwamba kimsingi wamefurahishwa na ushindi wake wa urais nchini humo.
Ifahamike kuwa uchaguzi huu umekuwa na dosari kadhaa kabla na wakati wa uchaguzi. Dosari ambazo huku kwetu hazijawahi tokea. Siku chache kabla ya uchaguzi, mkuu wa IT wa tume ya uchaguzi nchini humo aliuawa kinyama.
Inasemekana mtu huyu ndie alokuwa na password ya data base za IT na kifo chake kimehusishwa na uchaguzi huu.Ilipofika siku ya uchaguzi upinzani uligundua kutokea kwa udukuzi katika data base ya IEBC na kutoa taarifa lakini hakuna hatua iliyo chukuliwa badala yake waliambiwa kuwa kama hawaridhishwi na matokeo waende mahakamani na tume ikaendelea kutangaza matokeo.
Swali fikirishi,kwa nini Musando afe siku chache kabla ya uchaguzi? na kwa nini muuaji achukue vidole vyake? Unaweza pata connection kuwa inawezekana kweli kuna mchezo mchafu ulifanyika kwenye data base ya IEBC though hatuna uhakika.
Wapinzani waliomba issue ndogo tu, waruhusiwe kuangalia taarifa za matokeo direct kwenye data base lakini walikataliwa.Kwa nini wakataliwe ? mimi na wewe hatujui
Maswali ninayo jiuliza;
unawezaje kumsupport mtu ambae wapinzani wanadai kaiba kura? Wewe ni mpinzani 2020 unatazamia kuingia kwenye vita kama alokua nayo mpinzani mwenzako leo,vipi huo wembe ulomyoa mwenzio leo ukikunyoa 2020, utalalamika?
Uchaguzi hauwi huru na haki kwa kuwaruhusu wafungwa na diaspora kupiga kura tu, bali unakuwa huru na haki katika hatua zote za uandikishaji, kampeni, upigaji wa kura, kuhesabu na kutoa matokeo.
Kwa hawa wenzetu kutokana na madai ya upinzani kulikwa na tatizo katika kuhesabu kura za urais ndio maana waliomba access katika data base za IEBC wakanyimwa. Jiulize kwa nini walinyimwa.
Mwisho niwashauri ndugu zangu hawa kabla hawaja toa matamko wawe wanafanya uchunguzi wa kutosha,si vema kutoa tamko leo afu kesho likakugharimu.
Wajifunze kutokana na makosa yao wenyewe:
-2008 lowasa fisadi;2015 wanamsafisha.
-2005-2015 Rais wa awamu ya nne dhaifu 2017 wanamsifia kuwa alikuwa rais bora sana
-Kabla ya 2015 walisema wanataka rais mkali atakae simamia nchi;leo Kaja JPM wanaanza kulia.
Free mind jaruri
0712207633